Tuondokane na kununua Matrekta used kwa bei kubwa yanayokaribiana na bei ya trekta jipya

Tuondokane na kununua Matrekta used kwa bei kubwa yanayokaribiana na bei ya trekta jipya

mkulima2010

Member
Joined
Jul 8, 2015
Posts
39
Reaction score
40
Ndugu wakulima wenzangu tuondokane na kununua Matrekta used kwa bei kubwa.

Tuondokane na kununua Matrekta used kwa bei kubwa, utumiaji wa mafuta, gharama za spea, Pia hayo matrekta used bei zake zinakaribiana na bei ya trekta jipya.
 
Mkuu Mkulima2010 km hujui vitu kaa kimya au uliza mimi JF imenisaidia sana maisha yangu hasa jukwaa hili nimejiajiri kutokana na ushauri nilioupata kutokana na mawazo ya watu sijawahi kukurupuka kuanzisha uzi.

Usipotoshe watu mkuu mimi ninayo matractor mapya na used kwa ufupi tu massey 385 mpya (hizi zilishachakachuliwa zinatoka Pakistan) haiwezi kumaliza masaa 24 ikikaribia kufikisha masaa 20 inabadili mlio na ingine inapoteza nguvu inabidi uipumzishe wkt massey 290 used inamaliza masaa 24 bila tatizo.

Wahindi wapakistan na wachina wameleta matractor mabovu sana kuweni makini ktk kuchagua hayo matractor mapya, mimi nilipewa somo zuri na jamaa zangu wauzaji maana nina marafiki wanauza matractor mapya na used, used ukichagua vizuri ni bora zaidi mara mia kuliko hizi mpya zao feki.
 
Mimi nilikuwa natumia ford 6600 na massey 160 ambazo nilinunua used kutoka Europe, nilipata ushauri nikayauza nimenunua trekta mbili mpya, moja ni swalaji new model ford new holland hizo ni kiwembe balaa speed shambani nguvu na utumiaji wa mafuta ni mzuri, tatizo lenu humu jf ni kwamba mnajifanya mnajuwa kila kitu, mimi ninalima mashamba makubwa ninayajuwa haya matrekta vizuri kifupi nenda kibaigwa uliza pale sokoni or angalia trekta zinazoingia pale ni mpya nyingi. Uliza wakulima wakubwa wa mahindi kibaigwa watakuambia kwanini wananunuwa matrekta mapya.
 
Mkuu Kiogwe mimi sio dalali ni mkulima hivi kweli mtu mzima na akili zake auziwe trekta useed milioni 20, wakati anaweza pata trekta mpya kwa bei hiyo hiyo tena akakopeshwa na kulipa kwa miaka mitatu hizo massey fergusion zina matatizo ya hydraulic repair kit, hydraulic pump, angalia kitu cha SWARAJI NI WASTANI WA EKARI 30 KWA MASAA KUMI NA MBILI TU, NEW HOLLAND NI EKARI 35 KWA MASAA KUMI NA MBILI, FARM TRAC NI EKARI 25 KWA MASAA KUMI NA MBILI, KUBOTA NI EKARI 30 KWA MASAA KUMI NA MBILI, TAFFE NI EKARI 26 KWA MASAA KUMI NA MBILI, CASE NI EKARI 30 KWA MASAA KUMI NA MBILI UWEZO WA KULIMA KWA TREKTA
 
Nimekuja kasi kuangalia hii post inayosema trakta mpya kwa bei nafuu naishia kuona viluwiluwi tu. Hapa kama huyu ni marketing officer basi ameajiriwa kwa bahati mbaya.
Ni ajira ya baba mkwe
 
Mimi nilikuwa natumia ford 6600 na massey 160 ambazo nilinunuwa used kutoka europe, nilipata ushauri nikayauza nimenunuwa trekta mbili mpya moja ni swalaji new model ford new holland hizo ni kiwembe balaa speed shambani nguvu na utumiaji wa mafuta ni mzuri, tatizo lenu humu jf ni kwamba mnajifanya mnajuwa kila kitu, mimi ninalima mashamba makubwa ninayajuwa haya matrekta vizuri kifupi nenda kibaigwa uliza pale sokoni or angalia trekta zinazoingia pale ni mpya nyingi. Uliza wakulima wakubwa wa mahindi kibaigwa watakuambia kwanini wananunuwa matrekta mapya

Mkuu kweli wewe ni mkulima. Naomba kujua wapi na utaratibu wa kukopa hizo tractor mpya
 
Mkuu Kiogwe mimi sio dalali ni mkulima hivi kweli mtu mzima na akili zake auziwe trekta useed milioni 20, wakati anaweza pata trekta mpya kwa bei hiyo hiyo tena akakopeshwa na kulipa kwa miaka mitatu hizo massey fergusion zina matatizo ya hydraulic repair kit, hydraulic pump, angalia kitu cha SWARAJI NI WASTANIWA EKARI 30 KWA MASAA KUMI NA MBILI TU, NEW HOLLAND NI EKARI 35 KWA MASAA KUMI NA MBILI, FARM TRAC NI EKARI 25 KWA MASAA KUMI NA MBILI, KUBOTA NI EKARI 30 KWA MASAA KUMI NA MBILI, TAFFE NI EKARI 26 KWA MASAA KUMI NA MBILI, CASE NI EKARI 30 KWA MASAA KUMI NA MBILI UWEZO WA KULIMA KWA TREKTA

Data nzuri nitazifuatilia lakini mimi nilitaka ninunue John Deer nazo vipi uwezo wake zikilinganishwa na hizi ulizotaja?
 
