Kuna siku nipo semina pale Dom ukumbini Wizara ya Fedha.
Kama kawaida Wizara ya Fedha ikaalika taasisi kadhaa Kuja kuongea na watumishi.
Akaanza UTT, mzee mmoja hivi amevaa suti nyeusi safi, aka project mada yake pale kwenye screen.
Kwa dakika 40 alizoongea hakutoa mfano hata wa mwalimu wa TGTS C ndio awe base yetu.
Nilitaka kunyoosha mkono nimwambie aache kutoa Mifano ya wapata mil 50 na 100 aje kwa majority ya watz wa kipato cha kawaida.
Ila nikaona na yeye yupo tu kazini, hivyo nichune amalize kipindi chake akasaini dole gumba mwisho wa mwezi aingize chake.
Chance ndoto
#YNWA