Tupeane Uzoefu: Biashara gani ilikushinda?

Tupeane Uzoefu: Biashara gani ilikushinda?

Mpesa na Tigo pesa changamoto ni Chuma ulete tu na MTU atakaye kaa hapo shop amua ukae mwenywe au umuweke mkeo tu
Ukiweka kijana utalia tu

Kuhusu Chuma ulete pesa zako usizichanganye na pesa za Wateja hata cku moja

Sent using Jamii Forums mobile app
Imani ya kijinga kabisa hii ya chuma ulete. Na mtu unayemini kwenye jambo kama hili ukifeli kwenye biashara utalaumu? Hupaswi kulaumu. Inaonyesha kabisa huna abc za biashara.
 
[QUOTE="kapunika,
Umesema kweli tupu. Halafu kuna kitu kingine watu wanaona ni kidogo kumbe kinachangia sana: kuamini ushirikina. Kuna mdau anajiita mtena amesema kuwa sababu ya kunaguka kwenye biashara za Mpesa etc ni pamoja na ''chuma ulete''! Hili ni tatizo kubwa kwa wafanya biashara wengi.

Mtu anaanzisha biashara anaacha kuwekeza nguvu kwenye kanuni za biashara na badala yake anafanya ushirikina uwe ndiyo mwongozo wake! Mtu wa aina hii ataacha kufeli? Unakuta wengine kwa mfano anafungua Bar, badala ya kuboresha huduma na kufanya ubunifu zaidi ya wengine yeye anakimbilia kuzika kondoo au wanyama wengine kwenye eneo la biashara.

Matokeo ni kuwa anakuwa amejiridhisha kuwa sasa atapata wateja na mambo kama huduma nzuri anayasahau.
 
Wakuu, ni mambo ya kushangaza lakini yako sana na tunayafanya karibu Mara zote. Fikiria lifuatalo: ikiwa mtu usiyemfahamu angekuja na kuazima laki moja kwa makubaliano afanyie biashara na kila siku arejeshe 1000 kama RIBA ya kukaa na pesa yako huenda tusingemkubalia kwa kuwa hatumfahamu. kwa upande mwingine, unachukua bajaji yako ya milioni saba au zaidi au pikipiki ya milioni mbili na kumkabidhi mtu mwingine ambaye humfahamu ukiamini atafanyia kazi na kukupa riba na kutunza mtaji ( chombo)

- hujui ana malengo gani kimaisha, ana uchungu kiasi gani wa kutaka kuboresha hali zake kiuchumi na kijamii.

- hujui anashughulikaje na Mali zake binafsi na hivyo atashughulikaje na milioni zako (chombo)

- hujui anaonaje suala zima la wewe kumkabidhi milioni zako kuwa ni fursa ya ninyi wawili kukua pamoja na kufanya mambo makubwa pamoja baadae au anatafuta kamtaji ka kibanda cha chipsi halafu muachane.

Mengi yanahusika wakuu juu ya aina ya watu tunaoamua kufanya nao biashara au kuendesha miradi yetu iwe ni maduka, vijana wa kulisha mifugo, Bodaboda nk. Lazima tuwafahamu na watufahamu, wajue tunatazamia nini toka kwao na kwa nini wao na si wengine waliokabidhiwa hizo milioni. Sisi pia hatupaswi kupoteza mtazamo kuwa zile ni milioni za pesa na sio pikipiki tu.
 
macho_mdiliko,
Mkuu Macho wanasahau hesabu za msingi kabisa tunazojifunza kabla hatujaanza shule kuwa 1+1=2 na 2-1=1.

Kuorodhesha kinachoingia na kutoka ndio msingi wa kuondoa imani ya chuma ulete, lakini muhimu zaidi ni kupanga nini kinatoka lini na kinaenda wapi, kufanya nini. Ikiwa chuma ulete atachukua kiasi Fulani basi tujue pia kiasi hiki kilichukuliwa na chuma ulete na tuorodheshe hivyo kwenye daftari.
 
Biashara za mtandaoni zimekuwa za pasua kichwa nakumbuka enzi za four corner alliance group, forever living, mara fahari ivestments, mara global alliance,Mara cjui na zingine mnazijua hizi hazijawahi kumuacha mtu salama walikwisha jaribu kufanya kwa miaka ya karibun hapa!!!
Kuna moja imeingia mjini sasa inaitwa LongRich. Naona watu wameichangamkia. Kuna watu wanapiga nazo hatua, nadhani ni malengo tu...
 
Niliwahi fanya kilimo cha nyanya 2 years back asee sitasahu

kipindi naanza bei ya kuuza kwa tenga ilikua 40K nikasema pesa si ndio hii nimeingia kichwa kichwa nikalaza 1.2 shambani heka moja .

