Tunga Sentensi ikianza na maneno "Tafuta Hela"

Tunga Sentensi ikianza na maneno "Tafuta Hela"

Hatupendi kuambina ukweli. Kuna ndugu yangu yeye alikuwa na tabia ya kukutafuta siku akiwa na shida tu. Kuna siku nikamwambia basi hata siku ukiwa na raha tutafutane sio siku ya shida tu. Alipotea mazima toka 2012 sijawahi wasiliana nae tena.
mwache aende Mungu mwenye amesema nikumbuke siku za ujana wako( ukiwa na nguvu), sio umezeeka na magongo ndo ujifanye katekisti
 
Acha kujitapa eti una hela! Utalogwa bure pengine hata hela huna,ulimbukeni tu unakusumbua
Kumbuka mwenye hela huwa hajitangazi Bali hutangazwa.
IMG_20230212_031009.jpg
 
Acha kujitapa eti una hela! Utalogwa bure pengine hata hela huna,ulimbukeni tu unakusumbua
Kumbuka mwenye hela huwa hajitangazi Bali hutangazwa.View attachment 2630027
Tafuta hela uache makasiriko. Kuombwa hela sio lazima uwe na billions kadhaa au millions kadhaa. Hata ukiwa na elfu 10 unaweza kuombwa tu. Acha makasiriko ndugu.
 
Mbali na semi nyingi zinazotrend kuhusu kutafuta hela kama vile..
1. Tafuta hela V8 sio gari ya serikali
2. Tafuta hela kitanda hakikai kwenye kona[emoji23]
3. Tafuta hela wanawake hawakai mbali na simu [emoji23]
Na nyingine kibao..

Hu usemi wa tafuta hela ndugu sio wachache nimeamini. Sina kiasi hicho ila namshukuru Mungu angalau kidogo naweza hata kula mara 3 kwa siku. Sasa ndugu zangu sijui wananionaje aisee. Unapigwa mizinga mpaka unatamani kuzima simu. Kwa siku lazima upokee simu 2 mpaka 4 sijui mie mtoto wa fulani, mie fulani, siku ya mwisho anataka hela imsaidie jambo fulani duh... ndugu zangu mie sina hela kihivyo maisha ni magumu kama lilivyo jina langu.
Tafuta hela uache kusumbua ndugu.
Pesa sio kila kitu kwenye maisha haya, kuna vitu muhimu pesa haiwezi kuvitatua kabisa.......huo usemi wa tafuta pesa ni wa limbukeni.
 
Back
Top Bottom