Tupeane mawazo wapendwa

Ukifikiria mara mbili mbili naona kama ni bora kubaki single hivi, nimenufaishwa na mawazo yenu wote, naona bora nibaki single tu

But ukifikiria mara ya tatu, utaona kuwa kubaki single nako hakuna maana. Mungu ametupa maisha tuyaishi, sio tuyakimbie...
 
Ukifikiria mara mbili mbili naona kama ni bora kubaki single hivi, nimenufaishwa na mawazo yenu wote, naona bora nibaki single tu

Maty usiogope kuingia kwenye ndoa kiasi hicho,
kwa sababu siyo kila ndoa ina matatizo makubwa sana ambayo hayazungumziki na kutafutiwa ufumbuzi.

UKIPATA MTU MNAYEKUBALIANA KUITENGENEZA NDOA YENU VIZURI basi aah raha mstarehe kila kikwazo kinapojitokeza hamuiti tatizo bali mnaita changamoto, na maisha ya ndoa yataendelea kuwa ya raha bin mstarehe.

Nimesoma comments za wana JF wote lakin SIJAONA comments YA NYUMBA KUBWA naona leo hayupo on line,

Yeyote atakayemwona NYUMBA KUBWA amwambie nina RB yake haraka sana naomba achangie hii thread....lol, pia nataka anipe ufafanuzi wa ile comment ya FIDEL aliyosema ,
eti nyumba kubwa inarekebishwa na nyumba ndogo,
hata sijui atasemaje katika hili.....lol.
 

thanks..

Nafikiri ni busara watu kufanyia kazi ndoa, na kutokuiacha isijendeshe yenyewe..unaposema unampenda mtu (You are in love with someone) maana yake upo tayari kuvumilia, kuondoa kiburi, kutokuwa mbinafsi (kuishi kwa ajili ya mwenzako),na kutomtendea mwenzako mabaya..

Hakuna kitu kizuri kama ndoa ikiwa walioingia kwenye ndoa wanajua nini kilichowaunganisha. Inapendeza sana pale unaposhirikiana na mwenzako mkiwa ndani katika kushauriana,kutiana moyo, kubembelezana.

Ni kweli ndoa zina matatizo, lakini hii threads ime-address negative nyingi kuliko faida. Na kuna mtu (Nyumba Kubwa) anasema kuwa si rahisi watu kuzungumza mazuri ya ndoa kwa sababu yanakosa 'attention'... si rahisi mtu kuja hapa na kuanza kumsifia mkewe au mume wake.
Kwa wale wanaojiandaa kuwa wake wema wangependa kupitia hii blog hapa (Ndoa « Women Of Christ)
Mabinti wa JF jueni nyie ndo mna nafasi ya KUIDUMISHA ndoa au KUIBOMOA
 

Mpendwa ushauri mzuri sana huu ubarikiwe
 

Thanks tuko, naisubiri hiyo thread kwa hamu, maana inawezekana mtu unataka kuongea na mwenzio kwa mema ila jinsi ya kumuongelesha unakosea, badala ya kujenga ndio unabomoa kabisa
 
MPENDWA...Ndoa sio ya mtu mmoja hivyo haiwezi kuangushwa au kujengwa na mmoja tu.Kama mmoja anajenga na mwenzake anabomoa hawatafika popote...kinachohitajika ni kusaidiana, hapo tu ndio ndoa itafanikiwa!
 
Mpendwa ushauri mzuri sana huu ubarikiwe

ubarikiwe na wewe pia!

Binafsi nimeshuhudia kwa jinsi ambavyo wanawake wanavyoweka juhudi kubwa kuhakikisha watoto wana maisha yanayostahili (pale ambapo mume haoneshi juhudi)..Wataenda kukopa, watafanya biashara, n.k.

Swali, kwa nini juhudi kama hizo usimuoneshe mumeo katika kutunza ndoa yenu..lakini unathamini watoto, ambao kesho keshokutwa watakuwa na maisha yao..
Ni kweli si kila tatizo la ndoa lina ufumbuzi, lakini kama mtu unaingia kwenye ndoa una hakikisha ndoa yako inasimama kwa gharama yeyote ile. Wengi wetu tunanyenyekea kazi zetu za maofisini, tunahakikisha hatufanyi mambo ambayo yanaweza kupelekea kufukuzwa kazi.
Ni vyema mume na mke wakafanya hayo katika ndoa.
Ikivunjika na ivunjike...lakini unakuwa umefanya kwa sehemu yako. Hizi ndoa za Hollywood, na kwenye tamthilia za ITV ni maigizo yale..Ndoa sio kitu cha KUJISIKIA, ni kitu cha KUKIFANYIA kazi kila siku kwa sababu kukutanisha tabia za watu wawili waliolelewa na kukulia katika mazingira tofauti si jambo dogo.
 
MPENDWA...Ndoa sio ya mtu mmoja hivyo haiwezi kuangushwa au kujengwa na mmoja tu.Kama mmoja anajenga na mwenzake anabomoa hawatafika popote...kinachohitajika ni kusaidiana, hapo tu ndio ndoa itafanikiwa!

