SUMPRODUCT ni function ambayo inatumika kupata jumla ya zao/product kati ya array mbili au zaidi (kiswahili kigumu, tutaelewana kwenye mifano)
Syntax
=SUMPRODUCT((array1),[array2],[array3].....[nth array])
Ukiona alama ya [text] imetumika kwenye syntax basi ujue hiyo ni optional, sio lazima kuiandika kwenye formula yako, hivyo SUMPRODUCT inaweza ikawa na array moja tu na ikaleta jibu (kama utaweka array moja tu, SUMPRODUCT itakuletea sum ya hiyo array pekee (eg. Sum of 1×(array))
Tuanze na mfano wa kwanza
Mfano1
Column A ina 1,2,3,4 kuanzia A1 mpaka A4 ( hii ni array ya kwanza)
Column B ina 5,6,7,8 kuanzia B1 mpaka B4 (hii ni array ya pili)
Tukiandika formula ya SUMPRODUCT kwa kutumia arrays mbili hizi (eg =SUMPRODUCT ((A1:A4),(B1:B4)) ) kitakachofanyika ni hiki
(1×5)+(2×6)+(3×7)+(4×8)=70
Unaweza ukaweka arrays zaidi ya mbili lakini inatakiwa arrays zako zote ziwe zina size moja vinginevyo itakuletea Error (mfano hapo juu array ya kwanza na ya pili zote zina element nne, ukiweka array zenye size tofauti itakuletea error ya #VALUE)
Array ikikutana na non numerical( string/text), huwa inaibeba kama zero, mfano kama tungeweka neno JF kwenye A1 basi formula ingefanya hivi
(0×5)+(2×6)+(3×7)+(4×8)=65
Sasa kuna muda utataka uweke logical argument kama array yako kwenye SUMPRODUCT (logical test/argument ni arguments ambazo huwa zinareturn TRUE au FALSE kulingana na condition iliyopewa mfano nikiandika =EXACT(A1,B1) , jibu litakuja FALSE kwasababu A1 haifanani na B1.
Sasa ili haya maneno (true na false) yabadilishwe yawe number na zitumike kimahesabu, huwa tunaweka double negative kati ya equal sign na function
(value ya true huwa ni 1 na value ya false ni 0)
Mfano
Tukiandika =--EXACT(A1,B1) jibu litakuja 0 ambayo inawakilisha neno la FALSE (kama jibu lingekuwa true, basi ingekuja 1) utaona matumizi yake ktk mfano unaofata
Mfano wa SUMPRODUCT ambao una logical test
Assume Column C ina 2,4,6,8 na column D ina 3,4,9,8
Tukitumia SUMPRODUCT (=SUMPRODUCT (--(EXACT((C1:C4),(D1😀4)),(D1😀4))
Kifatachofanyika ni hiki
(0×3)+(1×4)+(0×9)+(1×8)=12
C1 haifanani na D1, halikadhalika C3 na D3 ndio maana jibu limekuja 0, lakini C2 inafanana na D2, halikadhalika C4 na D4 ndio maana jibu limekuja 1.
Kama tusingeweka double negative kwenye function ya EXACT maana yake SUMPRODUCT ingekuwa inaleta zero kila inapokutana na true ama false kwa sababu true na false ni text sio number.
Ngoja tuishie hapa, baadae nitaendelea na matumizi ya SUMPRODUCT kufanya LOOKUP kama inavyofanya Vlookup/Hlookup au INDEX with MATCH