Leo tuangalie kazi ya FILL
Kuna muda unakuwa na list ndefu mfano unataka uandike namba kuanzia 1 mpaka 1000 kwenye column A , hapa unaweza ukaandika 1 kwenye A1 na 2 kwenye A2 then ukadrag lakini itakuchosha sana.
FILL inarahisisha kazi na kufill series yako bila formula wala kudrag.
Andika namba ya mwanzo unayotaka ianze (mfano 1 kwenye A1) piga enter then select cell yako, baada ya hapo click FILL(FILL ipo kwenye categories za home tab,upande wa kulia mwishoni mwishoni )
Ukishaclick,kuna list itakuja ,chagua series.
Baada ya hapo kuna kibox kitakuja, chagua column kama unataka series yako ikae vertically, au row kama unataka series yako ikae horizontally.
Kuna option nyingine hapo kati, kwa huu mfano wetu tutachagua option ya linear.
Chini kabisa utaweka step value ambayo ni 1 kwa hii case yetu, na stop value tutaweka 1000 then click OK utaona series yako imejifill ktk column A.
Matumizi yake ni mengi, kwa mfano huu nadhani mtakuwa mmepata mwanga wa kutumia hiyo fill, unaweza ukaitumia kufanya autofill ya task mbalimbali bila ya formula ama kudrag