Tungekuwa wapi leo bila Rais Samia?

Tungekuwa wapi leo bila Rais Samia?

Mwananchi Huru

JF-Expert Member
Joined
Nov 20, 2021
Posts
2,128
Reaction score
1,896
Toka ndani ya mioyo yetu tutafakari haya kwa pamoja huku tukimshirikisha Mungu wetu:

1. Kama sio Rais Samia Suluhu Hassan kupewa kibali na Mungu,Je watu wasiojulikana wangekuwa wamepoteza wenzetu wengine wangapi mpaka leo, Wewe unayempinga Rais Samia leo Je umewahi kujiuliza kama ungekuwa hai mpaka leo kama sio huyu Rais Samia unayempinga na kumbeza kila leo?

2. Kama sio Rais Samia Suluhu Hassan kupewa kibali na Mungu tungefanyaje kumaliza upungufu wa madarasa wa miaka mingi yanayofikia elfu 15 sawa na wastani wa madarasa matatu katika kila Shule ya Sekondari ya Serikali nchi nzima na mengine zaidi ya elfu 3 kwa shule za msingi Shikizi najua mnajua kabla tulisema Tanzania hatuna maambukizi ya Covid 19 hivyo tusingeweza kupata mkopo ule usio na riba,

3. Kama sio Rais Samia Suluhu Hassan kupewa kibali na Mungu nilini tungekusanya kodi inayofikia Shilingi trilioni 2.51 kwa mwezi mmoja tena bila kunyanyasa wala kukimbiza walipakodi wetu,Kwani simnakumbuka Mzee Jakaya yeye alikusanya wastani wa trilioni 10 kwa mwaka mzima pesa tunayoweza kuikusanya kwa miezi minne tu sasa!!

4. Kama sio Rais Samia Suluhu Hassan kupewa kibali na Mungu nani angeweza kuongeza mzunguko wa fedha kwenye nchi ( M3 ) kwa mara mbili zaidi kutoka asilimia 6.5 hadi asilimia 12.7 tena kwa miezi tisa tu,

5. Kama sio Rais Samia Suluhu Hassan kupewa kibali na Mungu nani angeufikisha Uchumi wetu kwenye ukuaji wa Pato la Taifa wa asilimia 5.4 kutoka mdororo wa asilimia 2.1 wakati wa mtangulizi wake,

6. Kama sio Rais Samia Suluhu Hassan kupewa kibali na Mungu ni lini tungeifikia sera yetu ya 50/50 kwenye nyadhifa mbalimbali za Kivyama, kiserikali na taasisi nyingine mbalimbali kwani kupitia yeye Tanzania na dunia vimejifunza kuwa ni kweli kuwa " A Woman Can Lead anywhere at any Post "

7. Kama sio Rais Samia Suluhu Hassan kupewa kibali na Mungu nani angeinusuru miradi hii mikubwa ya kimkakati ya SGR na SG iliyokuwa ikijengwa kwa mikopo ya masharti ya kibiashara,Je umewahi kuwaza nini ingekuwa hatma ya Tanzania na Watoto wa Watanzani kwa madeni haya hatari ya kibiashara?

8. Kama sio Rais Samia Suluhu Hassan kupewa kibali na Mungu nani angewaachilia huru Mashekhe wetu wa uamsho waliosota gerezani kwa miaka zaidi ya 10 bila kosa au Nani angewaachia Wana-CHADEMA waliokuwa wametapakaa karibu kila gereza hapa Tanzania?

9. Kama sio Rais Samia Suluhu Hassan kupewa kibali na Mungu nani angeifungua Tanzania kimataifa baada ya kuchafuliwa vibaya na kwa muda mrefu na akina Tundu Lissu na wenzake kiasi cha kunyimwa misaada na mikopo ya masharti|riba nafuu kulikotulazimu kama Taifa kuanza kuiingiza nchi yetu kwenye mikopo ya kibiashara wakati nchi haifanyi biashara ila inatoa huduma tu hili lilikuwa ni bomu kwa nchi,

10. Kama sio Rais Samia Suluhu Hassan kupewa kibali na Mungu nani angewaongezea mishahara na madaraja makubwa makubwa watumishi wetu wa Serikali waliosota miaka mitano mfululizo bila kuona senti ya Serikali?

11. Kama sio Rais Samia Suluhu Hassan kupewa kibali na Mungu nani angewaondolea Wasomi wetu VRF ya asilimia 6 toka makato ya asilimia 15 toka HESLB kwani leo wanakatwa asilimia 9 tu tena mpaka upate kazi ndio uanze kukatwa,

12. Kama sio Rais Samia Suluhu Hassan kupewa kibali na Mungu nani angekivusha Chama Changu cha Mapinduzi Salama mwaka wa Uchaguzi 2024|25 ikiwa ni baada ya Rais Samia kurudisha Ushawishi wa Chama kwa jamii|Umma kutokana na matendo mema na mazuri ya Chama Chake na Serikali yake,

#Kama Sio katazo la Katiba kwa kudra za mwenyezi Mungu huyu Mama alitakiwa apewe miaka 20 ila katiba iheshimiwe twende na Mama mpaka 2030 itatufaa sana,Wewe unasemaje?

photo_2022-01-10_12-09-25.jpg
 
Samia ndo rais mwenye machawa wengi sana. Yani mtu akitaka teuzi anasifia sifia hata kama ujinga ili aonekane.