Yeah..ni kweli..
DEFINITION ya upendo ni nini??
Kama kweli anakupenda, maana yake atakulinda, atakuwa tayari kufanya chochote kwa ajili yako..UPENDO is a two way traffic (lakini ni jukumu la mwanaume zaidi).. (wanaume wanaambia na vitabu vya dini, PENDENI wake zenu, na wanawake wanaambiwa, MUWATII waume zenu)

mwanaume kama hawezi KUPENDA, ndoa itakuwa matatani,
na mwanamke kama hawezi KUTII ndoa itakufa tu..(tunaweza kutumia busara zetu, akili zetu, na mambo mengine, lakini kama hayo mambo hayatelekwezi, usitegemee ndoa itakuwa nzuri)
unatakiwa utafute mwanaume atakaye-KUPENDA na utakaye-MTII.
 

Mpendwa nakubaliana na wewe, ila kuna ndoa nimeshuhudia mwanamke anafanya kila awezalo kumuhudumia mume na kuonyesha anavyomjali na si huyo tu na watoto pia anahudumia yeye, matokeo yake ndio kwanza mwanaume anajawa na kiburi kwa kuona mke wangu ananipenda sana basi vituko haviishi
 


HATA SIJUI KWANINI WAMETOA THANKS, NATAMANI WANAJF TUANDAMANE ILI UONGOZI WA JF WARUDISHE THANKS....lol
manake naona like kwa point kama hii hailingane kwa uzito.

THANKS, MPENDWA kwa 100% kwa uelewa wangu huu mdogo.
 
yani umesema vizuri mpaka nimetabasamu ubarikiwe sana.

 

ni kweli,,huyo mwanaume haijui nafasi yake katika ndoa.. alipaswa aketishwe chini afundishwe nini maana ya ndoa.

Siku hizi tuko radhi kutenga muda mrefu kujifunza STYLE za SEX, tutasoma kila kitabu... lakini wengi wetu hatuna muda wa kujifunza jinsi ya kuimarisha NDOA, utumie njia gani kuepusha migogoro, jinsi gani ya kuwezesha mawasiliano yadumu n.k

Pia ni muhimu kutafuta msaada wa Mungu ili atuongoze tundokee kwenye mikono ya watu ambao tutakuwa TUNAELEWANA. Ni rahisi mtu kukupa sifa tu, sijui una macho mazuri, kiuno kama dondora, usiku silali nakuota wewe, siwezi kuishi bila wewe, n.k ukajua umepata..Yes, atakuridhisha, lakini je anafaa kuwa mume kwako...
 

Yaani hapa umemaliza kabisa! mods tafadhali kitufe cha thanks kirudishwe
 
Yaani hapa umemaliza kabisa! mods tafadhali kitufe cha thanks kirudishwe


Umeona eeh hayo mapoint ya MPENDWA siyo ya kupewa like,
Bora hata ningekuwa naruhusiwa kusema I LOVE IT ....lol,


Tangu nijiunge JF sijawahi kujutia kwann nimeingia,
ksb kila sekunde niyoipata kuwa JF najifunza kitu kipya...
I REAL LOVE JF + ALL JF MEMBERS.
 
Mpendwa we jinsia gani? Kama unatekeleza uliyoandika she/he very lucky indeed


 
MPENDWA...Ndoa sio ya mtu mmoja hivyo haiwezi kuangushwa au kujengwa na mmoja tu.Kama mmoja anajenga na mwenzake anabomoa hawatafika popote...kinachohitajika ni kusaidiana, hapo tu ndio ndoa itafanikiwa!
nazani hii ndio pointi anayoimiss mpendwa, haiwezekani mimi huku home navumilia kunyimwa unyumba halaf mama chanja yeye anaonekana billicanus anaomba vocha kwa DJ. Huu ni u b w e g e sasa si uvumilivu.
 

Hapa umewaonea wakina mama .Mara nyingi wenye kuhama vitanda ni wababa hasa wakishakolea kwa nyumba ndogo,ataanzisha visa visivyokwisha.Wababa ndio wa kulaumiwa kwa kweli.
 
Hivi kuna mtu alishawahi kujiuliza kuwa ni nini atakuwa amemtendea mwenzako, hadi mwenzake huyo aamue kumuacha? Hapa namaanisha kuwa baada ya kuishi nae, je umeshamsoma kuwa ni kwa sababu gani ambazo mwenzio anaweza kukuacha?
 
Dada nimekukubali, kama umeolewa nadhani ndoa yako ni bomba sana na kama hujaolewa heri yake mmeo mtarajiwa. Shida kubwa wanawake wanataka kupambana na wanaume.
 
Mpendwa we jinsia gani? Kama unatekeleza uliyoandika she/he very lucky indeed


Yawezekana she/he lucky,
lakin nijuavyo mimi ,
SIYO KILA MHUBIRI MZURI (na hasa wengi wa siku hizi) NDIYO MTENDA MEMA.
PIA SIYO KILA MWANASAIKOLOJIA MZURI SANA WA MAPENZI BASI NA YEYE ANA MAPENZI MAZURI KWA MPENZI WAKE.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…