Tupeane mawazo wapendwa

 
hili post ukichanganya na hayo ma lips mie kwisha habari yangu. naomba nikuwe msomaji tu kwenye hii sred

Kloro inabidi ubandike hizi lips kwa wall yako..ha ha Eniwe, haya maisha inabidi mtu utafakari mara mbili mbili maamuzi unayochukua kuambatana na jinsi maisha yanavyokuendea. Hakika nitavumilia kinachovumilika laa sitowezi kuishi na mume kwa roho ya chuki, hasira na uadui sababu ya watoto. Ndio mana nikisikia watu wameachana najua si jambo rahisi!!

Unaweza ukawajali watoto wakawa na msingi imara kimaisha kwa kulelewa na mzazi mmoja au walioachana..kila mtu na package yake katika maisha haya!!..mwingine unaweza kuwa kwenye ndoa hajali hao watoto kabisaa mpaka watoto wanaelewa hali ya nyumbani na kuathirika kimalezi!!

Siyo kwa vile kuna kitu uvumilivu basi mtu uvumilie mpaka uvumilivu wenyewe unakwambia enaf! Life hii imejaa scenario nyingi..

Upande mwingine
Maisha ya ndoa na changamoto zake ukipata mtu ambaye mnaelewana vizuri, kuwasiliana hata mkikwaruzana, kusikilizana, kujali familia, na mambo yote mazuri hapo safi kabisa..tena kama mwanandoa mwenzio ni kama besti frendi wako inapendeza siyo cheo cha mke na mume hamtaniani wala kuwa huru kila mmoja wenu..Tatizo ni kukutana na mtu wa aina hiyo, naona mara nyingi hasi zinakutanaga na chanya!!
 
Mpendwa hapo umenena sawa,na ndivyo hata biblia inasema mwanaume anapaswa kumpenda mkewe na vilevile wanawake wawatii waume zao
 
kuachana sio dili but sometime inabidi, kupata muda wa kufikiri na kuheshimu maamuzi....... D knob
 
True that!Mmoja anaweza kuweka juhudi kwenye kujenga mwingine kubomoa!Hapo hamtafika popote zaidi ya kuishia kuishi maisha ya kukomoana!

sred klosed
 


Kumradhi,
...sijui kwanini mmeweka kigezo cha usomi kwenye mada hii.
Inahusiana vipi, labda mimi sijaelewa.

Apart from that, binafsi naamini zipo irreconcilable differences ambazo
mkijilazimisha kuishi pamoja, matokeo yake ni uadui ambao mmoja wenu
huenda akajipatia hata maradhi kutokana na msongo wa mawazo.
 
Happnines is within you, you have never been happy since you born? Unataka huyo mwanamke au mwanaume afanye muujiza gani kuja kukufurahisha wewe ambayo hujawahi kufurahi?

Hivi tunapozungumzi ndoa kuna watu wanaelewa kweli? Sometimes watu wanafanya utani na maisha ya watu wengine. Unaolewa leo kesho unakuwa na jeuri ya kusema eti funga kilicho chako urudi kwenu? Kwa nini? wewe ni nani kusema hivyo? Its the right tine to cast those DIMONS, jengeni utamatuni wa kusoma vitabu vihusuvyo maisha, how to behave, mwenzio akikosea basi wewe rekebisha siyo na wewe kesho ufanye kosa lake kwa excuse kwamba naye alifanya hukusema.

Hawa watoto waliorundikana mitaani tutamwambia nini Mungu wetu? Women I urge to learn how to pray, nyien ndo wamama wa nyumbani, vinara, na madereva wa nyumbani. Chochote kinachotokea nyumbani watu watakutangalia wewe, hata mumeo akikutwa anafanya upuuzi barabarani wanasema hivi kweli ana mke yule? That means wewe ungeshakemea tabia hiyo kirahisi na si kumwacha akafanya anavotaka.

