Tupeane Uzoefu: Biashara gani ilikushinda?

Tupeane Uzoefu: Biashara gani ilikushinda?

Lima kilimo cha kisasa mkuu
Ni cha kisasa mkuu lakini gharama zake ni kubwa mno kiasi kwamba ukija kukaa chini ukipiga hesabu na muda wako uliopoteza unakuta hujaingiza kitu na wakulima wengi huwa hawapigi hizo hesabu wanaangalia kavunaje basi,labda shamba liwe lako ndio utaona faida lisiwe na kukodi kabisa
 
kuna sehemu ulikosea mkuu
 
Bishara ya kuza dawa za chooni aiseee nilikutana na changamoto Sana ila hili la mteja mmoja kunikabidhi dekio chafu ni lisugue kwa dawa likitakata ndo anunue sikulivumilia na kupiga chini hiyo biashara
duuh kuna watu jeuri[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Niliwahi shiriki kilimo cha mpunga cha kutegemea mvua. Niliishia kuvuna fedheha. Nililima misimu miwili. Imagine kwenye plot ambayo the precious year imetoa gunia 25 we unavuna gunia 5. Msimu ujao nasubiri mavuno kisha ninunue zangu mzigo niweke stoo niuuze soko likikaa vizuri.

Nina shida na ule mchele ulionyooka kama wa Kamsamba
Naweza kupata?
 
Na changamoto kubwa katika kilimo ni usimamizi mzuri. Unakuta mtu yuko Dar ila anajiita mkulima kwa kuwa na shamba la mpunga huko Kyela. Kila siku unapigiwa simu mara mbolea inahitajika, mara dawa unatuma hela, mtu anaenda kupiga picha shamba la jirani kisha anakutumia. Basi unajua mavuno yatakuwa ni mazuri. Ukifika msimu wa mavuno jiandae kupokea Breaking News.
Breaking News[emoji23][emoji23][emoji23]
 
vinyago nilikuwa napeleka marekani,hasara tupu serikali wanachukua kodi mpaka mtaji unaisha,nikaamua niingie kwenye ngada saizi mimi ni multi billionaire

Once a baharia always a baharia
afu huyu jamaa hatanii maana hata jina lake tu "PABLO" kwa wanaomjua jamaa alikuaga mbrazili/coliumbia kama sijakosea ndo alikuwa nguli wa kupush ngada
 
Back
Top Bottom