Tupeane maujanja ya Excel

Tupeane maujanja ya Excel

Asante Kwa Swali lako mkuu... Hii itasaidia wengi

Katika Excel Kuna functions zifuatazo


Ukiandika =UPPER(A1) Maneno yaliyopo katika A1 kama yapo katika small letters yatakuwa Capital letters

Ukiandika =LOWER(A1) kama yako katika capital letters yatakuwa small letters

Ukiandika =PROPER(A1) yataanza na Herufi kubwa tu


Hebu fanya na utupe feedback
Nmefanikiwa Ila sasa nakuwa nakolamu mbili za majina, nikfuta ya mwanzo na column ya pili inafutika. Haiwezekani kubadili hapo hapo kwenye original column?
 
Yes ni kazi nzuri na hapo inaonesha umeielewa VLOOKUP kisawasawa!! Congrats!!

Ila changamoto ipo hapa.. Je kama mtu kupata D ni aliye na marks kuanzia 0-30 na wapo zaidi ya kumi Kwenye list?
Me pia naipenda hii ni rahisi, labda kama ina changamoto tuambie.
 
Wakuu nilikuwa nimebanwa kidogo na Majukumu kiasi kwamba JF nilikuwa nachungulia tu na kutoka


Kuanzia kesho tunaendelea na uzi wetu huu wa kibabe..


Karibuni Kwa Maswali
 
Wadau,

Kujua Excel Spreadsheets ni muhimu sana...

Tunaweza tukashirikishana tricks mbalimbali katika Excel hapa ili tujifunze wote..

Unaweza pandishwa CHEO au Kupata kazi kirahisi Kwa kujua EXCEL vizuri.. Watanzania wengi udhaifu wao upo hapo.. So Unaifanya WEAKNESS hiyo kuwa Strength kwako.Kwenye Ofisi yeyote mtu ambaye haogopi excel huwa anaonekana ni kichwa sana.. unaweza pia ukamvutia bosi wako kama utaijua kumshinda yeye na atakufanya rafiki yako ili usimuumbue...

Kwenye Interview ndio utawamaliza kabisa ..ukikutana na viherehere wakakuchokoza hapo ndio unawaonesha ujuzi wako wote... wengi huwa hawaijui kwasababu ya uvivu... Kwa hiyo usiogope..Niliwahi ulizwa swali na panelist kwenye Interview nikaenda deep mpaka akaogopa maana kuna vitu alikuwa havijui na yeye akaamua apotezee hilo swali akarukia kitu kingine kukwepa aibu..

Weka Trick yako hapo chini ili wengine wafaidi au kama unaswali uliza nitakujibu mimi au wadau wengine...

Ingependeza sana pale unapokwama uulize swali hapa.. Ili tujadiliane vitu ambavyo ni useful katika mazingira yetu ya shule au kazini...

Dunia ya sasa sio lazima uende darasani.. Unaweza tumia muda wako na MB zako vizuri mtandaoni na ukaongeza Ujuzi polepole

**Kama unatafuta kazi na umeandika Kwenye CV kwamba una ujuzi na Excel fuatilia huu uzi na group uwe updated na vitu mbalimbali ili usije umbuka siku ukiwa unafanya written au Oral Interview

** Nitakuwa naelezea Common questions ambazo waajiri hupenda kuuliza kukupima uelewa wako katika Spreadsheets.. Ni Muda na MB zako tu.. Sihitaji kingine...

Please NOTE

** Usiulize kitu unachokijua kupima watu Bali andika trick unayoijua ili wengine wafaidi na kama unaswali ULIZA wataalam tutakusaidia



PS:
Kama upo Telegram unaweza Ingia Kwenye Public Channel ipo hapo chini Kwa vitu ambavyo haviwezekani kuelezewa hapa vizuri..Kama video na files. Ni public channel ya kusoma na Sio sehemu ya chatting!


gonga hapo >>>> Excel/SpreadsheetsTZ

Naomba kuwasilisha!

Ethos
Ebana bonge la somo shukran kwa mtoa mada japo nimechelewa kuikuta lakini nitafuatilia mdogo mdogo
 
Wakuu nilikuwa nimebanwa kidogo na Majukumu kiasi kwamba JF nilikuwa nachungulia tu na kutoka


Kuanzia kesho tunaendelea na uzi wetu huu wa kibabe..


Karibuni Kwa Maswali
mkuu vipi mbona kimya
 
Njoo upate hayo maujanja ofisini kwetu The Computer Skills (ComSkills), Makumbusho Business Complex, 2nd Floor kuanzia saa 2 asub mpka 2 usiku. You will not be disappointed. Call 0717718519
mie napenda sana ni bei gani Uko
 
Jinsi ya kutumia Excel imeandikwa kwenye Excel programme yenyewe yaani kuna user manual pale kwenye Help. Na kwenye Help kuna mifano kabisa yenye diagrams hivyo wewe ni kucheza na mfano ukileta majibu sahihi unapiga kazi unayotakiwa kufanya.
 
Nmefanikiwa Ila sasa nakuwa nakolamu mbili za majina, nikfuta ya mwanzo na column ya pili inafutika. Haiwezekani kubadili hapo hapo kwenye original column?
Ukimaliza kubadili una coppy ile uloibadili then una paste special na kwenye dialog chagua value then ok
 
Wataalam naomba msaada kwa anaefahamu VBA ya xls, ni siku nyingi nafanya kazi na xls sheet naifahamu kiasi fulani ila inapokuja issue ya developing program through xls nashindwa hata kutengeneza form ama kiprogram kidogo cha kuwasaidia end user wengine. Msaada tafadhali kwa wanaojua kupiga code za VBA xls
 
Back
Top Bottom