Kumbukeni mke na mume ni watu wawili waliokutana ukubwani, kila mtu amekuwa na tabia yake toka huko alikotoka, kukemea tabia ya mwenizo itoke unahitaji upako wa hali ya juu, maombi ya kufunga na kukesha ukimaanisha kurudisha kile kilichopotea. Ebu fikiria, kama unaachana na mumeo ni nani aliyemwema? THERE IS NO PERFECT MAN IN THIS EARTH, we all learn thorough our mistakes. Usichukulie kosa la mwenzako kuwa chanzo cha tatizo ongea mpaka Yesu atokeze kuachana NO. Nyie mnaotaka kuishi maisha ya raha, amani na starehe nyingi bila kubanwa kwa taarifa yako "If you never been happy since you born who do you think can make you happy" Utazunguka milima na mabonde, unatafuta amani na furaha kwa mtu baki wakati wewe mwenyewe hujifurahishi au kujipa amani"

Wanawake oneni mbali, fungukeni macho, mlilie Mungu akutengenezee njia naamini anatenda, mwaminifu, hana ubaguzi. Alikujua kabla hujatoka tumboni mwa mama yako.

NI changamoto ila kuachana siyo SULUHU. Take precautions GIRLS. Be blessed.
 
....
Apart from that, binafsi naamini zipo irreconcilable differences ambazo
mkijilazimisha kuishi pamoja, matokeo yake ni uadui ambao mmoja wenu

huenda akajipatia hata maradhi kutokana na msongo wa mawazo.



Hizi differences ila wengi wanazisema, mimi najua moja tu ya kucheat (anyway wengi wetu tunaisamehe pia). Hizi nyingine ni zipi?
Tufunguane macho please tusijeishia kwenye uadui na watu tunaodhani kuwapenda.
 

Pole Mbu hapo kiwango cha elimu nimeweka kwenye post yangu kwa kuwa mtoa mada amekizungumzia kama mojawapo ya sababu za kuvunjika kwa ndoa nyingi au chanzo cha matatizo . Ndio nikawa najaribu kumwelewesha kuwa inategemea na hulka ya mtu na ulimbukeni wake... kuna waliosoma na kusoma awe mwanamke au mwanaume lakini akijua jukumu lake kama mama/baba au mme /mke mambo yanakuwa swari tu.....si kila ndoa za wasomi zina matatizo spo tunarule out variable ya usomi a.k.a. kiwango cha elimu katika kuexplain matatizo au kuvunjika kwa ndoa.
 
Nafikiri huwa wanakosa roho za uvumilivu ingawa hakuna sababu ya kuvumilia maumivu.
 
hivi mpaka mnaoana hukujua si chaguo lako?tuache tamaaa ndoa zitadumu

Mike1234 hili ni swali zuri sana......mimi nafikiri si vema kutumia sentensi au sababu hii eti hakuwa chaguo lako .......nafikiri ULIMCHAGUA ndipo ukamwoa unless umechaguliwa na wazazi ndo unawezasema hakuwa chaguo lako. Hii ni lame excuse kwa kweli. Uko sahihi pia kuwa tamaa zimetuzidi, unacho ndani but unaona kilichoko nje ndo kizuri zaii ........ni kama mpenzi wa chipsi............. akikaangiwa nyumbani katika hali ya usafi hazinogi anatamani chipsi vumbi......................Jamani ndoa si lelemama

Hovi hatujiulizi jinsi tu ilivyo ngumu kumlea mtoto uliemzaa mpaka akakuelewa sembuse mtoto wa binadamu mwingine ambaye mmekutana akiwa na meno yake 32 kamili?? kama hakuelewi hatokaa akuelewe hata umbembe mgongoni kila siku asubuhi
 
Reactions: Mbu
Lazima mtendeane Haki jamani mwenzio ana kiu wewe ndo kwanza unajifunika blanketi unataka hiyo kiu akaitoe wapi?

Sasa ndo hapa unaona umuhimu wa nyumba ndogo mzee anaamua kujitafutia kiform iii kiwe angalau kinampa massage.

