Tupeane Uzoefu: Biashara gani ilikushinda?

Tupeane Uzoefu: Biashara gani ilikushinda?

Daud1990,
Ndugu unachanganya madawa. Biashara na kamari ni vitu viwili tofauti. Kwa kuwa kwenye biashara kuna kufeli basi hilo halifanyi iwe kama kamari!
 
Achaaa mkuu yani nilipata hasara na duka nikafungaa mwaka 2015.

Kuna mda samaki zinakuja zimeharibika

Kifupi biashara yoyote inataka moyoo
Hii bisahra ukiwa na lori lenye freezer inaweza kuwa nzuri sana.
 
Na changamoto kubwa katika kilimo ni usimamizi mzuri. Unakuta mtu yuko Dar ila anajiita mkulima kwa kuwa na shamba la mpunga huko Kyela. Kila siku unapigiwa simu mara mbolea inahitajika, mara dawa unatuma hela, mtu anaenda kupiga picha shamba la jirani kisha anakutumia. Basi unajua mavuno yatakuwa ni mazuri. Ukifika msimu wa mavuno jiandae kupokea Breaking News.
Hii kitu ni kwel na biashara nyingi na kilimo hufeli hapa kwenye usimamizi , siku zote pesa hazina uaminifu hata kidogo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
MIGUGO,
Hii ni hatari sana. Kipindi cha nyuma kuna jamaa alikuwa na ki-pub chake Kariakoo kinalika sana. Alikuwa na vi-bar maid vizuri mno na alikuwa lazima avilambe. Haikuchukuwa muda akaugua ukimwi na sasa ni marehemu.

Siyo kama namlaumu kwani wanaume wengi wangeweza kuingia kwenye huo mtego kwani kipindi hicho ukimwi ulikuwa haujajulika sana na watu walikuwa hawatumii Condomu.
 
Umewezaje??hasahasa ufugaji wa kuku wa nyama umeniliza sana mpk vidonda vya tumbo

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] Ila Wengine wanatajirikia huko


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Sio biashara hiyo, ila ni ile uonekane tu una biashara!! Pikipiki mpya kwa sasa hadi 2.5 milioni, unampa mtu kwa mkataba wa mwaka ambapo kila siku atakuletea 10,000,kwa mwezi ni 300,000 kwa mwaka ni3. 6 milioni, faida hapo ni kama 1.1 milioni, na sio rahisi kuipata pesa yotekwa mwezibila longo longo, ukitafuta faida halisi hapo kwa mwezi ni kama 100,000/!!!!!!bado wasiwasi wa kuibiwa.
Umenena vyema mkuu,
 
Niliwahi fanya kilimo cha nyanya 2 years back asee sitasahu

kipindi naanza bei ya kuuza kwa tenga ilikua 40K nikasema pesa si ndio hii nimeingia kichwa kichwa nikalaza 1.2 shambani heka moja .

Nyanya zimeanza kutoka maji yakawa ya shida kumwagilia zikadumaa zikaishia kukuua vidogo vidogo vinaiva nikakomaa nikamwaga mbolea wakaingia panya wakala kma robo heka nyanya zote zilizokua zimeanza kua nyekundu

Nikapiga dawa huku na kule ugonjwa mwingine asee nilikuaga naishi km kichaa

Mwisho wa siku nilivuna tenga 9 out of 120 na bei ya kuuzia ikashuka hadi elfu 8 na kwakua nyanya zangu zilitoka ndogo ndogo sana na nyingi zina maginjwa nikauza tenga kwa elfu tano Kati ya 1.2M , muda na nguvu nilizotumia niliambulia elfu 45 tu 🥶


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Wakuu, Kuna shida sehemu. Ukichunguza post za wengi hapo juu utagundua wengi waliingia na kuanza project zao kwa bidii lakini wakiwa hawana uzoefu na shughuli husika. Yaani si shughuli ambazo wamekuwa wakizifanya kwa miaka mitatu au zaidi.

Kwa nini wakinga huwa hawafeli Mara kwa Mara? Ni kwa sababu wana tabia ya kufndishana kazi kabla ya kupeana mtaji. Hata project iwe nzuri vipi bila ujuzi (sio elimu) kufaulu si rahisi.
 
Utawala wa biashara ni kitu muhimu sana, anayetawala biashara anaweza kuona kupanda na kushuka kwa biashara. Stratergy ya biashara yako ni ipi ili ufikie malengo yako, vitu gani vinajenga hiyo strartergy yako ili ifikie malengo. Baada ya hapo ni tabia gani huyo anayesimamia biashara awe nayo, tabia sahihi ya msimamizi wa biashara ni sehemu ya mafanikio bila hiyo tabia inayotakiwa biashara imekufa kabla ya kuanza.
 
Wewe mimi kabisa hii biashara niliitamani nimenunua boda nikampa dereva mwanzoni hela ya hesabu wanaleta vizuri kati wanabadilika mpaka hela ya hesabu ikifika mimi ndio nimtafute na kumfata kwake.

Jamani hii biashara ina presha mwisho wa siku nikaiuza na boda yenyewe sitaki hata kuisikia mtu aniambie mambo ya kufanya biashara ya boda.
Acha tuu..mwanzoni ukiwakabidhi chombo wanakua wazuri,,katkkati apoo uwiiii wanakua pasua kichwa ndugu yng..nlikua nazo tatu nimewanyanganya zote nimeuza mbili moja nimebaki nayo mm ..hiii biashara hapana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom