Tupeane updates za Ajira za Polisi 2024

Hakuna mishahara hii polisi
Mishahara ya polisi unalipwa kwa aina mbili kwa cheo na elimu (nayo inatofautiana kulingana na kada;afya,Tehama na nyinginezo)
Mf. Form 4(Constable) analipwa wastani wa 460+
Form 6 (constable) analipwa mshahara sawa na koplo
Diploma (Constable) analipwa sawa na Sargent kwa kada nyinginezo na kwa kada ya afya analipwa sawa sm(RSM)
Degree (constable) analipwa sawa sm (RSM) kwa kada nyinginezo, Tehama analipwa sawa Assistant inspector, na kada ya afya analipwa sawa superintendent
Nawasilisha
 
CCP Ni Kambi Mama Kwa Mafunzo Ya Jeshi La Polisi Pamoja Na Kuwa Ina Kambi Nyingine Mbili Zilizopo Kilimanjaro Pia Zinazoitwa KAMBAPORI Na KILELEPORI. .. CCP Ni Kambi Kubwa Kwa KWELII, Majengo Ya KUTOSHA Na Wakufunzi Waliobobea Kwenye Mafunzo.

Sifa Za Kutoboa Ni NIDHAMU Cha Kwanza, UVUMILIVU Ndo Jambo Mama Maana Nidhamu Lazima Itakuja Maana Wote Ni Watafutaji Na Lengo Ni Kumaliza Kozi Kazi Za Watu Ziendelee.

Kama Kawaida Kila Siku Mtaamka Saa 8 Usiku Mabio Almost Kilomita 7 Kuzunguka Kambi Nzima... Hamtakimbia Jumapili Tu Pamoja Na Siku Za Sikukuu Tu.

Mbali Na Mafunzo AFYA Ndo MTAJI Wako Muhimu Ili Umalize Mafunzo, Tunza Afya Yako... Vaa Viatu Vizuri Vyenye Soli Kubwa Chini.

Acha Kujionesha Mbele Ya Maafande, Acha Sifa Za Kutaka Kuonesha UNAA Mbele Ya Wenzio Na Maafande.

Ushirikiano Na Wenzio/Viongozi Wa Platoon/Kombania Ndo Itakufanya Umalize Kozi.

Hudhuria Fatiki/Kazi Zote Zilizopangwa Acha Kudoji Vipindi Mbalimbali


Mbaya Zaidi Lugha Za Matusi, Kupigana Na Kuibiana Ni Jambo Ambalo Huwezi Kusamehewa Kamwe Ni Kufukuzwa.

Mapenzi Mwiko Kambini... Uvumilie

Mengi Zaidi Tutajuzana... Mwenye Swali Lolote Anakaribishwa Nitajitahidi Kujibu Kadiri Navyoona Inafaa Bila Kupotosha Jambo.


Asante.
 
Hii Mishahara Sio Sahihi... Makadirio Yapo Chini Sana Bado... Nitakuja Kuonesha Na Mishahara Yao Pamoja Na Michanganuo Ya Posho Pia Hapo Mbele Kidogo...
 
Simu pia
 
Vipi issue ya kupata kitengo mafunzoni hili lipoje mkuu
 
Vipi issue ya kupata kitengo mafunzoni hili lipoje mkuu
Vitengo Vipo Vingi Tu Ila Inategemea Na Depo... Mfano Kuna Baadhi Ya Depo Wanaruhusu Sana Vitengo Kutokana Na Uhitaji Ila Usitegemee Sana Vitengo Maana Baadae Mbeleni Itakuja Kuwasumbua Hasa Mwishoni Mwa Kozi Na Hata Mkifika Mikoani.

Maana Hautojua KWATA Sana Pamoja Na SILAHA Hautoifahamu Kwa Undani Zaidi

Mfano Madaktari, Manesi Na wenye Taaluma za Afya huwa Wanapelekwa Zahanati Kama Kitengo.

Pia kama kuna Ujenzi Baadhi Kujichagua/Kuteuliwa Kwenda Kitengo

USHAURI: Usitegemee Sana Vitengo Maana Sio Nzuri Na Itakufanya Kuonekana MZEMBE Sana Ukiwa Kwenye Majukumu Yako Hapo Mbeleni... Nenda Kafanye Mafunzo Sio KUANGUSHIA KOZI
 
Naam shukran mkuu
 
Noted ✍️
 
Ni kweli lakini kaka c unajua tena wengine tunaforce tuu sio kwamba hatupendi bali Kuna muda mwili unakusaliti
 
Vip kuhusu utaratibu wa kupata cheo, hua wanazingatia nini kwa askar mpya kupandishwa cheo ukiachana na icho cheo cha kwanza cha uconstable?
 
Kweli kabisa mkuuπŸ‘
 
Na
Na je vipi Kama ikatokea katikati ya corse ukaumwa may b ikakuhitaji ukae bila kufanya issues ngumu Kwa miezi miwili au mitatu apa unarudishwa nyumbani au watakuvumilia
 
Na

Na je vipi Kama ikatokea katikati ya corse ukaumwa may b ikakuhitaji ukae bila kufanya issues ngumu Kwa miezi miwili au mitatu apa unarudishwa nyumbani au watakuvumilia
Naskia ukienda uko ishu ya kuomba mungu ni kwamba usiumweumwe hovyo mzee ukiwa unaumwaumwa wanakwambia ww ni unfit then unarud nyumban na nafas yako chapu tu anapewa mtu mwingine πŸ€”
 
Vip kuhusu utaratibu wa kupata cheo, hua wanazingatia nini kwa askar mpya kupandishwa cheo ukiachana na icho cheo cha kwanza cha uconstable?
i.elimu
ii.nidhamu
iii.utendaji kazi nzuri
iv.weledi,fanya kazi kwa uadilifu ukiharibu kazi zao watakushitaki na mashitaka yatakuondoa kwenye sifa ya kupata cheo kwa miaka kadhaa.

C&P.
 

Km 14 kawaida watu watakimbia tu
Endeleeni kubishana watu walisha ripoti TPS kitambo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…