Tuongeeni tu ukweli, foleni za Dar kwa sasa zinatisha!

Foleni ya Dar ni jambo la kujitakia. Nasema hivyo kwa sababu Dar haina magari mengi kama watu wanavyodhani. Watu walikuwa wame-relax bila kufikiria kesho na keshokutwa ni nini kitatokea. Hili tatizo ni kama tatizo la mafuriko. Huko nako watu walikuwa wamelala utafikiri miji inayojenga mitaro ni wajinga. Mji wowote bila mipangilio endelevu inakuwa na matokeo mabaya ambayo kuyarekebisha ni vigumu sana.
Njooni mbeya foleni hakuna wenye magari wote wanajulikana wakina mwakibete, mwakasungura yeye anagari tatu za kutembelea
 
Apande daladala. Atafika mjini haraka kama enzi zile tulizokuwa tunatumia dakika 3 kutoka Mlimani hadi Kariakoo kwa mabasi ya DMT. Sasa hivi ni dakika zaidi ya 120 kwa sababu ya utitiri ya magari ya binafsi.
Hizo daladala mnazoongelea ziko wapi nyie? Watu wanakaa vituoni hadi wanaugua!
 
Akilinza msukusu zinasema flyover ya tazara, ubungo ikikamilika tatizo la folen Dar litaisha kabisa
Hizo flyover na bypass hazimalizi foleni moja kwa moja. Kitakachoondoa foleni Dar ni feeder roads (barabara za michepuko). Hizi ndio zitasaidia sana kumaliza shida.
  1. Mtu anaetoka Mbagala kwenda Gongolamboto asilazimike kupita TAZARA, kuna njia za ndanindani kama nne hivi, Buza, Msongola, Mchicha na Mwanagati
  2. Anaetoka Kimara kwenda Temeke asilazimishwe kupitia Ubungo, Kuna short cut ya Bonyokwa ambayo inaungana na Nyerere road pale Majumba 6 then anaingia Jet mpaka Buza.
  3. Anaetoka Tegeta kwenda Kibamba ama Mbezi Luis asilazimishwe kupitia Tangibovu, anaweza kupita Wazo akatokea Goba Njia nne mpaka Mbezi Luis kisha akaenda Kibamba nk. Ni bahati mbaya sana kwamba almost ofisi nyingi zikoKariakoo n posta, lakini vinginevyo wale ambao hawana ulazima wa kufika posta na Kariakoo wangetengenezewa njia mbadala
 
Aisee hii ni kweli, kwanini wasiboreshe tu hizo barabara za michepuko, maana sio lazima wote tubanane TAZARA, Ubungo na Mwenge
 
Umeona eeh kiongozi, Hizo shortcut ziko nyingi sana nimetaja chache tu kama kuchokoza mada. Njia za kutoka Kinondni kwenda Sinza ziko kibao sana, ila watu tunabanana kwa Mtogole na Ali Hassan mwinyi, kwa sababu hazijatengenezwa.
 
Hizo daladala mnazoongelea ziko wapi nyie? Watu wanakaa vituoni hadi wanaugua!
Mkuu wala asikubabaishe. Siku zote watu wavivu hutafuta visingizio kuhalalisha uvivu wao. Tatizo la Dar siyo magari binafsi kuwa mengi. Kwanza Dar haina magari mengi. Tatizo liko kwenye mipango na maono ya viongozi wetu. Wamejikalia tu wanafikiri mambo huwa yanajiendea na kujipangilia yenyewe. Haya ni mabo yalitakiwa yawe yanapangwa miaka iliyopita. Sasa hivi tunachoona ni matokeo ya uzembe wa siku za nyuma. Na bado sioni matatizo yakiisha siku za karibuni kwani inaonekana kama hatujui tufanye nini hasa. Watu wanafanya majaribio ya kupapasa hapa na pale. Kila mtu ana solution yake mfukoni nayoona inafaa kwa sababu itampa ulaji.
 
Hizo flyover na bypass hazimalizi foleni moja kwa moja. Kitakachoondoa foleni Dar ni feeder roads (barabara za michepuko). Hizi ndio zitasaidia sana kumaliza shida.
  1. Mtu anaetoka Mbagala kwenda Gongolamboto asilazimike kupita TAZARA, kuna njia za ndanindani kama nne hivi, Buza, Msongola, Mchicha na Mwanagati
  2. Anaetoka Kimara kwenda Temeke asilazimishwe kupitia Ubungo, Kuna short cut ya Bonyokwa ambayo inaungana na Nyerere road pale Majumba 6 then anaingia Jet mpaka Buza.
  3. Anaetoka Tegeta kwenda Kibamba ama Mbezi Luis asilazimishwe kupitia Tangibovu, anaweza kupita Wazo akatokea Goba Njia nne mpaka Mbezi Luis kisha akaenda Kibamba nk. Ni bahati mbaya sana kwamba almost ofisi nyingi zikoKariakoo n posta, lakini vinginevyo wale ambao hawana ulazima wa kufika posta na Kariakoo wangetengenezewa njia mbadala
Ni kweli. Ila ni vizuri kusisitiza kuwa tatizo litatatuliwa kwa kutumia multiple solutions.
1. Ring roads (ambazo najua tuna uwezo wa kuzijenga ila dhamira hakuna)
2. Magari ya dala dala yawe mabasi makubwa na magari madogo yaondolewa
3. Kujenga vituo vya daladala kila sehemu na kuhakikisha madereva wanavitumia.
4. Kuhakikisha sheria za barabarani zinafuatwa (hili nalo linachangia sana foleni)
5. Kuwa na trains na trams
6. Flyovers
 
Naunga mkono hoja yako [emoji106] [emoji106] [emoji106]
 
Hizo daladala mnazoongelea ziko wapi nyie? Watu wanakaa vituoni hadi wanaugua!
Zitapatikana za kutosha na bora baada ya magari binafsi kuzuiwa kuingia mjini au yatakapoanza kutozwa ushuru mkubwa, kama shs 50,000 kwa siku kwa kuingiza gari binafsi mjini siku za kazi!!
 
Kwanini wasiboreshe sasa ili mtu asione umuhimu wa kwenda na Gari lake. Eti wataboresha baada ya kupiga ban, mwajiri/mteja anakuvumilia tu!
Huwezi kuboresha wakati magari yamejazana barabarani. Yanaondolewa kwanza na ndani ya muda mfupi mabasi mazuri yanaingia barabarani.
 
Mamlaka zikawasiliane na mzee lowassa, alituambia ana mbinu za kumaliza kabisa foleni za dar ndani ya mwezi baada ya kuchaguliwa endapo angechaguliwa.
 
Mfanye kama wanavyofanya Nairobi. Magari ya binafsi hayaruhusiwi kwenda city centre isipokuwa siku za week ends tu. Siku zingine wote mpande public transport except government ministers and senior government officials kwa magari ambayo plate numbers zake zinaonyesha utambulisho huo pamoja na magari ya wagonjwa. This is the best, easiest and cheapest solution. Kwani lazima uende na gari lako kazini? Kumuonyesha nani? Hamieni mikoani kama mnataka kwenda kazini na magari yenu.
Wabongo wanavyopenda sifa za kudrive ukimwambia hiii fact atakuona kichaa.
 
Zitapatikana za kutosha na bora baada ya magari binafsi kuzuiwa kuingia mjini au yatakapoanza kutozwa ushuru mkubwa, kama shs 50,000 kwa siku kwa kuingiza gari binafsi mjini siku za kazi!!
Unaishi kwa hisia kama sio mihemko!
 
Back
Top Bottom