Nilipoamua kuingia kwenye hii game nilianza na eka moja na nusu kule Kilolo, Mheshimiwa Mbunge Mwamoto alinipa msaada mpaka kufika kile kijiji na nikapata shamba eka moja na nusu kwa Tsh 22,000/. Nikaagiza hela jamaa wanioteshee, hawakuotesha lote, msimu uliofuata nikakaza buti mwenyewe, nikamalizia kipande, yaani miaka miwili nikaotesha eka moja na nusu.
Wakati wote nilikuwa nasoma game kwa madogo na wenyeji. Nilipolijua game, nikawatimulia vumbi kwa speed ya 120km/h. Imebaki historia pale kijijini. Huwa nawapitia siku nikienda kukagua misitu, basi kukiwepo maji tunakunywa.