Tupeane connection za mashamba/viwanja vya gharama nafuu

Brother Jof

Senior Member
Joined
Nov 5, 2018
Posts
114
Reaction score
153
Hello wanajukwaa,

Kama kichwa cha habari kinavyojieleza hapo juu. Naomba tupeane connection za maeneo ambayo kuna viwanja au mashamba makubwa kwa bei nafuu kwaajili ya uwekezaji au ujenzi.

Mimi binafsi niko Dar, natamani sana kupata eneo au shamba lenye rutuba nzuri angalau ekari 10 pembezoni mwa jiji au katika mkoa wa Pwani kwa gharama ya wastani wa milioni moja (1,000,000Tsh) ili nikajichimbie huko nilime na kufuga. Maeneo ninayopendelea ni kama Kisarawe, Chanika (ndanindani huko), Bagamoyo, Wilaya ya Kibaya, Mkuranga n.k.

Asanteni
 
Mkuu nishawah kusikia sehem hii ndio maana nikaja hapa nipate wadau wenye connection
 
Miono iko wilaya ya chalinze,bei laki mbili mpaka laki,usafiri toka mbezi mwisho au tegeta nyuki moja kwa moja
Labda miono ndani ndani hukooo lakini pale karibu Sasa kwa hiyo bei itamlazimu afunge na kuomba na kuwapiga upofu na dhiki wamiliki wauze Bei aitakayo.

Kule mbele ya miono maeneo ya Mandamazingara kwenyewe kumeshapanda vile barabara ya east Afrika yapita hapo.
 

Miono heka kumi kwa milioni moja?
Upande upi wa miono?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…