Sijapotea,
Nipo sana, na Mungu jalia nitaendelea kuotesha miti zaidi. Kama nilivyosema 2019 nimeotesha pines 150,000 sio za watoto ni zangu mwenyewe mkuu. Baada ya anguko la uchumi tumebaki wachache sana kama tulivyoanza. Idadi inapungua sana ila mimi na wenzangu tuliopinda bado tunaweka vitalu vya miche.
Tunapoona matajiri wa Kiarabu na Kihindi katika nchi yetu, ujue misingi yao ilijengwa muda mrefu sana na waliowatangulia. Fuatilia wote utaona. Natamani uwekezaji wangu uje kukivusha kizazi chang kwenda level nyingine kabisa.