Tungekuwa na Baraza la Mawaziri sharp na smart tungekuwa tunaipeleka SGR Uganda kwa focus ya kuifikisha Sudan Kusini na Afrika ya Kati

Dunia hailali. Kila siku watu wanaumiza vichwa vyao wafanyaje kukamata fursa ili kuwa na maendeleo makubwa kiuchumi.

Kenya anapambana akamate soko la mizigo la Uganda, Sudani Kusini , Ethiopia na baade Afrika ya Kati kupitia Sudani Kusini. (Kupitia mpango wao wa The Northen Corridor)

Wiki hii Waziri wa Miundombinu wa Uganda ametangaza wanaanza ujenzi wa reli (SGR) kutoka Malabo hadi Kampala. Huku Kenya anapambana kufikisha SGR yake Malabo kutoka Mombasa.

Sisi tunapeleka SGR hadi Burundi na kisha Congo (alafu tunalizika tu). Hivi tunashindwaje kuipeleka hadi kagera iingie Uganda alafu tupambane ifike hadi Sudani Kusini kabla ya Kenya?

Kama tungekuwa na Baraza la Mawaziri lenye akili zinazochaji kweli sasaivi nilitegemea tuwe na taarifa ya SGR kufika kagera mpaka wa Tanzania na Uganda alafu watu wanapambana iunganishwe hadi kufika Sudani Kusini.

Viongozi wetu wanalala sana. Ujinga wa Watanzania unawafanya wasiumize kichwa kufikiri kwa ajili ya kesho ya Tanzania zaidi ya Matumbo yao tu.

OMBI KWA RAIS SAMIA
Anzisha ujenzi wa Reli ya SGR kuelekea Kagera ifike hadi mpaka wa Tanzania na Uganda haraka iwekekanavyo kabla ya Kenya hajaanza kutekeleza ujenzi wa SGR Mombasa- Kisumu- Malabo.

Lord denning
Sinza, Dar es Salaam!
Kwa biashara ipi ya south sudan?
 
Kwani SGR ya sasa inajengwaje Burundi?

Umeishia darasa la ngapi?

Hujui sisi tukiwahi kuifikisha SGR mpakani mwa Uganda na Tanzania kabla ya Kenya itasababisha Uganda na South Sudan wabadili mipango yao na kuja Tanzania hivyo Tanzania kufaidika zaidi?
Akili ya kuwaza kujenga jenga ilihali hata vilivyopo havijatumika ipasavyo ni kuongeza umasikini...kwa hiyo wewe unawafundisha Uganda na Sudan kusini kuona kile ambacho hawajakiona bado! wao wana vipaumbele vyao hata ufikishe reli mpakani km si kipaumbele kwao huwezi kuwafundisha! tumia kwanza miundo mbinu iliyopo kwa ufanisi wao ndio watakuomba ujenge hiyo reli!
 
Endelea kulamba asali. Mada za namna hii zimekuzidi sana uwezo
 
Kenya anapambana akamate soko la mizigo la Uganda, Sudani Kusini , Ethiopia na baade Afrika ya Kati kupitia Sudani Kusini. (Kupitia mpango wao wa The Northen Corridor)
Uliisoma jiografia vizuri na kuielewa; halafu ukaiunganisha na elimu yako ya uchumi?

Huko Sudan Kusini, Ethiopia unako maslahi gani kupeleka SGR ya Tanzania huko?
Utaachaje kupambania soko kubwa zaidi lililo mlangoni kwako hadi uende kubanana huko mbali?

Ndiyo, Uganda nisingemwacha pembeni, pamoja na kwamba Mombasa kwake ni rahisi, lakini huyu huwa anahangaishwa sana na huyo jirani yake kila mara.
Ningepitisha hiyo SGR huko Uganda nikipambania pia sehemu za kaskazini mwa DRC.

Rwanda, hana sababu yoyote ya kupeleka mizigo Mombasa, naye ningemtumia kunyoosha SGR hadi DRC na hivyo hivyo Burundi.

Lakini pia ningeweka juhudi zaidi za kumfikia DRC kupitia ziwani moja kwa moja; kwa kuwepo bandari mbili au zaidi kufikia eneo la katikakti na kusini mwa DRC
Zambia nisingemwachia Angola (Lobito) na Afrika Kusini. Huyu ningemvuta tu aje huku kwa kumfikishia reli yenye nguvu, hata hiyo TAZARA ingetengenezwa iwe na ufanisi zaidi.

