Tupeane mawazo wapendwa

 
Ulokole peke yake hautoshi kusimamisha ndoa...
Ndoa ina nguzo zake, kama kuheshimiana, kusikilizana, Upendo, Hekima etc etc...
.. maana mnaweza mkaishia kushusha mapazia nje ya ratiba, ha ha haaa!.

Nadhani wengi wetu tunahitaji more, hatuzingatii ipasavyo au hatujui nini heshima, masikilizano na upendo unaotakiwa kwenye ndoa. Labda imefika wakati wa kufafaua haya na kutaweka sawa ili kila mmoja wetu ayaelewe kabla hajaingia kwenye ndoa.
 

Dear maty yaani leo umegusa mtima muhimu sana katika maisha yetu ya sasa. Kusema ukweli hal hii inatisha na kwa bahati mbaya sana ndio kwaaanza inakamata chati kwa kasi. Sometimes nasema bila kumtanguliza MUNGU katika ndoa na maisha yetu, mambo kama haya ni inevitable kabisa. Na kama ulivyosema ndoa za wenye viwango flani vya elimu mamb ndo huwa magumu zaidi kuliko ndoa ambazo wanaume ndo wenye elimu au mali kuliko wanawake. Kwenye ndoa ambayo wenzi wote wana viwango sawa vya elimu au kipato mara nyingi kuna mambo ambayo katu hayatavumilika na pande yoyote kati yao. Mf. Katika ndoa kama hii kwa wale wanaume wenye tabia ya kunyanyasa wanawake kwa kisingizio kuwa ni mkewe na hapaswi kuuliza, hoji au kufuatilia mambo anayoyafanya yeye kama mume ni wazi akileta ubabe kwa vitu ambavyo ni obvious mke atapata kichwa kuwa asimbabaishe.
hali kadhalika mke anawezakuwa ndo chanzo cha matatizo especially kama naye akikinga mkono kiganja kinajaa....... anawezajikuta analeta hadithi za usawa mpaka kwenye kugawa dozi............jana nilikupa leo nami napumzika (utadhani akitoa anayefurahia ni mpewaji tu). Sasa kwa mwanaume mwenye mke wa hivi ni lazima hatakubali na ataona ni bora atafute amani huko inakopatikana.

Ni tofauti na nyumba ambayo mke ni msomi, mume msomi but kila mtu anajua na kutimiza wajibu wake kama mume/mke na kama Baba/mama. Hawa wataishi kwa amani pamoja na kuwepo kwa migongano ya kawaida, heshima inatawala zaidi na kila mtu anatambua thamani ya mwenzie. Kinyume cha hapo ni kutengana.
wa maisha halisi ya w



Darling maty...........when worse comes to worse sometimes ni bora mkatengana kuliko kuwakuza watoto katikati ya uwanja wa vita. Madhara yake ni makubwa kuliko yale wanayoyapata kwenye utengano kwani huko unawezakupanga mpangilio maalumu. Kulea watoto ndani ya ndoa yenye migongano kila kukisha (sisemi ile ya kawaida) but sometimes watu wanakuwa na irreconciliable issues ambazo nyingine wanashindwa kabisa kuzicontant na kutozionyesha kwa watoto. Mfano kupigana, kutukanana, kunyanyasana n.k. madhara ni makubwa sana kisaikologia kwa watoto wanaokulia ndani ya familia za aina hizo na usijeshangaa mtoto akakua na yeye kuwa violent au na tabia za ajabu kwa familia yake........ni effect aliyoipata wakati anakua na ameichukulia ndivyo ndoa zilivyo au zinavyotakiwa ziwe. Mtoto anayekuwa kwenye familia ambayo mama yake haeshimiwi, ananyanyaswa na mama huyo kukaa kimya naye atachukulia kuwa ndivyo mke mwema anavyopaswa kuwa...so mkewe akiwa tofauti tu ni tatizo. The same kwa watoto wa kike, kama baba ananyanyaswa, anatukanwa au anapigwa watategemea kupata wenzi wenye nidhamu kama baba yao.

So I dont think kuwa mara zote kutengana ni kuwadeprive watoto amani. ila tu kuwe na zingatio kubwa katika kujaribu kuwaelewesha why hali imekuwa kama ilivyo (epuka kuonyesha ubaya wa mwenzi wako kwa watoto)


Maty unauliza maswali mengii............. kuhusu kama ni suluhisho ninawezasema ndio na hapana. Itategemea unapoamua kuachana na mwenzi wako umejipangaje kukabili maisha yako ili usijikute kwenye wakati mgumu utakaokufanya ujutie maamuzi yako. Lakini vile vile kabla hujaamua "mimi sasa basi" ni vema ukachukua muda mzuri wa kukaa na kutafakari ili kujidhihirishia kuwa unachukua uamuzi sahihi na changamoto zake unazijua vema na una mikakati ya kukabiliana nazo. Epuka kuamua kwa hasira. Itakuumiza mwenyewe.

