Tupeane visa na mikasa ulivyowahi kukutana navyo kwenye pilika za kusaka utajiri

Sitasahau, nilipewa deal na Wazungu fulani kutoka Nairobi Kenya, wakanipa na mtaji wa mabanda kabisa. Wakaniletea vifaranga vya Γ±yoka, na wataalam wa kunifundisha kuwafuga, nikawafuga wakaja baada ya miezi mitatu, wakavuna sumu ya nyoka, na nikapatiwa kiwango kizuri sana cha fedha za kigeni.

Wakaja tena baada ya miezi mitatu mingine, nikalipwa vizuri zaidi ya mwanzo.

Wakanipeleka Nairobi kwenye ofisi zao, kwa gharama zao. Hakika nikaona maisha nimeyapatia.

Waliporudi mara nyingine ikawa ndio mwisho wa kuja kwao, wakaniachia mijoka mingi na nisijue pa kuwaweka.

Siku nikaamua Bora mabanda niya spray petrol nyoka wote wafe.

Hivyo ndivyo ilivyokuwa
 
Pole sana Mkuu hii story umesimulia zaidi ya mala moja inaonekana hili jambo limekugusa sana
 
Mwaka 1992 kwenye kusaka hazina ya mjerumani.. Zile sarafu.. Nilinyonga baiskeli kilometer zisizopungua 20 milima na mabonde kisha nikatembea kilometer 8 Mlimani.. Ni kama nilikuwa naenda mwisho wa dunia
Hatimaye nikafika kwa mhusika babu mzee hasa over 90 yes. Nikamweleza shida yangu naye bila hiana akanitolea chungu kimejaa sarafu za zamani akaniambia nitafute nikipata ninayo hitaji atanipa bure.. Maana kufika tu huko ni adhabu tosha
Nilitumia massa karibia matatu nachambua kwa kurudia nikatoka kapa
Mwisho akaniambia tunaongopewa sana kwakuwa miaka inayotafutwa kwenye hizo sarafu haipo kwakuwa hazikuwahi kuzalishwaπŸ˜­πŸ˜‚πŸ˜­πŸ˜‚
Niliondoka nikiwa hoi mno..
 
Waliokuwa wanatudanganya wao walikuwa wanapata faida GANI?
 
Mkuu siungevuna tu hiyo sumu kuliko kuua mradi kbs
 
Uzi mzuri sana ila kwakua wabongo wengi mawazo yao wamewekeza kwenye kukuna na kunyambua nyapi humu hutawaona kwa wingi
 
Naikumbuka sana hiiπŸ˜‚
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…