Naam,
Fedha inatokana na shughuli yenyewe. Huwa naanda vitalu vya miche, nauza miche mingi, faida nanunulia mashamba na kuendeleza, kwa hiyo ni uwekezaji unaojiendesha wenyewe. mwanzo nilikuwa nanunua vimisitu vidogo nafuga, akija mteja napiga bei, kwa hiyo vikaniinua sana. Huku nina miche na kule kamsitu kamepata mteja, basi siku zinasonga.
Niko njombe pia napiga parachichi. Nimeangukia pua mara mbili kwenye parachichi, yaaani miche ilikufa sana. Nikagundua miche ya bei rahisi ni hasara. Sasa hivi natumia miche ya bei mbaya, haifi.
Kule Lutukira niliangukia pua kwenye Tangawizi, ile namalizia camping, bei ikashuka vibaya nikaondoka fasta.