Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hahaha kuna cousin wangu aliwekeza kwenye kilimo cha nyanya,alikopa km laki 7 na 80
Ilikuwa wakivuna tenga litauzwa kwa 4,500.
Daah kutahamaki wkt wa mavuno biashara ikuwa hovyo,nyanya kila mahara tenga mia 7
Alijuta na pesa ilikuwa ya mkopo.
Na hela za bandia usisahau[emoji31]Mpesa na Tigo pesa changamoto ni Chuma ulete tu na MTU atakaye kaa hapo shop amua ukae mwenywe au umuweke mkeo tu
Ukiweka kijana utalia tu
Kuhusu Chuma ulete pesa zako usizichanganye na pesa za Wateja hata cku moja
Sent using Jamii Forums mobile app
Changamoto zake ni zipi mkuu.salon ya kiume sitakuja kuifanya hii biashara
vinyozi siyo waaminifu,biashara siyo nzuri.ukimpata mtu wa kuwasimamia vinyozi watamlaghai hadi abadilike awe pamoja nao wakuibie
Biashara yoyote inahitaji usimamizi wa 100% ukiwa hapo hapo.
Nakumbuka nilikuwa na Pub mkoa flani ilinifilisi ili niimaintain iendelee kuwepo.Vibaa med nilivitoa straight from unyaturuni.Lazima niwalambe kwanza.Vitoto "Onion a**" havikatai kwa mi boss wao.Wife aliipiga vita nilivyohamishwa kikazi akafurahi na ikafa.
Na changamoto kubwa katika kilimo ni usimamizi mzuri. Unakuta mtu yuko Dar ila anajiita mkulima kwa kuwa na shamba la mpunga huko Kyela. Kila siku unapigiwa simu mara mbolea inahitajika, mara dawa unatuma hela, mtu anaenda kupiga picha shamba la jirani kisha anakutumia. Basi unajua mavuno yatakuwa ni mazuri. Ukifika msimu wa mavuno jiandae kupokea Breaking News.
Nipe mbinu basi ya kupata matangazo.nina acount ipo vizuri ila sijajua jinsi ya kupata matangazo.Niliwekeza hela nyingi kwenye bando nikakuza account instagram aaah nilipiga hela za matangazo kama kichaa yani kwa mwezi laki mbili kitu kidogo sana nikajikusanya nikanunua cm ya maana mfukoni nikabaki cna kitu hacker akafanya yake mbaka leo roho inauma sanaa🤦🏽♂️🤦🏽♂️
Lkn nimeanza na account mpya mambo co mabaya nasogea
Sent using Jamii Forums mobile app
Imani ya kijinga kabisa hii ya chuma ulete. Na mtu unayemini kwenye jambo kama hili ukifeli kwenye biashara utalaumu? Hupaswi kulaumu. Inaonyesha kabisa huna abc za biashara.
ila hii ni kweli 100%Asante sana mkuu kulisemea hili..mm nikifeli huwa simlaumu mtu..kaa chini jitafari wapi ulifanya kosa.be honest yourself...! Usipeleke lawama.za machuma ulete...mie siamini..!
kuna kaka ana duka kubwa sana la nguo..siki hyo tuko naye kkoo anahesabu kila laki haipo 10000! Akapanic..akasema chuma ulete...mm nikampa ukweli...nikamwqmbia simjui mkeo hanijui..anayekupga hizo pesa ni mkeo...naongea kutokana na mm ni ke! Alibisha balaa nikamwambia usimwambie mkeo..mtegeshee hela km hatadokoa...ananiulizaga had leo ww maathai ulijuaje? Nikamwambia i knw..mbaya wako alwys huw yuko karibu sana na ww! Hakuna chuma ulete wala nm!ukiweka imani za ushirikina kwa biashara jua utasindikiza wenzako tu...huna hesabu za biashara jua kufel nje nje
Jaribu kulima karangaKama mimi nimepoteza muda sana kwenye mpunga mpaka sioni pakwenda mtaji wote umekata sijui hata nianzie wapi ila kilimo ni zaidi ya noma labda kilimo cha matunda/miti kinaweza kua ahueni.
[emoji23][emoji23]salon ya kiume sitakuja kuifanya hii biashara
ahhahhahahaahNiliwahi fanya kilimo cha nyanya 2 years back asee sitasahu
kipindi naanza bei ya kuuza kwa tenga ilikua 40K nikasema pesa si ndio hii nimeingia kichwa kichwa nikalaza 1.2 shambani heka moja .
Nyanya zimeanza kutoka maji yakawa ya shida kumwagilia zikadumaa zikaishia kukuua vidogo vidogo vinaiva nikakomaa nikamwaga mbolea wakaingia panya wakala kma robo heka nyanya zote zilizokua zimeanza kua nyekundu
Nikapiga dawa huku na kule ugonjwa mwingine asee nilikuaga naishi km kichaa
Mwisho wa siku nilivuna tenga 9 out of 120 na bei ya kuuzia ikashuka hadi elfu 8 na kwakua nyanya zangu zilitoka ndogo ndogo sana na nyingi zina maginjwa nikauza tenga kwa elfu tano Kati ya 1.2M , muda na nguvu nilizotumia niliambulia elfu 45 tu 🥶
Sent from my iPhone using JamiiForums
Biashara inahitaji uvumilivu wa hali ya juu...nilifanya biashara ya maji na juisi jumla jumla....unaingiza mtaji wa 1m faida alfu kumi. nikafungua book shop huko ndio mtaji ukapotea kabisa.
Una kuku wangap? Na upo mjini au kijijini?
Na shida na za uzazi kwa wanaume.Binafsi biashara yangu ya dawa za nguvu za kiume..dawa wa uzazi za wanawake na kuongeza shape zinaniendea vizuri tu Sina changamoto.
Daaaa!! Kamsamba, umenikumbusha mbali sana, mwaka jana nilikuwa huko, ila daa kutoka hapo mlowo kuitafuta Kamsamba ni shughuri pevu, hizo km 132!! Sio mchezo na kuna poli zito kuna sehemu inaitwa) BOT), kuna kona kali majambazi ndio huwasubilia wafanyabishara na kuwapola pesa!
kiukweli kule kuna mchele mzuri ila kuna sehemu inaitwa MAJIMOTO, ipo mkoa wa katavi(mlele) kule ndio balaa, ni sindano mchele wa kule, na unaweza tokea hapo hapo Kamsamba hadi kule. Nilikuwa kwenye utafiti wa biashara hiyo hiyo ya mchele.
Soma vizuri!! Mimi nazungumzia mpunga ni pasua kichwa ila mchele ndio nzuri, kuna utofauti wa biashara ya mpunga na mchele.
Unauzaje kwa jumla?Ninao 400 nafugia kijijini