View attachment 800825 Kwa kizazi cha nyuma kidogo na kizazi cha hip hop nadhan washasikia sana habari za wanamuziki hawa wawili Tupac Na Biggie au B.I.G kuanzia Urafiki wao na baadaye Uhasama uliopelekea Vifo vyao. sitaki kuuza sana chai kuhusu walizaliwa wapi na kukulia wapi.najikita katika mahusiano yao kama marafiki,maadui na mwisho vifo vyao na game nzima ya Hip Hop.
Tupac na Biggie walianzaje ushkaji?
mara ya kwanza kabisa Tupac anakutana na Biggie ilikuwa mwaka
1993 huko Los angeles. USA. Biggie alikuwa akiparty na washkaji kadhaa..wakati huo angalau si haba Tupac alikuwa ametoka tayari kiaina, kwenye game anafahamika.na tayari alikuwa ameashaanza kukomaa na game sana…so Biggie akaomba kwa mshkaji mmoja ambaye alikuwa ni Muuza Unga mitaa ya kati ....kuwa amkutanishe na Mchizi Tupac. Basi washkaj wakakutanishwa ,wakapeana tano na mwishowe Tupac akaona amwalike Biggie maskani kwake. Biggie akatia timu mpaka kwa Tupac. Anasema huko alishirikiana na washkaji kibao pamoja na Tupac ku fanya mambo mengi mengi na mwishowe pia pamoja masela waka share majani,msuba,ganja.… wakiwa high ile kinoma noma Biggie anasema Tupac alivuta bag flan hivi toka kabatini rangi ya kijani. Hilo bag lilikuwa limejaa miguu ya kuku na miguu ya swala (bastola na machine guns) anuai. Wakawa wakishangaa shanga jamaa jinsi alivyokuwa na mashine nzuri kabisa ambazo zilikuwa za kisasa.. na wakiwa katika hali hiyo wakawa wanachezea chezea zile guns kule uani wakikimbizana na kutishiana. Bahati nzuri hazikuwa loaded yaani hazikuwa na njugu ndani.
Basi Mchizi Tupac baadaye akaingia jikoni kupika msosi ..ingekuwa huku maybe angeenda kusonga ugali mkubwa sana na nyama choma.na si unajua tena watu wakishavuta msuba na hamu ya kula sometime huwa inaongezeka sana.. So Tupac akaingia jikoni ili afanye makaratee mezani. kucheck kwenye jokofu lake kulikuwa na nyama, akakaanga na vyepe kadhaa na mkate waka kaa chini wakapiga msosi… daahh..ilikuwa kama party flan hivi amazing na washkaji tupu. Hakukuwa na mademu. Na hapo ndo urafiki wa Biggie na Tupac ukawa umeanza.
EDI Mean anasema walipomwona mara ya kwanza Biggie walimwona kama ni rapper flan hivi mchovu… kipindi hicho Tupac na wana wake walikuwa na Group lao walilokuwa wakiliita
OUTLAWZ. Tupac akamzawadia Biggie chupa ya Hennessy… kifupi ilikuwa ni siku ya kuparty sana kwa masela. Na usiku ulipofika Tupac akamkaribisha Biggie alale kwenye kochi. Hii ikawa ni kama kawaida kila Biggie akienda California alikuwa anaenda kulala kwa msela kwenye kochi lake.Siku moja Tupac akiwa ametia Team New York akaenda mpaka maskani ya Biggie akamchukua wakiwa pamoja kwenye Limousine Nyeupe. Tupac akawa anatembea tembea naye mitaa ya kati.
Na hapo ndo wakaenda Mpaka kwenye concert moja huko
Madison Square Garden mwaka huo 1993 wakawa wakifanya free style…..hapo biggie akiwa ameshika Mic anaflow nakumbuka alichana mistari
“ oh my God I’m dropping shit like a pigeon/I hope you re listening/smacking babies at their christenin” jamaa ni kama alipagawa kinoma yaani…. Ya know what am sayin? Cool.
Sikiliza hapa washkaji wakichana Mistari kwenye hiyo concert
So mbali na tukio hilo bado Biggie hakuwa nafahamika sana nje ya Brooklyn,Tupac ambaye alikuwa tayari anafahamika kinoma akiwa ameuza album yake kufikia mauzo ya Platinum, wakati huo huo ni mwigizaji ndo alikuwa kama anamwongoza Biggie kinamna flani. Biggie na wachanaji kadhaa waliokuwa wanachipukia.. you know.. underground rappers walikuwa wanakusanyika studio au chumba cha hotel kumsikiliza Tupac akiwapa Darsa kuhusiana na game. Tupac alikuwa anasimama kati kati yao na kuanza kuwapa darsa …haya maneno aliyasema Mshkaji wa tupac EDI Mean “ kila mtu alikuwa nasikiliza kwa makini sana mshkaji akishuka madini ile kinoma noma…tukimfuatilia kwa makini maana yeye alikuwa ameshatusua kwenye game” ila Tupac akawa anaweka msisitizo sana kwa Biggie akionesha kumkubali zaidi.
Tupac anadai yeye ndo alichangia sana kumfanya Biggie awe na style aliyokuwa nayo ya kuandika mistari.."
Nilikuwa na mwambia mshkaji kuwa …kama unataka kutengeneza mapene,unapaswa urap kwa ajili ya mademu. Usiimbe kwa ajili ya machizi. Mademu watanunua nyimbo zako…na machizi huwa wanataka kile ambacho mademu hutaka” anasema Tupac huku akitabasamu kidogo.na kama ushahidi Biggie akawa anafuata Ushauri wa Tupac...hapa katika kuonesha alivyombadilisha kuna nyimbo huwa anazitaja za kipindi cha nyuma kabisa. Nyimbo kama “
party and bullshit” hii ilikuwa nyimbo ya kigumu hasa ilikuwa jiwe ile kinoma yaani..na analinganisha nyimbo kama “
big poppa” hii nyimbo mademu waliipenda haikuwa jiwe kama ile ya kwanza…ilikuwa nyimbo flani hvi kisponge. Biggie akaona ni bora awe karibu zaid na huyu mwana so akaomba naye aungwe kwenye group lingine la Tupac lililokuw alikifahamika kama
Thug Life…. Tupac anasema “
nilimfundisha mchizi,alikuwa kama luteni wangu, msaidizi wangu kwenye game”
Lakini kabla wimbo wa “
ready to die “ haujatoka Biggie alikuwa anawasi wasi kuwa usingefanya vizuri ukichukulia kuwa alikua amesaini label ya
“BAD BOY. Iliyokuwa ikimilikiwa na meneja wake
Sean Puffy combs a.k. Pdiddy ilikuwa bado haijakamata sana kwenye game. Na akaona kama atachelewa akijilinganisha na Tu Pac. Akawa kama analalamika flani hivi kwa mshkaji wake..yaani akitaka Tupac awe Meneja wake. Akitegemea kuwa Tupac angemsaidia kupanda kwenye chati kwa haraka sana kama yeye alivyokuwa.
Tupac alikataa hilo ombi la Biggie na kumwambia “
hapana , endelea kuwa na Puffy atakufanya uwe star”
Mwaka 1994
ITAENDELEA NA KUMALIZIWA KESHO