Tupeane maujanja ya Excel

Tupeane maujanja ya Excel

Mkuu Ethos naomba kutoa ushauri. Kwamba badala ya kwenda randomly kwa nini tusikuombe ufundishe function moja moja, labda unaanza na Vlookup then HLookUp etc.

Natanguliza shukrani zangu za dhati.
Asante Kwa ushauri wako mkuu King kan...

Nitajitahidi kufanya hivo ili mtiririko uwe mzuri..

Ni wazo zuri sana!
 
Mimi nataka kujua jinsi ya kuselect item moja mfano nauza dawa mwaka mzima kila aina nimeeanda sheet yangu yenye item elfy 3000
 
Nataka kujua metacalfin ziko ngapi, panadol ziko ngapi may na albendazol ziko ngap toka January hadi December
 
natak kujua metacalfin ziko ngap panadol ziko ngap may na albendazol ziko ngap toka january ad december

mim natak kujua jinsi ya kuselect item moja mfano nauza dawa mwaka mzima kila aina nimeeanda sheet yang yeny item elfy 3000
Karibu mkuu cc12 na Asante Kwa Swali Lako zuri!

Kuna Function inaitwa COUNTIF inaweza kutumika hapo Kwa kadiri ya maelezo yako na mahitaji..

Kama unayo list ya hizo items 3000 katika Column moja ni rahisi sana..

Peleka Cursor yako Kwenye sehemu unayotaka hiyo idadi itokee..au unaweza andaa column ingine na ipe jina Panadol... then chini andika hii formula =COUNTIF(A1:A3000,''Panadol'') hapo nimetumia A kama mfano unaweza andika kutokana na data zako zilivojipanga.

Na endelea kufanya hivyo hivyo Kwa Metacelfin, Paracetamol nakadhalika.. Kumbuka COUNTIF inahesabu idadi

Kama unaswali au hujanipata vizuri unaweza uliza

Karibu
 
TIP OF THE DAY :

Tumia Google Sheet Kwenye simu yako sio lazima. Uwe na Computer

Ingia play store andika Google Sheets halafu pakua..

Anza kufuatilia vitu vidogo vidogo wadau wanavyouliza hapa hata kama ukiwa safarini au kijiweni unapiga story..

Waswahili wanasema haba na haba hujaza kibaba...

Ukisha ipakue Kuna templates ambazo zimeshatengenezwa unaweza ukacheza nazo kupata maujuzi pia..

Kuna ya Calendar, Attendance Kwa walimu na hata Financial Statements Kwa wahasibu

Nitazielezea huko mbeleni

Enjoy!
 
Google Sheet Inafanana Na Excel!!?? @Etho
 
Back
Top Bottom