Mimi nadhani ktk marketing eleza chako kilivyo kizuri sio kuponda vingine utaharibu kila kitu wewe.
 
mkuu kweli wewe ni mkulima. Naomba kujua wapi na utaratibu wa kukopa hizo tractor mpya
Makampuni yanayokopesha ni mengi unaweza kwenda direct or ukapitia mfuko wa pembejeo wakakuzamini, or ukaenda direct pale suma JKT wana ukakopeshwa kupitia hti ya kimila ya halimashauri suma jkt wao wa aina mbili za matrekta farm trak na new holland, piya ukienda toyota pugu road nao wanakopesha matrecta aina ya case kupitia benki zao wao, piya kuna wengine wapo it quality plaza wao wanakopesha aina ya kubota kupitia link zao za benki na mfuko wa pembejeo, wengine ni taffe hawa wapo kariakoo mtaa wa lugoda na wanatoa mkopo wa matrekta
 
data nzuri nitazifuatilia lakini mimi nilitaka ninunue john deer nazo vipi uwezo wake zikilinganishwa na hizi ulizotaja?
Mkuu kwa kazi za kilimo usinunue trekta kwa pesa cash, hizo pesa zako weka akiba tafuta trekta nzuri jipya ununuwe kwa kulipa asilimia 30 ya bei. Kwani kilimo kina changamoto nyingi sana unapo anza inabidi uwe na akiba ya pesa piya ni vizuri tukatumia fursa za mfuko wa pembejeo nakushauri fanya tafiti kwanza kabla ya kuamua unakwenda lima wapi, aina ya mazao, masoko na changamoto mbalimbali zilizopo.
 
mi nathani ktk marketing eleza chako kilivyo kizuri sio kuponda vingine utaharibu kilakitu wewe
Asante ila mimi sifanyi marketing nilikuwa natoa ushauri tu nikaanza pigwa mawe na wauza chuma chakavu (used) kazi yangu ni mkulima.
 
Ndugu wakulima wenzangu tuondokane na kununua Matrekta used kwa bei kubwa.

Tununue matrekta mapya, ambayo gharama zake za uendeshaji zipo chini sana , utumiaji wa mafuta, gharama za spea, Piya hayo matrecta used bei zake zinakaribiana na bei ya trekta jipya.

Tuyapate wapi mkuu, yako wapi na bei gani?

Vv
 
Ndugu wakulima wenzangu tuondokane na kununua Matrekta used kwa bei kubwa.

Tununue matrekta mapya, ambayo gharama zake za uendeshaji zipo chini sana , utumiaji wa mafuta, gharama za spea, Piya hayo matrecta used bei zake zinakaribiana na bei ya trekta jipya.

Check hili bazaz nalo!!
 
Mkuu Kiogwe mimi sio dalali ni mkulima hivi kweli mtu mzima na akili zake auziwe trekta useed milioni 20, wakati anaweza pata trekta mpya kwa bei hiyo hiyo tena akakopeshwa na kulipa kwa miaka mitatu hizo massey fergusion zina matatizo ya hydraulic repair kit, hydraulic pump, angalia kitu cha SWARAJI NI WASTANIWA EKARI 30 KWA MASAA KUMI NA MBILI TU, NEW HOLLAND NI EKARI 35 KWA MASAA KUMI NA MBILI, FARM TRAC NI EKARI 25 KWA MASAA KUMI NA MBILI, KUBOTA NI EKARI 30 KWA MASAA KUMI NA MBILI, TAFFE NI EKARI 26 KWA MASAA KUMI NA MBILI, CASE NI EKARI 30 KWA MASAA KUMI NA MBILI UWEZO WA KULIMA KWA TREKTA
Mkuu mimi nazani kuna kitu unatuficha wewe ni dalari wa matractor hayo unayoita mapya japo yote ni fake yani kulinganisha tractor used na Tafe kubota au Case kiutendaji kimatumizi hata kimaslahi kwa mkulima ni sawa na kulinganisha kifo na usingizi faida ya hayo matractor mapya ni kuwa unakopeshwa japo kulipa nayo ni tabu kiukweli haziwezi kazi sana mimi huu msimu wa ufuta nimepeleka moja tu 290 used inapakia ufuta viroba 120 au 80 za mahindi au mbao za 2 by 10 futi 10 napakia 150 bila shida huo mzigo hakuna new Holland inayonyanyuka nao ninazo huko polini haziwezi.subiri kuna order ya ekari elfu 2 naivizia nikiipata ntakwambia uje uone vyuma used zinapigaga ekari 120 ndani ya masaa 24 kila tractor nimeajiri ma operator 2
 
Nimekuja kasi kuangalia hii post inayosema trakta mpya kwa bei nafuu naishia kuona viluwiluwi tu. Hapa kama huyu ni marketing officer basi ameajiriwa kwa bahati mbaya.
Same to me, maana nilipita maonesho ya 7/7 bado trekta si la mkulima bei juu sana
 
Back
Top Bottom