Fide ulishawahi hata siku moja kujiuliza why mamsap anatoa sababu ya kuchoka?? Jamani kina baba msijisahau.........kupata huduma kwahitaji maandalizi, mbona mkiwa mwahitaji huduma za hospital au benk huwa mwajiandaa?? Hata huduma hii pia mnatakiwa kuandaa vizuri mazingira.....wewe umeamka asubuhi kama ndo umejaliwa kupata "breakfast' basi indicate kuwa hata jioni unatarajia.........sio kukaa kimya na kusubiri ifike jioni 'ugonje sahani' kama ishara ya kutaka chakula ..la hasha............sifia....baada ya ;breakfast' kama umebahatika chombeza hata kwa neno moja aumawili ...I cant wait menu ya jioni........ ni signal tosha kwetu sie kuwa leo bwana anahitaji kunifurahisha na mie nijiandae........asa wengine unahudumiwa asubuhi unagumia tu husemi hata aksante kwa kahawa..........afu ukirudi usiku na mipombe yako unageuza tu sahani upande wako...jamani sometimes na sie tunajisikia vibaya...hakuna tofauti na bosi wa ofisini anavyokutreat na mikazi yake ....ndo hapo mwapata visingizio vya nimechoka n.k.
 
Reactions: Mbu
Nnunu nimeshaingia kazini. Nachoweza kusema kuhusu nyumba ndogo si kuwa inarekebisha nyumba kubwa ila inafanya husband arudie vows. Maana nikigundua kuna kimada mziki wake ni lazima urudie maneno yote mazuri ulonambia toka tuna date mpaka unaapa kanisani. Haa. Mwanzo wife anakuwa na hasira, baada ya muda anashukuru nyumba ndogo kwani amefufua mapenzi katika ndoa. Kwa experience yangu wanaume wakibambwa wanarudisha descipline na mapenzi yana double! Na hii si kurekebisha nyumba kubwa ila inamfanya mume nae atie akili. Unafikiri ni rahisi ku divorce mke alokuzalia watoto wanaokufanya nawe uitwe kidume.

Mimi nina experience ya ndugu yangu yaani mume wake alicheat alafu yeye mwenyewe cheater ndo kaita kikao cha wana familia kwani anaogopa ndoa isije vunjika.

Inawezekana mkikaa bila hawa vicheche ku interrupt ndoa yenu ndoa ikawa boring. Hizo ndo challenges zenyewe. Ila sasa kilichoharibu maradhi!


 
Kipato ni matokeo. Wengi wanaoana wakiwa hawana kitu zaidi ya Elimu. Baada ya muda ndo unakuta mmoja kajaaliwa zaidi ya mwingine. What is money by the way. How can you compare those papers with LOVE?

 
Hizi differences ila wengi wanazisema, mimi najua moja tu ya kucheat (anyway wengi wetu tunaisamehe pia). Hizi nyingine ni zipi?
Tufunguane macho please tusijeishia kwenye uadui na watu tunaodhani kuwapenda.

...mnh FA wala sikutajii! ...Mw'mungu akupitishilie nazo mbali uishi na mumeo mpaka kifo kitapowatenganisha.
Mimi na Mwj1 twajua kilichotukumba, tuacheni hivi hivi, LOL!

The topic is hot...Ndoa yangu bado changa so naobserve na kulearn... Thanx Maty kwa kuanzisha hii thread... Okey, 2endelee...

Mkare, there's no need to learn/go deep on this topic, observe 10 commandments, na mtangulize Mw'mungu ndoa yako itasimama. Thread hii haina mantiki ya kuzijenga ndoa. Ni dongo letu sie 'wajane!' acha tupambane nalo!
 
Nafikiri huwa wanakosa roho za uvumilivu ingawa hakuna sababu ya kuvumilia maumivu.

...hapo sasa,...!

Unajua mambo haya yasipokukuta, huoni justification yeyote ya kuachana.
"Kitanda usichokilalia," ni ngumu kujielezea/kueleweka pale utaposema 'enough is enough!'.

...acha tu niendelee kubugia popcorn zangu hapa 😛op2:...si muda mrefu
atakuja mtu hapa na post yake 'keshatendwa!' haoni tena thamani ya maisha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…