Lord denning
JF-Expert Member
- Jun 3, 2015
- 15,819
- 33,255
Dunia hailali. Kila siku watu wanaumiza vichwa vyao wafanyaje kukamata fursa ili kuwa na maendeleo makubwa kiuchumi.
Kenya anapambana akamate soko la mizigo la Uganda, Sudani Kusini , Ethiopia na baade Afrika ya Kati kupitia Sudani Kusini. (Kupitia mpango wao wa The Northen Corridor)
Wiki hii Waziri wa Miundombinu wa Uganda ametangaza wanaanza ujenzi wa reli (SGR) kutoka Malabo hadi Kampala. Huku Kenya anapambana kufikisha SGR yake Malabo kutoka Mombasa.
Sisi tunapeleka SGR hadi Burundi na kisha Congo (alafu tunalizika tu). Hivi tunashindwaje kuipeleka hadi kagera iingie Uganda alafu tupambane ifike hadi Sudani Kusini kabla ya Kenya?
Kama tungekuwa na Baraza la Mawaziri lenye akili zinazochaji kweli sasaivi nilitegemea tuwe na taarifa ya SGR kufika kagera mpaka wa Tanzania na Uganda alafu watu wanapambana iunganishwe hadi kufika Sudani Kusini.
Viongozi wetu wanalala sana. Ujinga wa Watanzania unawafanya wasiumize kichwa kufikiri kwa ajili ya kesho ya Tanzania zaidi ya Matumbo yao tu.
OMBI KWA RAIS SAMIA
Anzisha ujenzi wa Reli ya SGR kuelekea Kagera ifike hadi mpaka wa Tanzania na Uganda haraka iwekekanavyo kabla ya Kenya hajaanza kutekeleza ujenzi wa SGR Mombasa- Kisumu- Malabo.
Lord denning
Sinza, Dar es Salaam!