Tungekuwa tunategemea mashamba ya Serikali, wengi tungekufa njaa

Tungekuwa tunategemea mashamba ya Serikali, wengi tungekufa njaa

Keynez

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2007
Posts
2,428
Reaction score
3,937
Ndugu zangu,

Kila leo najaribu kutafakari mustakabali wa taifa hili na mienendo ya taasisi mbalimbali za Serikali na utendaji wake. Ni jambo la kusikitisha, kutisha na kustaajabisha na ukosefu wa ubunifu, na utendaji duni wa taasisi nyingi.

Umeme ni kitendawili, hili najua wengi mmeliongelea. TANESCO wanacheza draft na umeme, unakaa hapa unakata, unasema embu ngoja nitoke, unaenda pale unakata pia! Mgao hauna mpangilio maalumu ukiachilia mbali uhalali wa kuwepo mgao wenyewe.

Juzi juzi nimepanda mwendokasi pale Morocco, nikawa napanda daraja lile nikajiuliza, hili lilikuwa wazo la nani kujenga daraja hili kama suluhisho la kutoka upande mmoja hadi mwingine? Je waliwaza watumiaji wake? Hii mwendokasi tumeambiwa ipo huko miji mingine mikubwa, wana madaraja ya namna hii?

Imefikia wakati nawaza hivi nchi hii mashamba yote yangekuwa yanaendeshwa na Serikali hali ya chakula nchi hii ingekuwaje?
 
Back
Top Bottom