Kwa nini Malawi, hasa sehemu ya Kaskazini na kati asivutwe kuja kwetu? Bandari yenye uwezo wa kuhudumia ziwani ingekuwa ni njia nzuri ya kumvuta, pamoja na reli ya TAZARA.

Lakini yote hayo yanategemea kuwepo na Bandari zenye uwezo wa kuhudumia maeneo yote haya kwa ufanisi.

Bagamoyo inatakiwa ianze kujengwa mara moja.
Tanga na barabara/Reli kwenda Musoma ni njia rahisi zaidi ya kumfikia Uganda

Ukiweza kuweka utando wa miundo mbinu hii, na kuhakikisha inafanya kazi vizuri, kwenda huko Afrika ya Kati na Kwingineko haiwezi kuwa ndoto tena.
 
Sifa za waziri.
1. Umri usizidi miaka 55
2. Awe na degree Ila asiwe na PhD. Awe na gpa ya angalau 4.0
3. Awe na mke mmoja na asiwe na nyumba ndogo Kama huyu..nanihii wa Jimbo la mkoa wa ..
4. Asiwe anampiga mke wake mpaka majirani wakajua.
5. Asiwe mlevi Wala mzinzi Wala mwizi. Aridhike na mshahara.
6. Awe na kitambi kiasi na awe anakula nyumbani kwake chakula alichopika mke wake.
7. Watoto wake wasome shule za serikali anayoitumikia.
8. Asiwe na watoto wa nje.
9. Asitembee na mwanamke wa ofisini kwake hata iweje.
10. Asinywe maji akiwa kwenye vikao.
 
Endelea kulamba asali. Mada za namna hii zimekuzidi sana uwezo
Pamoja na kutokubaliana naye kwa baadhi ya hoja yake, lakini kuna ukweli katika andiko lake hilo.

Kwa mfano hilo la "kuwaonyesha ufanisi" hao unaotaka watumie njia zako za usafiri.
 
nchi jirani iwe by the way tu kwamba itawafikia tukishafikisha reli kwa watu wetu kwanza …
Very Wrong Idea!

Kuunganisha mtandao wa ndani ni sahihi; lakini kusema "jirani iwe by the way", is absolutely wrong!

Hii ni biashara mkuu 'kijakazi", biashara ni lazima iingize faida ili miradi iweze kujiendesha yenyewe. Kusafirisha mizigo mingi toka nchi jirani, ikiunganishwa na hii ya humu humu ndani ndiyo biashara iliyo noga hiyo.
 
Kipaumbele Kwa Sasa ni zanzibar.hujasikia mama amesema wizara ya miundombinu waharakishe ujenzi wa daraja kuunganishwa Zanzibar?
Hilo Daraja nalipa jina leo hii" "Daraja la Chura Kiziwi" - legacy ya mama hiyo!

Hilo daraja liunganishwe ili Zanzibar iweze kuitawala vyema Tanganyika! Hiki kweli ni kipaumbele cha mama.
 
OMBI KWA RAIS SAMIA
Anzisha ujenzi wa Reli ya SGR kuelekea Kagera ifike hadi mpaka wa Tanzania na Uganda haraka iwekekanavyo kabla ya Kenya hajaanza kutekeleza ujenzi wa SGR Mombasa- Kisumu- Malabo.
Hapana.
Hizi zitakuwa ni papara ziso kuwa na malengo maalum.
Ndiyo, Uganda tunaweza kumvuta atumie "baadhi" ya mzigo yake huku kwetu; lakini kijiografia, yeye ni mtu wa Mombasa, 'naturally'. Kenya watakuwa wamejipotea sana kumwacha Uganda atangetange kwingineko. Sudan Kusini? Hapana.
 
Very Wrong Idea!

Kuunganisha mtandao wa ndani ni sahihi; lakini kusema "jirani iwe by the way", is absolutely wrong!

Hii ni biashara mkuu 'kijakazi", biashara ni lazima iingize faida ili miradi iweze kujiendesha yenyewe. Kusafirisha mizigo mingi toka nchi jirani, ikiunganishwa na hii ya humu humu ndani ndiyo biashara iliyo noga hiyo.

