Tupeane Uzoefu: Biashara gani ilikushinda?

Biashara ya chips, hii nilikosa mtu sahihi na pia usimamizi wangu ulikua mdogo sana
Kazi yangu inanibana mno kiasi kwamba sipati muda wa kufanya mengine
 
Huwa unawapa Bodaboda iwe yao baada ya mwaka?? Au mkataba gani mkuu
Ndiyo mkuu, akimaliza mkataba chombo inakuwa yake na walio wengi huchemka Mf. Anaweza akapiga mkataba miezi 5 afu akashindwa anarudisha chombo kwa bosi kwaiyo akirudisha chombo we ndo unazidi kunufaika na akimaliza mkataba bado unanufaika vile vile.
 
Hii nzuri sana.
 
Hahahahaa daah kilimo cha vitunguu Dakawa...
Sikupata hata cha mboga
Duu kweli biashara full changamoto, mimi kila nikipita maeneo hayo uona kama ni maeneo yenye kufaa sana kilimo cha vitunguu na nyanya
 
Mimi taksi. Madereva walikuwa pasua kichwa ati. Niliifunga.
Kipindi niko first year chuo nlinunua bodaboda mbili aisee io changamoto yake usipime stres tupu madereva pasua kinoma nikapiga chini nikaziuza zote aisee
 
Biashara ya taksi, pasua kichwa kweli kweli, kila ukiona simu ya dereva hata kama uko sehemu ya starehe, gambe inayeyuka yote kichwani
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji119][emoji119][emoji119]Biahara za vyombo vya moto majanga aisee...
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji119][emoji119][emoji119]Biahara za vyombo vya moto majanga aisee...
Kweli kabisa, yaani ukiweka gari ya biashara barabarani, hesabu hiyo gari siyo yako changamoto zake nyingi sana.
 
Duu kweli biashara full changamoto, mimi kila nikipita maeneo hayo uona kama ni maeneo yenye kufaa sana kilimo cha vitunguu na nyanya

Inasemekana pale hapafai kwa vitunguu
Ila panafaa kwa mbogamboga nyingine
 
Mchele wa kamsamba upo. Unahitaji kiasi gani...?

Nataka niuone kwanza nijiridhishe,
Then nitakuwa nanunua kwa interval fulani kuna mahali napeleka ila uwe wenyewe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…