Muonee huruma mzee wako basi.
Sitakuja kusahau jamaa flani chuo kila mwaka alikuwa anamtandika mzee wake laki 4 ya project hewa, mzee akikazia jamaa anaenda kuwapa simu rafiku zake wajifanya ndio wanaomsimamia kijana kwenye projekt[emoji23][emoji23].
Ngoma ikafika kwa bro wake msomi aliekuwa anaambiwa na mzee amtumie dogo pesa, yani inakuwa pembe tatu muamala kukamilika, kwanza dogo anamwambia mzee shida, pili mzee anamwambia bro wake hio shida, tatu bro akiona shida ina ulazima ndio atatuma pesa.
Sasa jamaa akampiga kizinga mzee wake anataka laki 4 ya project, mzee akafikisha kwa bro wake, bro wake akacheka akamtupia waya dogo akamwambia ana rafiki yake ambae ni mwalim (lecturer) hapa chuoni yeye hana namba yake kwahio dogo aende kumuomba namba ili wabonge na bro kuhusi hizo project, jamaa ikabidi asingizie huyo lecturer hayupo na project imeahirishwa [emoji23][emoji23].
Dogo karudi likizo bro wake ndo anamwambia unachofanya huko chuoni hakuna nisichojua, ujipange sana.