Huwa najiuliza mara nyingi lakini nakosa jibu zuri, naomba nipate mawazo tofauti tofauti, inaweza kutusaidia wengi wetu.
Wanandoa wengi hasa wa miaka ya sasa, wakikorofishana korofishana baada ya muda wanachoamua ni tuachane bwana kila mtu ataanza nataka niishi kwa amani, nahitaji furaha mimi maisha yenyewe mafupi haya. Ukute hiyo ndoa baba msomi ana kazi nzuri na mama vile vile ndio balaa, kila mtu anasema usinibabaishe ninaweza kumudu maisha.
Dear maty yaani leo umegusa mtima muhimu sana katika maisha yetu ya sasa. Kusema ukweli hal hii inatisha na kwa bahati mbaya sana ndio kwaaanza inakamata chati kwa kasi. Sometimes nasema bila kumtanguliza MUNGU katika ndoa na maisha yetu, mambo kama haya ni inevitable kabisa. Na kama ulivyosema ndoa za wenye viwango flani vya elimu mamb ndo huwa magumu zaidi kuliko ndoa ambazo wanaume ndo wenye elimu au mali kuliko wanawake. Kwenye ndoa ambayo wenzi wote wana viwango sawa vya elimu au kipato mara nyingi kuna mambo ambayo katu hayatavumilika na pande yoyote kati yao. Mf. Katika ndoa kama hii kwa wale wanaume wenye tabia ya kunyanyasa wanawake kwa kisingizio kuwa ni mkewe na hapaswi kuuliza, hoji au kufuatilia mambo anayoyafanya yeye kama mume ni wazi akileta ubabe kwa vitu ambavyo ni obvious mke atapata kichwa kuwa asimbabaishe.
hali kadhalika mke anawezakuwa ndo chanzo cha matatizo especially kama naye akikinga mkono kiganja kinajaa....... anawezajikuta analeta hadithi za usawa mpaka kwenye kugawa dozi............jana nilikupa leo nami napumzika (utadhani akitoa anayefurahia ni mpewaji tu). Sasa kwa mwanaume mwenye mke wa hivi ni lazima hatakubali na ataona ni bora atafute amani huko inakopatikana.
Ni tofauti na nyumba ambayo mke ni msomi, mume msomi but kila mtu anajua na kutimiza wajibu wake kama mume/mke na kama Baba/mama. Hawa wataishi kwa amani pamoja na kuwepo kwa migongano ya kawaida, heshima inatawala zaidi na kila mtu anatambua thamani ya mwenzie. Kinyume cha hapo ni kutengana.
wa maisha halisi ya w
Hapo kuna watoto mmezaa, lakini kila mtu utamsikia napenda kuishi kwa amani, ni vipi kuhusu watoto? Je hao hawatakiwi kuishi kwa furaha na amani wakiwa na baba na mama? Hivi hamuwezi kukaa mkazungumza na kuelewana ili mlee watoto pamoja badala yake mnafikiria kuachana?
Darling maty...........when worse comes to worse sometimes ni bora mkatengana kuliko kuwakuza watoto katikati ya uwanja wa vita. Madhara yake ni makubwa kuliko yale wanayoyapata kwenye utengano kwani huko unawezakupanga mpangilio maalumu. Kulea watoto ndani ya ndoa yenye migongano kila kukisha (sisemi ile ya kawaida) but sometimes watu wanakuwa na irreconciliable issues ambazo nyingine wanashindwa kabisa kuzicontant na kutozionyesha kwa watoto. Mfano kupigana, kutukanana, kunyanyasana n.k. madhara ni makubwa sana kisaikologia kwa watoto wanaokulia ndani ya familia za aina hizo na usijeshangaa mtoto akakua na yeye kuwa violent au na tabia za ajabu kwa familia yake........ni effect aliyoipata wakati anakua na ameichukulia ndivyo ndoa zilivyo au zinavyotakiwa ziwe. Mtoto anayekuwa kwenye familia ambayo mama yake haeshimiwi, ananyanyaswa na mama huyo kukaa kimya naye atachukulia kuwa ndivyo mke mwema anavyopaswa kuwa...so mkewe akiwa tofauti tu ni tatizo. The same kwa watoto wa kike, kama baba ananyanyaswa, anatukanwa au anapigwa watategemea kupata wenzi wenye nidhamu kama baba yao.
So I dont think kuwa mara zote kutengana ni kuwadeprive watoto amani. ila tu kuwe na zingatio kubwa katika kujaribu kuwaelewesha why hali imekuwa kama ilivyo (epuka kuonyesha ubaya wa mwenzi wako kwa watoto)
Hivi kuachana ni suluhisho la matatizo yako? Na je ukiachana na mwenzio ndio kusema hutaki kuoa/kuolewa tena? Na je ukioa/olewa halafu huyo mwingine akawa na matatizo pia pengine kuliko uliyoyakimbia mwanzo utaachana nae pia? Au utavumilia?
Tushirikiane kupeana mawazo wandugu
Maty unauliza maswali mengii............. kuhusu kama ni suluhisho ninawezasema ndio na hapana. Itategemea unapoamua kuachana na mwenzi wako umejipangaje kukabili maisha yako ili usijikute kwenye wakati mgumu utakaokufanya ujutie maamuzi yako. Lakini vile vile kabla hujaamua "mimi sasa basi" ni vema ukachukua muda mzuri wa kukaa na kutafakari ili kujidhihirishia kuwa unachukua uamuzi sahihi na changamoto zake unazijua vema na una mikakati ya kukabiliana nazo. Epuka kuamua kwa hasira. Itakuumiza mwenyewe.
Kuhusu kuoa/olewa tena...............uhmmmmm inategemea na kama uliamua kuufungua tena moyo wako kwa mwingine na kama maamuzi yako ya kuolewa/oa yalishirikisha experiences ulizozipata kwenye ndoa yako ya mwanzo. Usikurupuke kwa kuwa tu kuna jamaa kakutamkia anakupenda na wewe ukataka kumdhihirishie mtalaika wako kuwa "yeye alipokuwa akisema wa nini, kuna walokuwa wanajiuliza watakupata lini" utaumbuka.
Usinisahau kadi ya mwaliko mamito