Synthesizer
Platinum Member
- Feb 15, 2010
- 12,699
- 22,598
Ni sehemu iko katika barabara ya Moshi kwenda Arusha. Kuna bonde kubwa na daraja na huko nyuma Wajapan walikufa kwa ajali mbaya na hata pamejengwa mnara wa kumbukumbu kwa ajili yao. Kutokana na uwepo wa daraja hili na bonde pamefanywa kuwa sehemu ambayo huruhusiwi ku-overtake na sasa trafiki wamepafanya mradi wa kutoza watu faini.
Trafiki wanakaaa upande wa kuelekea Moshi, wengine wanajificha katikati, na wengine wanakaaa upande wa kuelekea Arusha wa daraja. Ni sehemu ndefu sana katika sehemu hii ambayo huruhusiwi ku-overtake, japo upande wa kuelekea Moshi kuna sehemu ambayo barabara imenyooka sana na unaweza kuona mbali na ku-overtake bila hatari, bado huruhusiwi ku-overtake.
Uki-overtake sehemu hii basi utakuta trafiki wanakusubiri mbele upigwe faini kwa kuwa wapo waliojificha na kazi yao ni kuangalia gari inayo overtake na kuwaambia wenzao. Matokeo ni kwamba mara kadhaa sehemu hii inakuwa na misururu mirefu sana ya magari pande zote mbili, hasa kukiwa na lori linaloenda taratibu.
Sasa wiki iliyopita tulikuwa na msururu mrefu sana wa magari kuelekea upande wa Arusha. Mbele yetu kulikuwa na lori la mafuta. Tukawa tunalifuata nyuma taratibu. Tulivuka daraja na kuanza kupanda mlima kuelelekea Arusha. Ghafla lile lori lilionekana kuanza kuishiwa nguvu, likitoa moshi mwingi. Likaanza kurudi nyuma na kukawa na honi nyingi sana za kupanick toka magari yaliyokuwa nyuma. Upande wa pili kulikuwa na magari mengi tu na hivyo wote tuliokuwa nyuma ya hili lori hatukuwa na sehemu ya kukimbilia zaidi ya kupiga honi! Mbele ya uso wangu nikaona ajali mbaya sana inakuja!
Dereva wa lori kwa namna fulani alifanikiwa kulisimamisha lori lake, na baada ya kupiga less (revs) nyingi lilianza kwenda mbele tena.
Ilinifanya niwaze sana, kwa kuwa kama dereva wa lile lori asingefaniiwa kulidhidhibiti, lingerudi nyuma na kufagia magari mengi sana kuelekea mtoni! Na katika watu kujaribu kulikwepa kungekuwa na kugongana kwingi sana! Na hata nikawaza vipi lile lori lingeanguka na kumwaga mafuta na moto kuwaka? Basi kwa kuwa ile sehemu hakuna sehemu ya kukimbili, magari yote yaliyokuwa nyuma ya lile lori yangewaka moto!
Hapo ndipo nikafikiria, je uwepo wa polisi hizi sehemu tatu za barabara kweli unalenga kusaidia au kupata fedha? Serikali ya Tanzania imeona suluhisho ya uhatari wa sehemu hii ni kuweka askari ili kupiga faini watu wanao overtake hata kama mbele yako ni lori la mafuta linaloenda spidi ya 20km/hr?
Kama serikali imeliona eneo hili kuwa la hatari sana, kwa nini haijaweka climbing lanes pande zote mbili za daraja? Au serikali itaua mradi wa kupiga watu faini? Nafasi ya climbing lanes ipo ya kutosha, kwa nini hawajaweka? Je serikali inaona kuweka miundo mbinu ya kuzuia janga baya sehemu kama hii si jambo la haraka kuliko kujenga fly-over Dar es Salaam? Gharama ya kuweka climbing lanes pande zote mbili za hili daraja ni kubwa kiasi gani kiasi kwamba serikali isifanye hivyo kwa haraka? Je serikali inasubiri hadi ajali mbaya itokeee ndipo iamshwe kujenga climbing lanes?
Eneo hili kwa wakati wote linakuwa na askari wa trafiki karibu 20, ambao kama climbing lanes zingewekwa wangepelekwa sehemu nyingine kuangalia usalama badala ya kukaa hapa kutwa nzima wakisubiri watu wa kupiga faini kwa ku-overtake au kwenda zaidi ya 50km/hr!
Kuna maeneo hatarishi sana katika barabara zetu ambayo yameua sana na suluhisho lake ni kuweka climbing lanes. Hili lilifanywa katika barabara ya Dar- es-Salaam - Morogoro ambayo ilikuwa inaua kila siku na ajali zikakoma baada ya kuweka climbing lanes. Sehemu hii ya Moshi, na ile ya pale mlima wa Mbalizi Mbeya na nyinginezo ni maeneo hatarishi sana na suluhisho lake ni rahisi sana kuweka climbing lanes, lakini naona kama Tanroads wako busy kujenga flyover Dar es Salaam kwa kuwa zitaitwa kwa majina yao, bila kujali usalama wa raia katika maeneo hatarishi sana!