Tupeane updates za Ajira za Polisi 2024

Shukrani mkuu🤝🤝
 
Vp na je mkishafika ccp pale ni kwamba ndo mnaanza kozi au hua kuna kua na mwezi mmoja au miwili ya uzalendo kama jeshini?
 
Mbinu ni moja tu. KADI YA UVCCM.
Hii utaivaa shingoni kama ID uingiapo kwa interview. Hautoulizwa chochote utajitambulisha tu na utakua umemaliza kila kitu.
Mkuu hii mbinu inatumika Zanzibar, Zanzibar kuna siasa mbaya sana tusiruhu iingie Tanganyika itaumiza wasiokua na hatia.
 
Vp na je mkishafika ccp pale ni kwamba ndo mnaanza kozi au hua kuna kua na mwezi mmoja au miwili ya uzalendo kama jeshini?
Kuwepo CCP tayari kozi imeshaanza tayari... Ila kuna siku maalum ambapo kozi hufunguliwa, Mfano depo iliyopita kozi ilifunguliwa miezi 2 toka watu walivyoripoti kambini.
 
Mkuu hii mbinu inatumika Zanzibar, Zanzibar kuna siasa mbaya sana tusiruhu iingie Tanganyika itaumiza wasiokua na hatia.
Kwa Zanzibar uhakika, hata baadhi ya watu toka kule waliotaka kujiunga Jeshi kule walishanigusia hili....
 
Maelezo Muhimu sana mkuu, ila siku hizi ukishaingia CCP Kutoka Jumapili kwenda kutembea hizo issue hamna tena...

Labda issue muhimu za rufaa za hospital, msiba nyumbani, Lindo la nje, otherwise NO RUHUSA Ya Kutoka Nje.

Kufukuzwa kupo sana wakuu, kuna Mwamba wa PCCB alifukuzwa kambini siku 3 kabla ya kuhitimu Depo iliyopita.
 
Shukrani sana mkuu🤝🤝
 
Alaf pia naomba kuuliza kwann kuanzia cheo cha staff sergent na kuendelea juu wao wakivaa uniform yao ile ya kaki wanavaa kama kaunda suti flani hivi hawachomekei alaf hawa wa cheo cha sergent kushuka chini mpaka police constable(cheo kdgo cha kwanza) wao wanachomekea mda wote…ni kwann eti wakuu?? mwanadodoma Mercenary2013
 
Na pia naomba kujua utaratibu wa kuvaa zile uniform kati ya ile ya kaki na ile ya green jungle ni unajiamulia tu kua leo nivae hii alafu kesho nivae ile au kuna utaratibu wa siku maalumu wa kuvaa kila uniform?? mwanadodoma Mercenary2013
 
Nadhani ni utaratibu wa mavazi tu,lakini
Ok ndugu,Depo yangu ile miezi miwili ya mwisho tulikuwa tunaruhusiwa Jumapili asubuhi mpaka saa 10 jioni kwenda kusafisha macho Mjini,kuhusu uliyeuliza suala la mavazi nadhani ni utaratibu wa mavazi tu. Ndio maana zamani kuanzia Nyota Moja mpaka IGP walikuwa wanavaa mikanda fulani myeusi tumboni na mmoja unapita begani,siku hizi naona hawavai hivyo
 
Pia naomba kujua utaratibu wa kupewa uniform hua mtu unapewa uniform pair ngap? Na je hua kuna utaratibu wa kupewa uniform mpya kila baada ya miaka kadhaa au ukitoka mafunzoni uniform utakazopewa ndo izoizo hupewi tena nyingine?? Maana hua unakuta askari wengne uniform zao zimechakaa kwelikweli mpka hua nakua sielew
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…