Lord Denning
JF-Expert Member
- Jun 3, 2015
- 23,491
- 57,973
Kwa Wanasheria na Mawakili, Moja ya kosa kubwa kabisa linaloweza kukufanya uzuiwe kuendelea kufanya kazi za Uwakili ni pale unapothibitika kufanya kosa la kitaaluma yaaani professional misconduct.
Katika sekta ya Sheria Proffesional Misconduct ya juu kabisa ni kudharau Mahakama. Ikiwemo kudharau Maamuzi rasmi ya Mahakama juu ya jambo fulani. Hili pia linaweza kuchukuliwa kama kosa la Kitaaluma hasa unapopotosha Umma kwa misingi ya Kitaaluma kama alivyofanya Tulia leo wakati anazungumzia Maamuzi ya Mahakama yaliyotoka juzi kusema Marekebisho ya Sheria ya Mwaka 2020 yalikuwa kinyume na Katiba.
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye Ibara ya 107A imesema wazi kuwa Mamlaka ya mwisho katika Masuala ya Utoaji Haki nchini Tanzania ni Mahakama. Hivyo lolote linaloamliwa na Mahakama katika muktadha wa Utoaji Haki hilo ndo linabaki kuwa Msimamo wa mwisho ndani ya Taifa la Tanzania.
Mahakama katika utekelezaji wake wa jukumu lake la msingi la kikatiba la Utoaji Haki inapoamuru Sheria fulani kuwa batili kwa mujibu wa Katiba na ikatoa muda wa Bunge kurekebisha Sheria husika, muda huo unapopita, Sheria husika haitatambulika rasmi kuwa Sheria na haitatekelezwa na Mamlaka za Serikali na Mahakama kama Sheria.
Mfano kwenye suala la umri wa kuoa/kuolewa. Kwa kuwa Mahakama ilitoa muda wa mwaka kwa Serikali kubadili kifungu cha umri wa ndoa kuwa miaka 18 na Serikali haikufanya kwa kupeleka Mabadililo ya kifungu kile Bungeni, Kifungu kile kilikoma kuwa Sheria baada ya muda uliowekwa na Mahakama kupita. Hivyo kwa sasa Mamlaka ya Usajili wa Ndoa ( RITA) Haiwezi kusajili ndoa ya Binti wa chini ya Miaka 18 kwa sababu tayari kifungu hicho kimekoma kuwa Sheria haijalishi Serikali walipeleka au Hawakupeleka mapendekezo ya kubadili Sheria hiyo Bungeni.HAPA NDIPO ULIPO MSINGI WA UKUU WA KATIBA ( CONSTITUTIONAL SUPREMACY) hasa ilipotamka kuwa Mamlaka ya mwisho katika Utoaji haki nchini ni Mahakama.
Hata kwenye Suala la Maamuzi ya Mahakama kuhusu marekebisho ya Sheria ya mwaka 2020. Endapo Serikali haitapeleka mapendekezo ya marekebisho ya Sheria kufuta vile vifungu, vile vifungu vitakoma kutumika baada ya kupita muda uliowekwa na Mahakama. Hivyo muda huo ukipita, Shauri litakalofunguliwa Mahakamani na raia yeyote dhidi ya Serikali au Spika au Jaji Mkuu litapokelewa na kusajiliwa Mahakamani kama shauri halali pia Wananchi watafungua mashauri bila kiapo cha kuonesha walivyosthiriwa na Mashauri hayo yatasikilizwa na Mahakama kama mashauri halali. HAPA NDIPO ULIPO MSINGI WA UKUU WA KATIBA ( CONSTITUTIONAL SUPREMACY)
Kwa upotoshaji anaoufanya Tulia Akcson Mwansasu tena kwa makusudi, tungekuwa na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam makini hakika hasa kadada kangeny'ang'anywa ile degree ya Sheria.
Soma pia Spika Dkt. Tulia ashangazwa na wanaosherehekea uamuzi wa Mahakama viongozi kushtakiwa