ngosha wa mwanza
JF-Expert Member
- Feb 23, 2015
- 3,832
- 11,964
Shida ni viongozi kua wafanya biashara hapo ndo shida inaanza wananunua milori, mabasi utegemee waje na wazo la kuua biashara zao.lakini km tunapata wazarendo hasa nchi hii ingekua haikopi ovyo wala wananchi tusingekua na kodi na tozo kandamizi.Bandari zetu zote zinaweza kuwa busy 24/7 tukilifanya hili.
Hii nchi imekaa kwenye eneo zuri sana kijiographia shida Katiba yetu inasababisha tuwe na viongozi wa hovyo sana kiasi ambacho tunaenda mwendo wa kinyonga
Marekani Viongozi wote wana mabishara makubwa mbona hatuoni waki sabotage mipango mizuri ya nchi yao kwa sababu ya biashara zao.Shida ni viongozi kua wafanya biashara hapo ndo shida inaanza wananunua milori, mabasi utegemee waje na wazo la kuua biashara zao.lakini km tunapata wazarendo hasa nchi hii ingekua haikopi ovyo wala wananchi tusingekua na kodi na tozo kandamizi.
Una wazo zuri ila reli kwa faida kubwa ni vizuri isafirishe both mizigo inayotoka ndani na nje ya nchi. Focus iwe mizigo ya nchi na nchi.
Sie ndio lango la kwenda Asia, Australia na Ulaya kwa ukanda huu. Tukiweza kulitumia hili vizuri tutafaidika sana!
Una hoja nzuri sana.ukifanya hivyo kwa maoni yangu unajenga utegemezi ambao in the long run ni hatari kwa kwa uchumi wako ikitokea vita hizo nchi unafanyaje? bandari inakufa au? kuna change of leadership kwenye hizo nchi ulizojenga utegemezi wa reli na bandari yako wakatafuta altenative na altenatives zipo siku zote tena nyingi tu tuliona tazara kwa nini ilikufa? moja kati ya sababu kuu ni kwamba ilijengwa kwa lengo moja tu kusafirisha shaba ya zambia kwenda China kupitia bandari yetu kipindi hicho Msumbiji, Angola na hata AK hali ya kisiasa haikuwa rafiki na China sababu ya cold war ndiyo dar ikawa kama option sasa leo hii Zambia
anatumia bandari nyingine pia za kusini kusafirisha shaba kwenda China uhitaji wa reli ya tazara na bandari yetu umepungua.
hivyo binafsi naona ni bora kujenga kwetu kwanza tuna mengi ya ku export eneo lote la kusini mikoa ya morogoro, iringa mpaka mbeya kuna resources nyingi sana ambazo ujio wa infrastructure bora unaweza kuleta uwekezaji mkubwa na kuexport kutumia reli yetu, huko Ifakara tu kilimo cha kisasa kinaweza kufanya export kubwa kutumia reli, ngano inayolimwa Manyara na kwingineko huko kaskazini tukiwekeza zaidi na wangepata infrastructure imara ingesaidia exports kuna nchi zinaishi kwa kuuza ngano tu for export, tuna mambo mengi tunaweza kufanya kutumia bandari zetu tuna coal deposits kubwa huko ziwa nyasa ingeunganishwa na reli mpaka bandarini uwekezaji mkubwa ungefwatia, you see tuna homework kubwa ndani ya nchi yetu bila ya kutegemea foreigners ofcourse they are (foreigners) welcome lkn haipaswi kuwa lengo kuu kwamba tunajenga infrastructure kwa mabilioni kutarget nchi za nje kwangu siyo sahihi kama tunaangalia mbele miaka 20-50 huko …
Nchi hii tunaongozwa na misukule. Border ya Tunduma inaingiza pesa nyingi sana lakini kupanua barabara hata kwa 30km tuu imekua changamoto. Tunasubiri mradi wa wa EPC + F kutoka Igawa- Tunduma 200+ km dual carriageway ambao sidhani kama utakamilika before 2030.
Zambia na DRC wanatuvumilia tuu kwa sababu hawana option nyingine ila foleni ya malori Tunduma inaepukika kwa nchi inayojielewa.
Pia wale ni wazalendo wanaipenda inchi yao huku viongozi wanaiba kama wanakomoa wakati hawajui wana vizazi vyao vinatakiwa vije vifaidike lakini wao wanaaangalia hapa hawaoni kesho .Kama anakuja kiongozi aamue kuwafilisi viongozi nafikiri hela walio iba inaweza kulipa deni lote la taifa 😂Marekani Viongozi wote wana mabishara makubwa mbona hatuoni waki sabotage mipango mizuri ya nchi yao kwa sababu ya biashara zao.
Shida kwenu ni ubinafsi, ujinga, kutokuwa na akili na exposure!
Sijategemea maoni haya kutoka kwako nguli Bufa!Bongo kwenyewe bado SGR haijaanza mjue ufanisi wake. Afu Sio nyie mnaolalamika tayari bei za huduma SGR zipo juu?
