Hawakunimind maana niliandika Notice ya kuacha kazi ndani ya masaa 24 nikarudisha Mshahara wao wa mwezi mmoja na Uniform zao nikasepa. Mtiti ulikuwa kupata ruhusa kwenda Chuo maana wakubwa wote Makao Makuu walikataa kusaini Fomu yangu maana walikuwa wanasema inakuaje Konstebo sijamaliza hata miaka miwili kazini nipewe ruhusa kwenda kusoma Degree😄Nilipambana kwelikweli nikagonga mwamba.Siku ya mwisho(kumbuka Chuo kimefungua Septemba)na hiyo ni Novemba mimi sijapata ruhusa. Kila nikienda kwa Makamishna pale Makao Makuu wananipiga mikwala na kunifokea kunikimbiza. Siku ya mwisho nikasema liwalo na liwe naenda kumuona Mzee wa Ngunguli IGP Mahita liwalo na liwe. Nikaibuka pale HQ saa 12 asubuhi,IGP alipoingia tu Msafara wake nikusubiri kaingia ofisini kwake mimi nikaenda kumuona Aide wake(Msaidizi wake)alikuwa anaitwa Diwani Athuman(ambaye baadaye alikuja kuwa Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU na kisha Mkurugenzi Mkuu wa Usalama wa Taifa)akaondolewa na Mama Samia mwaka jana nadhani,nikamueleza suala langu(kipindi hiko akiwa Msaidizi wa IGP alikuwa na Nyota Tatu au ASP).Huwa namshukuru mpaka leo,maana alichukua Barua yangu ya kuitwa Chuo,akanishika mkono akaniingiza Ofisini kwa IGP(kumbuka Konstebo kama mimi kuingia ofisini kwa IGP tena Mahita uoga nilikuwa nao si wa kitoto).Akamueleza IGP suala langu na jinsi Makamishna wanavyozingua kunipa ruhusa.Mwamba IGP alimpiga simu moja tu kwa Kamishna gani sijui yule alikuja na Faili langu kalishika mkononi.Akamwambia nataka huyu Askari apate ruhusa yake ndani ya dakika 3 aondoke kwenda Chuo😄sikuamini masikio yangu.Huwa namshukuru sana Afande Mahita na Diwani mpaka leo kwa msaada ule