Tuongeeni tu ukweli, foleni za Dar kwa sasa zinatisha!

FRANCIS DA DON

JF-Expert Member
Joined
Sep 4, 2013
Posts
38,920
Reaction score
44,970
Sijui tunaelekea wapi kwa foleni kali namna hii, hivi kweli unakaa foleni lisaa lizima bila kusogea hata hatua moja?! Kwanini serikali haijatangaza state of emergency mpaka dakika hii?!! Hii ni hatari, ni janga; KWA HILI NAPIGA KURA YA KUTOKUWA NA IMANI NA MAMLAKA HUSIKA, something has to be done immediately!

=====================================

 
Mbona Hakuna foleni Sasa kwani shule nyingi zimeanza kufungua.Kuwa specific na sio ki generalize .Traffic wanajifanya sana
 
Foleni ya Dar ni jambo la kujitakia. Nasema hivyo kwa sababu Dar haina magari mengi kama watu wanavyodhani. Watu walikuwa wame-relax bila kufikiria kesho na keshokutwa ni nini kitatokea. Hili tatizo ni kama tatizo la mafuriko. Huko nako watu walikuwa wamelala utafikiri miji inayojenga mitaro ni wajinga. Mji wowote bila mipangilio endelevu inakuwa na matokeo mabaya ambayo kuyarekebisha ni vigumu sana.
 
Yaani sababu ya foleni ya dar unataka nchi i declare state of emergency? Seriously?

America na ukubwa wote ule hawajahi ku declare state of emergency kisa jam ya magari. Hili nisuala lakushughulikiwa na uongozi wa mkoa.

Alaf state of emergency huwa declared pale nchi inapopatwa na majanga makubwa.

Msongamano wa magari tena dar... hell no..
 
Tatizo limeongezeka sababu ya mvua barabara nyingi sana zimeharibika vby sana magari yanapita taratibu.
 
Wewe huoni kuwa hili ni janga?!
 
mkuu pole sana ,hamia mkoan ikibid
 
Mfanye kama wanavyofanya Nairobi. Magari ya binafsi hayaruhusiwi kwenda city centre isipokuwa siku za week ends tu. Siku zingine wote mpande public transport except government ministers and senior government officials kwa magari ambayo plate numbers zake zinaonyesha utambulisho huo pamoja na magari ya wagonjwa. This is the best, easiest and cheapest solution. Kwani lazima uende na gari lako kazini? Kumuonyesha nani? Hamieni mikoani kama mnataka kwenda kazini na magari yenu.
 
Issue kubwa inachangiwa n'a desk officer or Engineer wa serekali kutokuwa n'a mawazo chanya hawawezi kufikiria nje y'a box ! Mfano ni msimamizi wa mradi wa dar metropolitan kwa upande wa kinondoni ni mzigo wa nawe !
 

Public transport wenyewe mwendokasi..Ptuuu

Watu wengi wamehamasika kununua magari kwa sababu ya shida za usafiri wa umma hasa hasa mwendokasi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…