Niliingia Polisi Depo ya June 1998 nikiwa na Elimu ya Kidato cha Nne niliyomaliza 1997.Nikiwa kazini nilijiendeleza na QT mwaka mmoja nikapiga Paper ya Form Six 2021 nikafaulu,nikachaguliwa Degree ya Kwanza UDSM.Nilipomaliza Degree tu. nikaripoti kazini nikafanya mwezi mmoja nikapata kazi UN kwa field niliyosomea Chuo na Mshahara ulikuwa mara 30 ya Mshahara wangu wa Polisi hivyo nikaacha kazi nikaenda zangu UN.
Mkimaliza Depo mnatawanywa mikoani kuripoti kwa ma-RPC,kisha mkiripoti kwa ma-RPC nao wanawapangia kwenye Wilaya za Mikoa yao kutegemea na mahitaji.
Kuhusu kukaa Kota inategemea kama zipo maana nazo kuzipata huwa ni deal.Hivyo wengi wakiripoti Mikoani huwa wanapangiwa kukaa kwenye mamesi kwa muda au kama una ndugu mkoa uliopangiwa unaweza kukaa kwa Ndugu,kisha ukilipwa Mshahara kama ulikuwa unakaa kwenye mesi ya Polisi unajiongeza kutafuta chumba mtaani maana kupata Kota ni mtiti huwa zinakuwa zimejaa,labda umuone Mkuu wa Kambi ucheze kama pale akusaidie