Kuhusu kuoa/olewa tena...............uhmmmmm inategemea na kama uliamua kuufungua tena moyo wako kwa mwingine na kama maamuzi yako ya kuolewa/oa yalishirikisha experiences ulizozipata kwenye ndoa yako ya mwanzo. Usikurupuke kwa kuwa tu kuna jamaa kakutamkia anakupenda na wewe ukataka kumdhihirishie mtalaika wako kuwa "yeye alipokuwa akisema wa nini, kuna walokuwa wanajiuliza watakupata lini" utaumbuka.

Usinisahau kadi ya mwaliko mamito
 


yaani jamani v2ko vyako mie vinaniacha hoi,hahaha nimecheka kwa nguvu zote sio mzima kabisa wewe haki ya nani vile.
 

hivi kile kitufe cha thanks nani kakiona?

ntarudi baadae aisee..
 
kaka/dada mcdhani kuna mtu anapenda kutengana na mwenzi wake na mkumbuke kuna mengine hayazungumziki/hayana suluhisho/yameshindikana...ikiwa hivyo inabidi tu.

Hapa ndo unapo ona ile point yangu ya zamani hit and run inavyo kuwa nzuri.
 
Jamani samahani sikujua kuwa njimeandika makitu marefu hivi duh..........wapi wanatoa mafunzo ya hatimkato?
 
Tena nakwambia Nyamayao ukikuta mtu ana imani zake utakoma kumbadili ni ngumu sana sikuzote ana amini ayafanyayo ni sahihi mpaka unabaki kujiuliza anayetakiwa kumsemea hayo ni nani ,waeza amini unafanya yaliyo sahihi kwa mwenzako kumbe ni kero tupu.




 
Katika hili naomba tuwe wakweli na wawazi kabisa, mwanamke analaumiwa kwa vile ni mwanamke lakini si ndoa zote zenye matatizo wanawake ndio tatizo, no no no no and big no!!!!!!!!! Nina mfano mzuri kabisa wa mwanaume mwenye gubu lisiloelezeka! Angalia kwanza
Mwanaume form iv
Mwanamke Masters
Mwanaume baba wa nyumbani
Mwanamke anafanya kazi yenye akili
Mwanamke ndo anaendesha familia including yeye mwanaume hadi gari mwanaume kamnunulia na mambo mengine meeeeengi
Lakini cha ajabu na kushangaza mwanaume hajatulia na ana gubu acha tu hadi watu wanamuonea huruma mwanamke. Sasa hapo utasema wanawake wana matatizo jamani? Mwanaume na mwanamke woooooote wanapaswa kuheshimiana kama mke na mume si jukumu la mwanamke pekee!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Inategemea unawaza nini maishani mwako. Kama unadhani kila kitu ni mteremko maishani basi ndoa siyo mchezo. Ukisikia mtu anakwambia nina miaka kumi ndani ya ndoa, jua kuna mishale mingi, mvua nyingi zimemnyeshea lakini amevumilia. Dunia ya sasa watu tunakosa uvumilivu, hata mumeo ama mkeo awe mbaya vipi, kuna moment mnashare ambazo kila mmoja anakuwa na furaha. Kugombana ndani ya ndoa ni kitu cha kawaida sana. Kinachahitajika ni kumuelewa mwenzio na yeye pia akuelewe. Kila mtu alizaliwa na kulelewa na wazazi tofauti, pia malezi nayo yanatofautiana. Kwa hiyo mlipokutana kila mtu alikuwa na tabia yake. Ku-i-shape hiyo tabia ya kila mmoja siyo tendo la siku moja. Uvumilivu unahitajika sana. Suluhisho siyo kukimbilia kuachana bali kuwaza ni wapi tunapokosea mpaka tushindwe kuishi. Jambo lingine linalotuharibu, tunaiga sana tamaduni za wenzetu. Wao kuoa na kuolewa ni fashion, believe me.. huwa wanaumia sana pia inapofika wanapoachana. Cha kujiuliza ni kwa nini wanakimbilia sana kuachana na mwisho wa siku wanalia divorce inapokuwa finalized??? All the best kwa wenye ndoa kama mimi..
 
Jamani samahani sikujua kuwa njimeandika makitu marefu hivi duh..........wapi wanatoa mafunzo ya hatimkato?

Ujifunze kuandika vifupi vifupi maana wengine tunashindwa kusoma mpaka mwisho tunasoma mwanzo katikati ya mistari na mwisho
 
Tena nakwambia Nyamayao ukikuta mtu ana imani zake utakoma kumbadili ni ngumu sana sikuzote ana amini ayafanyayo ni sahihi mpaka unabaki kujiuliza anayetakiwa kumsemea hayo ni nani ,waeza amini unafanya yaliyo sahihi kwa mwenzako kumbe ni kero tupu.

mie naamini kumbadili m2 mzima ni ngumu sana, huwa nawapa pole sana wale wanaoingia kwenye game kwa imani kwamba Asprin ni mlevi/mhuni wa kutupwa lakini mbeleni nitambadilisha, nabakiaga nashangaa, ni bora uingie ukikubaliana na alivyo huku ukiendelea kumbadili ukifanikiwa sawa, ikila kwako ujue uliamua mwenyewe tokea mwanzo...kumbadili kiumbe ni kitu kigumu sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…