ni waafrika tu ambao hawaelewi uchumi wa nchi unajengwa vipi ndiyo hufikiria hivyo, ulishawahi kufika Afrika Kusini na kuangalia infastructure walioijenga kwa miaka mingi iliyopita, unafikiri walijenga kwa kutarget nchi jirani au walijenga kutarget nchi yao kwanza? kwa maoni yangu lengo la kwanza la any big infrastructure project ambayo inajengwa na walipa kodi iwe kuhudumia ndani ya tanzagiza mambo ya nchi jirani ni extra kama nchi xyz inataka kuunganishwa na infrastructure tunaweza kushare cost waweke mezani kiasi kadhaa na sisi tuweke kiasi kadhaa tukubaliane tujenge lkn siyo sisi kufund reli maelfu ya km eti kwa ajili tu ya kuhudumia foreign country hiyo kwa maoni yangu siyo sahihi na huwezi kujenga uchumi wa nchi hivyo …
 
Hapana.
Hizi zitakuwa ni papara ziso kuwa na malengo maalum.
Ndiyo, Uganda tunaweza kumvuta atumie "baadhi" ya mzigo yake huku kwetu; lakini kijiografia, yeye ni mtu wa Mombasa, 'naturally'. Kenya watakuwa wamejipotea sana kumwacha Uganda atangetange kwingineko. Sudan Kusini? Hapana.
Maisha ni fursa. Dunia ya sasa kwenye maendeleo hakuna kuoneana huruma
 
ni waafrika tu ambao hawaelewi uchumi wa nchi unajengwa vipi ndiyo hufikiria hivyo, ulishawahi kufika Afrika Kusini na kuangalia infastructure walioijenga kwa miaka mingi iliyopita, unafikiri walijenga kwa kutarget nchi jirani au walijenga kutarget nchi yao kwanza? kwa maoni yangu lengo la kwanza la any big infrastructure project ambayo inajengwa na walipa kodi iwe kuhudumia ndani ya tanzagiza mambo ya nchi jirani ni extra kama nchi xyz inataka kuunganishwa na infrastructure tunaweza kushare cost waweke mezani kiasi kadhaa na sisi tuweke kiasi kadhaa tukubaliane tujenge lkn siyo sisi kufund reli maelfu ya km eti kwa ajili tu ya kuhudumia foreign country hiyo kwa maoni yangu siyo sahihi na huwezi kujenga uchumi wa nchi hivyo …
Ni hoja nzuri. Miundombinu inapaswa kuwa mahali pote kwa kurahisisha uzalishaji nchi nzima.

Ila kwa faida kubwa lazima tutoke na nje ya nchi maana huko ndo kuna faida kubwa
 
Kijakazi , ana hoja,

Wakati mwingine huwa naona sisi Watanzania ni kama hatujui tunaka mambo makubwa ili iweje,

Kijakazi anavyozungumzia reli ihudumie Tanzania na baadaye kwenda huko nje , ni kwamba kawaza kwa kuona mbali ,

Kwa nini sisi tumedumaa sana ktk kuzalisha mizigo yetu wenyewe?,

Hivi Tanzania leo tukirudi kama pale nyuma tulipokuwa tukizalisha mazao yetu ya kwenda nje, nikiyataja kama, Pamba, kahawa, katani, kuongezea na mifugo mahindi, nk. Je hii reli haitatufaa,

Tatizo tumerudi nyuma sana kiuzalishaji, akili zetu sasa zipo ktk uchuuzi,

Kwa uzalishaji wetu wa leo ni bora tungeboresha reli yetu ya zamani tu,

Kwa matrilioni tuliyotumia kwa SGR, nadhani tungetumia robo ya kiasi hicho kurekebisha reli ya zamani , ingekuwa poa sana,

Hata kwa kuongeza matawi mengine kama ya Mtwara to Songea,

Tunataka mambo makubwa , wakati madogo yanatushinda.
 
ni waafrika tu ambao hawaelewi uchumi wa nchi unajengwa vipi ndiyo hufikiria hivyo, ulishawahi kufika Afrika Kusini na kuangalia infastructure walioijenga kwa miaka mingi iliyopita, unafikiri walijenga kwa kutarget nchi jirani au walijenga kutarget nchi yao kwanza?
Hili kamwe haliwezi kuwa jambo la mjadala mrefu, kwa sababu sote tunaelewa umuhimu wa kuwa na network nzuri ya kusafirisha mizigo, iwe ya ndani au/na nje.

Sasa nikuulize, hiyo South Africa uliyo tolea mfano; Zambia na Zimbabwe mizigo yao mingi hadi hii leo inapitia wapi?
Sawa, walijenga wakilenga kurahisisha usafiri wa nchi yao; lakini hilo halikuzuia kuhusisha mizigo ya nchi jirani zenye uhitaji.
Nasi tujenge, na kwa kweli ujenzi wetu ni tofauti na huo wa makaburu enzi za wao wakiwa wanajiona ni taifa linalotakiwa kujitosheleza kwa karibu kila kitu, kutokana na siasa zilizokuwepo.

