FRANCIS DA DON
JF-Expert Member
- Sep 4, 2013
- 38,920
- 44,970
Sijui tunaelekea wapi kwa foleni kali namna hii, hivi kweli unakaa foleni lisaa lizima bila kusogea hata hatua moja?! Kwanini serikali haijatangaza state of emergency mpaka dakika hii?!! Hii ni hatari, ni janga; KWA HILI NAPIGA KURA YA KUTOKUWA NA IMANI NA MAMLAKA HUSIKA, something has to be done immediately!
=====================================
=====================================
Hizo flyover na bypass hazimalizi foleni moja kwa moja. Kitakachoondoa foleni Dar ni feeder roads (barabara za michepuko). Hizi ndio zitasaidia sana kumaliza shida.
- Mtu anaetoka Mbagala kwenda Gongolamboto asilazimike kupita TAZARA, kuna njia za ndanindani kama nne hivi, Buza, Msongola, Mchicha na Mwanagati
- Anaetoka Kimara kwenda Temeke asilazimishwe kupitia Ubungo, Kuna short cut ya Bonyokwa ambayo inaungana na Nyerere road pale Majumba 6 then anaingia Jet mpaka Buza.
- Anaetoka Tegeta kwenda Kibamba ama Mbezi Luis asilazimishwe kupitia Tangibovu, anaweza kupita Wazo akatokea Goba Njia nne mpaka Mbezi Luis kisha akaenda Kibamba nk. Ni bahati mbaya sana kwamba almost ofisi nyingi zikoKariakoo n posta, lakini vinginevyo wale ambao hawana ulazima wa kufika posta na Kariakoo wangetengenezewa njia mbadala