Tuombeane Watanzania, sababu tuna hali ngumu sana ambayo hatukuizoea

Tuombeane Watanzania, sababu tuna hali ngumu sana ambayo hatukuizoea

2019

JF-Expert Member
Joined
Dec 31, 2018
Posts
3,130
Reaction score
4,735
Unafiki soo mzuri mimi nimeshaanza kumkumbuka Magufuli. Yule mzee pesa za miradi mikubwa alikuwa anapata wapi? Hakukamua wananchi wa kawaida lakini ameacha alama kabisa. Sikumpenda lakini namkumbuka sana.

Nimenunua umeme wa 2500 nimepewa wa 500.Nyu mba sio yangu na mwenye nyumba hakai hapo.

Nimemwambia Mwenye nyumba aende TRA kutoa mita yetu akasema kama nimeichoka nyumba yake nihame au anipandishie kodi. Nimebaki njia panda. Japo tunajenga nchi yetu lakini makato yamezidi.

Screenshot_20210822_114132.jpg
 
Kwa maumivu haya,Nina wasi wasi Kuna siku nitakua gaidi,nianze kuvizia haya majitu yanayoleta maumivu nayachapa risasi
Wanajeshi wa Afghanistan sio wajinga wala sio kama hawakuwa na vifaa vya kupigana. Ila rushwa na ufisadi vilizidi ndio mana wakona bora wakose wote kuliko kuwe na unyonyaji wa wachache
 
Unafiki soo mzuri mimi nimeshaanza kumkumbuka Magufuli. Yule mzee pesa za miradi mikubwa alikuwa anapata wapi? Hakukamua wananchi wa kawaida lakini ameacha alama kabisa. Sikumpenda lakini namkumbuka sana.
Nimenunua umeme wa 2500 nimepewa wa 500.
Nyumba sio yangu na mwenye nyumba hakai hapo.
Nimemwambia Mwenye nyumba aende TRA kutoa mita yetu akasema kama nimeichoka nyumba yake nihame au anipandishie kodi. Nimebak njia panda. Japo tunajenga nchi yetu lakini makato yamezidi

View attachment 1903075

Lipeni kodi, nchi inahitaji maendeleo! Kikubwa pesa ifanye kazi tuliyoahidiwa!

Halafu unanunuaje umeme wa buku mbili aiseeee!! Ukinyoosha nguo moja si ushaisha??
 
Unafiki soo mzuri mimi nimeshaanza kumkumbuka Magufuli. Yule mzee pesa za miradi mikubwa alikuwa anapata wapi? Hakukamua wananchi wa kawaida lakini ameacha alama kabisa. Sikumpenda lakini namkumbuka sana.
Nimenunua umeme wa 2500 nimepewa wa 500.
Nyumba sio yangu na mwenye nyumba hakai hapo.
Nimemwambia Mwenye nyumba aende TRA kutoa mita yetu akasema kama nimeichoka nyumba yake nihame au anipandishie kodi. Nimebak njia panda. Japo tunajenga nchi yetu lakini makato yamezidi

View attachment 1903075
Hahaha..
Mi-5 tena!
 
Usidharau 2500 kwa sababu unayo omba sana Mungu usipite kwenye hali hiyo

Nilijua inaweza kuleta mtizamo hasi kwa baadhi ya memba na sikutaka kuandika sana!!

Refer tangazo la Tanesco la kuanza kwa makato na ndiyo utaelewa nilichomaanisha si dharau ila ushauri!! Wamesema usinunue umeme wa 2,000 hivi unategemea nini ukinunua wa 2,500!?

Check mwingine huyu 😂😂😂 Tate Mkuu
 
Sina ubaya na hiyo tozo lakini lazima utambue kuna watu wengi hiyo ni gharama kubwa sana.
Tanzania Lina idadi ndogo sana ya watu wenye kujimudu kiuchumi ndio maana hata makusanyo ya Kodi ni tatizo muhimu ni kulifungua hili kundi kubwa kwa elimu ya biashara na kuwahatamia wawe na vipato, nadhani itasaidia kuongeza wigo wa Kodi na kupunguza hizi tozo zinazoibuka ghafla
 
Akili yako siyo nzuri. Siyo wote ni matajiri kama wewe. Watanzania tulio wengi tunaangukia kundi la huyu muungwana. Tunanunua umeme wa sh 3,000/= kwa mwezi kwa ajili ya mwanga tu wakati wa usiku. Mshukuru Mungu kwa ulicho nacho. Usimcheke ambaye hana.
Yani maisha yamekuwa magumu Kwa kukatwa 2000 kwa miezi miwili?
Kunywa sumu ufe, hii nchi ili isonge mbele haihitaji Watu aina yako
 
Nilijua inaweza kuleta mtizamo hasi kwa baadhi ya memba na sikutaka kuandika sana!!

Refer tangazo la Tanesco la kuanza kwa makato na ndiyo utaelewa nilichomaanisha si dharau ila ushauri!! Wamesema usinunue umeme wa 2,000 hivi unategemea nini ukinunua wa 2,500!?

Check mwingine huyu 😂😂😂 Tate Mkuu
Ukinunua wa 2500 unapewa unit moja
 
Nami nasema unafiki sio mzuri. HAITAKUJA KUTOKEA NIMKUMBUKE MAGUFURI.

Rais genius alikuwa kikwete.
Wee Imagine:
MAFISADI YALIKUWA YANACHOTA MABILIONI, lakini:
* Alikuwa anajenga lami kuunganisha mikoa yote
*Alikuwa anapandisha madaraja na mishahara
*Jkt kuruta wanakula 50k kila kichwa
*Watumishi wakienda kwenge kaseminar kidogo..wanalamba posho
*Mtaani hela ilikuwepo, ukifungua kajibiashara unauza.

KIKWETE ALIKUWA GENIUS AISEE😀😀
 
Back
Top Bottom