Reli ya Kenya ilipoishia Naivasha, matazamio yake ya kuingiza faida na kujilipa gharama za ujenzi ilianza kuwa ngumu. Reli hiyo uwepo wa Uganda ndio uliokuwa ukiiongezea nguvu. Ndiyo maana sasa wanahaha tena kuipeleka hadi Uganda.
Biashara ya usafirishaji ni kuwa na mizigo mingi; na kadri ya nchi zinavyo ongezeka, mizigo nayo inaongezeka, na faida inapatikana.
Kwa hiyo, ni sahihi, kwamba nasi tunataka hiyo reli itusaidie kurahisisha usafiri wetu; lakini reli hiyo hiyo itafana zaidi wakipatikana na wengine wenye uhitaji wa kuitumia. Hili liko wazi kabisa.
Na kumbuka, siyo reli pekee itakayotunufaisha, bandari zetu nazo zitanufaika. Sasa hapo shida iko wapi?
yao kwanza? kwa maoni yangu lengo la kwanza la any big infrastructure project ambayo inajengwa na walipa kodi iwe kuhudumia ndani ya tanzagiza mambo ya nchi jirani ni extra kama nchi xyz inataka kuunganishwa na infrastructure tunaweza kushare cost waweke mezani kiasi kadhaa na sisi tuweke kiasi kadhaa tukubaliane tujenge lkn siyo sisi kufund reli maelfu ya km eti kwa ajili tu ya kuhudumia foreign country hiyo kwa maoni yangu siyo sahihi na huwezi kujenga uchumi wa nchi hivyo
Binafsi sidhani kuwa kujenga reli yetu ni kwa sababu ya nchi hizo nyingine. Sijapata kuona popote ikielezwa kuwa ujenzi wa reli ni kwa sababu ya nchi jirani. Tunajenga tupate nafuu ya usafiri; lakini kama fursa ipo ya kupata faida maradufu kwa kuhudumia nchi jirani shida hapo ipo wapi?
Reli pekee ninayojua ilijengwa ikiwa na lengo la moja kwa moja kuhudumia jirani, ni hiyo TAZARA, na ilieleweka; lakini pamoja na hayo reli hiyo ilikuwa ni kwa matumizi yetu pia.

Leo hii unajenga reli kuelekea Magharibi, halafu usione fursa tele zilizopo kwa majirani, ili zikupe sababu zaidi za kutimiza malengo yako mawili, ndani na nje; wewe utakuwa mtu wa namna gani?
 
Dunia hailali. Kila siku watu wanaumiza vichwa vyao wafanyaje kukamata fursa ili kuwa na maendeleo makubwa kiuchumi.

Kenya anapambana akamate soko la mizigo la Uganda, Sudani Kusini , Ethiopia na baade Afrika ya Kati kupitia Sudani Kusini. (Kupitia mpango wao wa The Northen Corridor)

Wiki hii Waziri wa Miundombinu wa Uganda ametangaza wanaanza ujenzi wa reli (SGR) kutoka Malabo hadi Kampala. Huku Kenya anapambana kufikisha SGR yake Malabo kutoka Mombasa.

Sisi tunapeleka SGR hadi Burundi na kisha Congo (alafu tunalizika tu). Hivi tunashindwaje kuipeleka hadi kagera iingie Uganda alafu tupambane ifike hadi Sudani Kusini kabla ya Kenya?

Kama tungekuwa na Baraza la Mawaziri lenye akili zinazochaji kweli sasaivi nilitegemea tuwe na taarifa ya SGR kufika kagera mpaka wa Tanzania na Uganda alafu watu wanapambana iunganishwe hadi kufika Sudani Kusini.

Viongozi wetu wanalala sana. Ujinga wa Watanzania unawafanya wasiumize kichwa kufikiri kwa ajili ya kesho ya Tanzania zaidi ya Matumbo yao tu.

OMBI KWA RAIS SAMIA
Anzisha ujenzi wa Reli ya SGR kuelekea Kagera ifike hadi mpaka wa Tanzania na Uganda haraka iwekekanavyo kabla ya Kenya hajaanza kutekeleza ujenzi wa SGR Mombasa- Kisumu- Malabo.

Lord denning
Sinza, Dar es Salaam!
Ila Wabongo bana mna Maneno mno
 
Kijografia kwetu tunaweza kufanya vizuri kwa miaka mingi kama tutafikisha SGR burundi then DRC..
 
Back
Top Bottom