Huko Congo na Burundi imefika tayari? Kama bado kwanini ukimbilie kwingine wakati hata malengo yako hayajatimia? Ndo maana hata biashara za nyanya zinawashinda.
Wabongo mnapenda ulalamishi bila kuwaza mambo mengine.
Afu hao kenya mnaoshinda kuwasifia kila kitu hata wakijamba nao wana challenges zao ambazo nyie mitanganyika huwa hamuoni sababu ya inferiority complex yenu. Nyie mnajua kusifia tu anything Kenyan.
Kenya’s SGR Drives Up Debt, Falls Short on Profits - Africa Defense Forum
ADF STAFF Kenya’s Chinese-built Standard Gauge Railway (SGR) was supposed to be an economic engine for East Africa, linking the middle of the continent to the port at Mombasa. Instead, the SGR has become a financial burden that consumes an ever-increasing chunk of the nation’s revenue. Although...adf-magazine.com
Sijategemea maoni haya kutoka kwako nguli Bufa!
Kwa sasa tupo kwenye hatua za kufanya. Potential tayari ipo na kila mtu anaiona. Tunashirikiana vizuri na Burundi na tayari wamesha secure a loan kujenga hii SGR itakayofika hadi Kigoma.
Kwa sasa tunaenda kwenye Africa Free Trade Area. Moja ya maeneo nyeti ni miundombinu na atakayefanikiwa kuweka miondombinu yake kwa haraka zaidi ndiye atakayefanikiwa zaidi.
Tukisema tusubiri kuona ufanisi kamwe hatutauona huo ufanisi. Sababu ni moja tu, unaposubiri, mwenzako anafanya.
Tanzania tuna Potential kubwa sana ya kuwa the economic powerhouse ya sio tu Afrika Mashariki na Kati bali Afrika nzima.
Tunahitaji tu kufanya maamuzi magumu yenye akili kwa wakati. Pia tunahitaji watu wanaoweza kuwaza vizuri hayo maamuzi na kuyatekeleza.
The priority should be Congo, Burundi, Rwanda, Uganda and South Sudan. Hawa wote ni potential customers!Priority ni wapi Congo, Burundi, au Uganda?
Kenya SGR imeanza lini na ujenzi wa kuexpand umeanza lini?
Sijui kama umesikia gharama za SGR mtakamuliwa hadi jasho kulipa hii ya sasa tu let alone hizpo mpya. Just breaking even itachukua years.
You make a good point ku expand huduma za SGR ila not so fast, mate.
The priority should be Congo, Burundi, Rwanda, Uganda and South Sudan. Hawa wote ni potential customers!
You are very right. Gharama ni kubwa sana na itatuchukua muda mrefu kuzilipa. Ila tukitaka kupata full potential ni lazima tufike kote huko
Haya ndo matokeo ya free speech.Wakati wewe unasema TZ iongeze wigo wa SGR wabongo wengine wanasema hata hii ya sasa itakufa tu within 5yrs sijui gov imsikilize nani. Kuongoza hii nchi kazi sana, tuwaombee viongozi
Kwa mtazamo wangu naona Treni ya SGR haitachukua miaka 6 itakufa
Niwapongeze watanzania (hususani watanganyika) kipekee zaidi watumishi wa umma kwa kufanikisha nchi yetu kuwa na moja ya miundombinu na usafiri wa kisasa nchini hakika pongezi ziende kwenu na naamini mtamsamehe magufuli kwa kutiwapandisha madaraja ili tunufaike tunu njema kama hii. Lakini siku...www.jamiiforums.com
Reli inaweza kufanya kazi vizuri na malori yakafanya kazi vizuri.Hii TU ya kufika Moro hadi mwanza iki survive for ten years bila shida utakuwa muujiza
Wamiliki wa malori na mabasi ni kikwazo mno kwenye sector ya usafiri na ndio wamejaa bungeni
Hii TU ya kufika Moro hadi mwanza iki survive for ten years bila shida utakuwa muujiza
Wamiliki wa malori na mabasi ni kikwazo mno kwenye sector ya usafiri na ndio wamejaa bungeni
Kweli kabisa.Kudhani SGR itaua road transportation ni ufinyu wa mawazo. Nchi gani reli imeua malori?
Natamani niwe nimekosea kuwaza na siku nitakapozeeka nione sgr ikiwa imegota Kigoma ,mwanza,Arusha n.kKudhani SGR itaua road transportation ni ufinyu wa mawazo. Nchi gani reli imeua malori?
Natamani kuona ukiwa uko sahihi nami niwe nimekosea na baada ya miaka kadhaa sgr iwe ndio tegemeo la usafiri tanzaniaReli inaweza kufanya kazi vizuri na malori yakafanya kazi vizuri.
Tunahitaji watu sahihi kwenye kuamua, kupanga na kutekeleza. Hata barabara zetu zikiboreshwa kuanzia mipakani hadi kwenye bandari zetu, sekta ya usafirishaji wa malori ita thrive sana