Tupeane uzoefu kidogo katika biashara hii ya Ng'ombe

Tupeane uzoefu kidogo katika biashara hii ya Ng'ombe

kitoto wa vitoto

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2019
Posts
375
Reaction score
410
Wakuu wanajamvi poleni na pilika za maisha

Nina mpango wa wa kufanya biashara ya ng'ombe katika mfumo mmojawapo kati ya hii:
  • Kunenepesha (nanunua bei rahisi wakati wa kiangazi nawapa lishe vizuri wakinenepa niwauze
  • Kununua ndama niwatunze wakiwa wakubwa niwapige bei
  • Ninunue mitamba(ng'ombe jike) nawapandisha wakipata mimba nawauza!)
  • Nifuge ng'ombe wa kawaida mchanganyiko
Ipi njia rahisi ya kunipa kipato?
Pia naomba wenye uzoefu mnisaidie mawazo.

Nawakaribisha

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nunua ng'ombe,pakia kwenye fuso kauze,nunua mnada huu,uza mnada ule,nunua mnada huohuo ila nje ya mnada,ingiza mnadani kula Cha juu hata hamsini hamsini,
Hivyo ndo wanafanya wanaotaka kupandisha mtaji chap chap,kuliko ufuge usubiri faida miezi mitatu mbele
 
Wazo jema sana!
 
Nimesoma mara tatu ili kujiridhisha kama nimeelewa swali lako. Kimsingi hapo hakuna option. Hiyo ndo biashara ya kufuga. Kila mfugaji anafanya hivyo vitu kwa wakati mmoja. Kuna ng'ombe utanunua na kukaa nao kama wazazi, kuna ng'ombe utanunua na kuuza n.k. Huo ndo mzunguko wa biashara ya kufuga.

Hapo utaanza na kununua ng'ombe..ndama, mitamba, madume etc. Baada ya muda utauza baadhi na kuonheza baadhi na wengine uta wa keep....mzunguko unaendelea hivyo hivyo.
 
Nunua ng'ombe,pakia kwenye fuso kauze,nunua mnada huu,uza mnada ule,nunua mnada huohuo ila nje ya mnada,ingiza mnadani kula Cha juu hata hamsini hamsini,
Hivyo ndo wanafanya wanaotaka kupandisha mtaji chap chap,kuliko ufuge usubiri faida miezi mitatu mbele
Asante sana mkuu
Je naweza kupata conection zaidi? Naomba kama una uzoefu au unaweza kuniunganisha na mtu mzoefu ili awe mwenyeji wangu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kitoto wa vitoto, Mfumo mmbovu kuliko wote ni wa kununua mnadani na kuuza,Na kununua ndama uje uwalee ndiyo uuze nao hovyo kabisa.
Hapo mpango mzima ni kununua ng'ombe wa Maziwa wenye Mimba na kuwauza.Rudi tena nikupe sababu ya hiyo mifumo mibovu.Nishapita kote huko.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kweli kabisa.Unanenepesha kwa miezi 3.tu!.Zaidi ya hapo ni hasara.Njia hiyo ni rahisi kwa watu wa Kanda ya Ziwa.Ngombe analishwa yale Makapi ya Pamba,siyo Mashudu.Bali Makapi.Ndiyo maana njia hii siyo rahisi kwa mikoa isiyolima Pamba

Sent using Jamii Forums mobile app
Hii unaweza kuifanya ukiwa mikia mingine.
Nilitaka kufanya kitu kama hicho mwaja huu lakini hali ya hewa haikuruhusu.

Nitatoa mfano kwa mkoa wa Manyara; kukiwa na ukame ngonbe wa laki 7 unaweza kumnunua kwa laki 1.5 sasa ukimoeleka mkoa mwingine ambako kuna hali ya hewa nzuri. Baaga ya mwezi moja unapata faida 100% au zaidi. Nina mfano hai wa hili

God save us
 
Back
Top Bottom