Ila ukweli huyu mama nchi imenshinda mfumuko wa bei za bidhaa kila kona, maisha yamekua magumu sana. Mfuko wa cement juu, bati juu, nondo usisemeee aisee mama anaupiga mwingi.
 
Samia ndo rais mwenye machawa wengi sana. Yani mtu akitaka teuzi anasifia sifia hata kama ujinga ili aonekane.

Ila ukweli huyu mama nchi imenshinda mfumuko wa bei za bidhaa kila kona, maisha yamekua magumu sana. Mfuko wa cement juu, bati juu, nondo usisemeee aisee mama anaupiga mwingi.
Kwani hii mada inajambo gani baya mkuu au wewe unachuki tu Rais Samia Suluhu Hassan,

mfumuko wa bei mbona ni dunia nzima?
 
Hebu toka ndani ya mioyo yetu tutafakari haya kwa pamoja huku tukimshirikisha Mungu wetu:

1. Kama sio Rais Samia Suluhu Hassan kupewa kibali na Mungu mpaka leo watu wasiojulikana wangekuwa wamepoteza wenzetu wengine wangapi,Je umewahi kujiuliza wewe unayempinga Rais Samia leo kama ungekuwa hai mpaka leo kama sio Rais Samia kuwako leo unayempinga leo?
Kwakweli bila Rais Samia sijui ata tungekuwa wapi maana duuuh,
 
Petrol juu,nondo juu,cement juu,mafuta ya kula juu,sukari juu....
Kwa Hali hiyo hata figure za mapato ya serikali lazima ziwe juu!
Na mapato ya namna hii hudumu Kwa muda mfupi,subiri kama watakutangazia mapato ya January!
Vitu vikapanda bei watu hawanunui kama hawanunui kodi ingetoka wapi?
 
Mbona Mzee Kikwete hashambuliwi?
Unaishi Dunia ipi?JPM alipoingia madarakani,Kikwete alishambuliwa sana!Mpaka watu wakasema utafikiri nchi haikuwa na Rais!
JPM hata yeye mwenyewe amemshambulia mtangukizi wake mara nyingi tu!
JPM ametokea,na yeye anashambuliwa japo ni marehemu,je angekuwa hai?
Nakuhakikishia,Samia akiondoka na yeye atageukwa na Hawa Hawa wanaomfagilia kwa Sasa!
 
Nampongeza raisi Samia kwa kutufikisha hapa tulipo leo, kwa muda mfupi aliokaa madarakani ameshafanya mengi mazuri na yenye manufaa kwa nchi hii. Ila pia siwezi kuwabeza maraisi waliopita maana na wao walifanya mazuri kwa taifa letu. Tunambiwa hakuna binadam aliekamilika, ikiwa na maana kila raisi alifanya mazuri yaliowapendeza watu, na mabaya yaliowachukiza watu (hata kwa bahati mbaya) Mzee Mwinyi aliwahi kusema kila nabii na kitabu chake, sasa tumuache raisi wetu aliepo sasa amalizie kuchapa upande wa kitabu chake uliobaki.
 
Ningekua hapahapa Tanzania nilipo sasa hivi ila haya yafuatayo yasingekuwepo.

Tusingekua tunatoa tozo.

Wanaomiliki nyumba wangeendelea kulipia kodi za majengo bila kuathiri bei ya umeme.

Tusingeona jinsi mhimili mmoja ulivyo dhaifu na wanaoutengeneza huo muhimili kuwa wanafiki na wanaojali matumbo yao zaidi kuliko kazi ya kuwakilisha wananchi.

Bei za vitu zisingeruka namna hii kama hali ilivyo sasa.
 
Unaishi Dunia ipi?JPM alipoingia madarakani,Kikwete alishambuliwa sana!Mpaka watu wakasema utafikiri nchi haikuwa na Rais!
JPM hata yeye mwenyewe amemshambulia mtangukizi wake mara nyingi tu!
JPM ametokea,na yeye anashambuliwa japo ni marehemu,je angekuwa hai?
Nakuhakikishia,Samia akiondoka na yeye atageukwa na Hawa Hawa wanaomfagilia kwa Sasa!

Never relax around blacks, atafanya kila kitu na kuimba mapambio yote ilimradi tu awe anahitaji kitu kwako.
 
... kwani wasiojulikana wamewahi ku-exist? Kama jibu ni ndio, awachukulie hatua na haki ionekane inatendeka ili tumshukuru badala ya kumpaka mafuta kwa mgongo wa chupa kama unavyojaribu kufanya ewe mnafiki!
 
Back
Top Bottom