Tupeane updates za Ajira za Polisi 2024

Shukrani mkuu🤝
 
Ukishakuwa Mkoa ulikopangiwa ni ujanja wako kupata Uniform mpya maana ni deal sana.Hivyo unatakiwa ujiongeze na watu wa Bohari unawatoa kitu kidogo wakupe Unifomu. Mnapomaliza Depo mnapewa Uniform za kuripoti nazo mikoani,sasa zikichakaa inabidi ujiongeze kupata mpya
 
Sawa sawa Mkuu
 
Na pia naomba kujua utaratibu wa kuvaa zile uniform kati ya ile ya kaki na ile ya green jungle ni unajiamulia tu kua leo nivae hii alafu kesho nivae ile au kuna utaratibu wa siku maalumu wa kuvaa kila uniform?? mwanadodoma Mercenary2013
Jungle green inavaliwa kama kuna operesheni muhimu mfano kipindi mchakamchaka, mazoezi ya Utayari lakini pia kuna kuwepo na siku maalum kutokana na ratiba itakavyoamuliwa ila muda mwingi sana Askari anapaswa kuvaa kaki wakati wa kazi.
 
Shukran maelezo yameshiba🤝🤝
 
Jungle green inavaliwa kama kuna operesheni muhimu mfano kipindi mchakamchaka, mazoezi ya Utayari lakini pia kuna kuwepo na siku maalum kutokana na ratiba itakavyoamuliwa ila muda mwingi sana Askari anapaswa kuvaa kaki wakati wa kazi.
Asante sana mkuu🤝
 
Sorry uliacha kazi mwaka gani na kwann uliacha kazi mkuu??
 
Alaf pia naomba kujua ukishatoka mafunzoni ni wote mnapangiwa mikoani au inakuaje na je kukaa kota unatakiwa ukae mda gani ndo utoke kota au hata ukitaka kukaa mda wote wa miaka yote ya kazi imawezekana?
 
Kuna maswali inabidi msubiri pdf ikitoka ndio muanze kuulizana huko pm, watu tumesubscribe kwenye uzi kusubiri pdf na lonja za muhimu, wengine mnaulizia utaratibu wa kupata uniform ya pili 😝😝 mkipata kazi si mtaambiwa vyote ?
 
Alaf pia naomba kujua nmepitia matangazo yao wanayotoa ya kuita watu chuoni naona hua wanasema twende na 54000 ya bima na pesa ya kujikimu…sasa naomba kuuliza hii pesa yakujikimu ya nn tena kwani posho hawatoi uko ccp au?
 
Kuna maswali inabidi msubiri pdf ikitoka ndio muanze kuulizana huko pm, watu tumesubscribe kwenye uzi kusubiri pdf na lonja za muhimu, wengine mnaulizia utaratibu wa kupata uniform ya pili 😝😝 mkipata kazi si mtaambiwa vyote ?
Mda haumsubir mtu, hawa watu wanajua mambo wapo hewani sasahiv ndo mda wa kuwauliza ukisema usubirie pdf ndo uulize wasipokuepo je…ni vzr kuchangamkia fursa
 
Shukran mkuu…ila kuna kitu umenichanganya aisee umesema umejiendeleza kielimu alaf ukapiga pepa ya form6 mwaka 2021 na kujiunga udsm kwa degree yakwanza that means ww ndo umemaliza chuo mwaka huu au inakuaje maana mm sijaelewa au mm ndo nmekuelewa vibaya?🤔
 
Typing Error sorry,niliingia Depo Juni 1998 na kumaliza February 1999. Nikaendelea na Judo Course mpaka December 1999 nilipomaliza na kupangiwa Mkoa wa kazi. Nikiwa kazini June 2000 nikaanza QT kisha Mei 2001 nikapiga Paper ya Six kama Private Candidate. Kisha 2002 nikapata ruhusa na kuingia UDSM Degree nikamaliza 2006. Mwaka huohuo 2006 baada ya ku-graduate nikaacha kazi
 
Anhaa apo nmekupata mkuu
 
Aisee ww ulikua ni mafya 🤣🤣…..yani umemaliza tu kusoma halafu ukawaambia kua hutaki kazi yao ya polisi aisee hawakukumaind kweli😂😂
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…