Nyanya zimeanza kutoka maji yakawa ya shida kumwagilia zikadumaa zikaishia kukuua vidogo vidogo vinaiva nikakomaa nikamwaga mbolea wakaingia panya wakala kma robo heka nyanya zote zilizokua zimeanza kua nyekundu

Nikapiga dawa huku na kule ugonjwa mwingine asee nilikuaga naishi km kichaa

Mwisho wa siku nilivuna tenga 9 out of 120 na bei ya kuuzia ikashuka hadi elfu 8 na kwakua nyanya zangu zilitoka ndogo ndogo sana na nyingi zina maginjwa nikauza tenga kwa elfu tano Kati ya 1.2M , muda na nguvu nilizotumia niliambulia elfu 45 tu 🥶


Sent from my iPhone using JamiiForums
Pole sana mimi kuna. Biashara niliwekeza last year Ilikuwa ya mtaji wa sh. Milioni mbili kasoro, Yan hapa nilipo najuta Kwanini nilifanya hivo, nimebaki na almost zero.
Roho inaniuma sana
 
Daaaa!! Kamsamba, umenikumbusha mbali sana, mwaka jana nilikuwa huko, ila daa kutoka hapo mlowo kuitafuta Kamsamba ni shughuri pevu, hizo km 132!! Sio mchezo na kuna poli zito kuna sehemu inaitwa) BOT), kuna kona kali majambazi ndio huwasubilia wafanyabishara na kuwapola pesa!

kiukweli kule kuna mchele mzuri ila kuna sehemu inaitwa MAJIMOTO, ipo mkoa wa katavi(mlele) kule ndio balaa, ni sindano mchele wa kule, na unaweza tokea hapo hapo Kamsamba hadi kule. Nilikuwa kwenye utafiti wa biashara hiyo hiyo ya mchele.
Duh maji moto ni mbali sana mkuu, nilishawahi fika hadi hapo kwenye hiyo Chem chem inayotoa maji ya moto, labda huo mchele uuzie mikoa ya karibu na sio kuleta Dar maana ni hasara
 
Walioingia kingi wengi ni watu wa Dar huko,
Shida watu wanapenda slope miaka hii
Forex Kama ilivyo biashara zingine Kuna matapeli ndani Yake... Hata biashara ya madini ukiingia kichwa kichwa unakutana na matapeli wanakuuzia chupa ukidhani ni dhahabu...

Cha kukutoa usiingizwe kwenye radar za matapeli ni Jitahidi kutafuta maarifa sahihi kutoka kwa watu sahihi... Tatizo Ni kwamba watu wanatafuta taarifa kutoka kwa watu wale wale matapeli.

Yani ni sawa na kwenda kuuliza kwa mwamposa kuwa kukanyaga mafuta ni nguvu za Giza au sio za giza. Watu wamelizwa saaana kwa hali Kama hii.


Mwisho wa siku kila biashara ina hasara na faida .. Leo humu tunaona shuhuda mpaka za Bodaboda Zina hasara.. Cha msingi ni kufanya biashara bila kuwa na ushawishi wa mtu. Fanya biashara kwa moyo wako kupenda hii itakusaidia kuwa na nguvu ya kupambana na hali zote ( faida au hasara)....

Kufanya biashara yoyote kwa msukumo wa rafiki, ndugu au kusikia hautaweza kuhimili mitikisiko ya hasara. Hata forex wengi wanateswa hapo.



All in all , utafutaji wa pesa haujawah kuwa mwepesi. Tufanye kazi kwa bidii na kumuomba mungu atupe nguvu za kuhimili hali ngumu tunazopitia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Niliwekeza hela nyingi kwenye bando nikakuza account instagram aaah nilipiga hela za matangazo kama kichaa yani kwa mwezi laki mbili kitu kidogo sana nikajikusanya nikanunua cm ya maana mfukoni nikabaki cna kitu hacker akafanya yake mbaka leo roho inauma sanaa🤦🏽‍♂️🤦🏽‍♂️

Lkn nimeanza na account mpya mambo co mabaya nasogea


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Daud1990, 2016 nilikuwa victim wa kupagawa na screen shot za profit za watu ila nikaja kungundua kuwa sio wote ni forex trader.

Nikaja nikaanza kununua signal bado ikawa ni janga.

Nimechoma account sana ila msingi usikate tamaa.

Nashukuru forex kwa sasa.

Kwa sasa nikikutana na mtu anae trade tukipiga story huwa ananiheshimu maana ni tofauti.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Duh maji moto ni mbali sana mkuu, nilishawahi fika hadi hapo kwenye hiyo Chem chem inayotoa maji ya moto, labda huo mchele uuzie mikoa ya karibu na sio kuleta Dar maana ni hasara
Inategemea, na hali ya soko, mbona watu wengi sana, wanaufuata huko, kwani kama mchele unatoka mpanda, na ki gharama za usafiri ni sawa tu!! Ki ukweli kule bei huwa sio juu sana, kutokana na ushindani kuwa mdogo wa wateja, mfano kilo moja hadi dar ni kama shilingi 100(usafiri)
 
Back
Top Bottom