sirluta
JF-Expert Member
- Nov 28, 2012
- 6,325
- 2,491
Habari wanajamii,
Ni muda mrefu sijaingia humu sababu ya pilikapilika zilizokuwepo pamoja na kuwepo kwa magroup ya whatsupp kumepunguza concentration ya kuchangia mada humu.
Naomba tupeane mbinu za kuishi na mwanamke mgomvi kwenye ndoa ambae kila wakati anakuwa mtu wa ku complain kwamba ananyanyaswa ila ukamwambia akueleze unamnyanyasa na kitu gani hana jibu, ukijaribu kuangalia ama kujiuliza unamnyanyasa na nini huoni.
Kuna wanawake ambao hawaridhiki hivyo kila unachomfanyia anaona humtoshelezi. Akitaka kila siku wiki nzima mle nyama mtakula ila bado atalalamika sili vizuri.
Kama una tv ndani, labda anataka yeye aangalie chanel zake tu kwakuwa labda ana interest na movies, atashinda asubuhi hadi jioni na tv, ila wewe ukitaka uangalie taarifa ya habari ya saa 2 usiku ya dakika 20, atasema huo ni udikteta na unambagua.
Hazipiti siku 2 bila kupigiana simu na mama yake, ila baba mkwe atakaa hata mwaka hajamjulia hali. Ukimwonya kitu anasema huo ni uonevu, sipendi kukoromewa nitaenda kwetu.
Mwanamke kama huyu ambaye hawazi positively hata siku moja bali kuwaza negatively kila wakati na anakuwa mpinzani kwa kila kitu katika ndoa ni njia gani nzuri ya kuishi nae maana wengine tuna mioyo ya ubushoke ila siyo kwa kupenda bali kutokana na heshima mtu unakuwa nayo sasa ukiwaza kuchukua maamuzi magumu, jamii itakuangalia tofauti.
Najua huku kuna washauri wazuri na waliobobea bila kuwasahau wafurahishaji, wapondaji na watukanaji.
Nawasilisha.