Tupeni mrejesho mliowekeza kwenye mashamba ya miti

Umesahau swala la moto pia linaweza tokea hapo. Biashara ngumu sana.
 
Thread closed....
 
Ulipotea sana,
Huku uwekezaji huu wanasema ni kwaajili ya watoto
Sijapotea,
Nipo sana, na Mungu jalia nitaendelea kuotesha miti zaidi. Kama nilivyosema 2019 nimeotesha pines 150,000 sio za watoto ni zangu mwenyewe mkuu. Baada ya anguko la uchumi tumebaki wachache sana kama tulivyoanza. Idadi inapungua sana ila mimi na wenzangu tuliopinda bado tunaweka vitalu vya miche.

Tunapoona matajiri wa Kiarabu na Kihindi katika nchi yetu, ujue misingi yao ilijengwa muda mrefu sana na waliowatangulia. Fuatilia wote utaona. Natamani uwekezaji wangu uje kukivusha kizazi chang kwenda level nyingine kabisa.
 
Umesahau swala la moto pia linaweza tokea hapo. Biashara ngumu sana.
Mimi nimewahi poteza eka 350 za miti ya mbao na nguzo kwa msimu mmoja yenye miaka mitano. Lakini msimu uliofuata nikaotesha zaidi ya hizo. Nilichofanya ni kutafuta sababu ya moto ule. Nilijua chanzo chake nikarekebisha na nina songa mbele.
 
Uwekezaji huu ilikuwa dili xana kipindi cha awamu ya nne ....kama unafanya saizi uwe huna hera kwa kupeleka lkn unafaida xana wengi waliwahi kuwekeza wametoka kimaisha .
Mpaka leo ni deal zuri, sasa hivi ukitembea kwenye misitu binafsi Kilolo, Mufindi na Njombe hupati mti hata mmoja wa kupata mbao za 1x12 au 1x10, sana sana ni 1x8. Kwa hiyo siku chache mbeleni huko watatokea wababe kwenye hii biashara na itakuwa haishikiki tena, sababu wengi wanakimbia na wengi wanashindwa kutunza mashamba.

Nimesema mapema, usiingie huku kama una hela za mawazo. Utashindwa kutunza msitu wako bure.
 
Hapo kwenye changamoto hebu fafanua zaidi mkuu.
Changamoto ya kwanza ni ardhi salama kwa kilimo hiki.
Changamoto ya pili ni manpower kwa ujumla wake
Changamoto ya tatu ni sera za nchi yetu
Changamoto ya nne ni miundombinu isiyo rafiki sehemu zenye ardhi nzuri na salama.
Changamoto ya tano ni hujuma inayotokana na sbb nyingi
Changamoto ya mwisho kipato kuyumba kwa wawekezaji.
 
Mimi nilipanda mikaratus ( milingoti) na kipindi hicho napanda ilikuwa Haina soko ,watu wengi walikuwa wanapanda miti aina ya pine, nikaamini kuwa mpaka ikomae itakuwa na soko huko nyumbani kwa sabab watu wengi walikuwa wanapanda aina ya pine.saiz nishaanza kupokea simu zinazotaka niuze na Mimi nalinga Sasa kwasababu tuko wachache wenye nayo. Sina haraka nayo Bado napambana na maisha kwa njia zingine Kwanza nimeiweka akiba Kama bomu la nuclear siku nikilipua itani boost Sana kiuchumi
 
Uko vizuri,
Nilipokuwa chuo, niliotesha miti 250 tu nyumbani kwetu, sasa hivi nasumbuliwa mno. Nimewaambia ile nimeiacha kwa ajili ya dharula maana ni hela kiganjani sio benki ukute ni jumamosi hawafungui, yaani nikiinua simu tu, mpunga ndani maana ndo imebaki hiyo tu iliyokomaa. Kila siku Wachina wa Mafinga wanapitia vimisitu vyetu kupitia madalali wao, nasema bado sana. Jirani yangu juzi kavuta mpunga wa maana pale Mapanda, kauza kwa mchina vigogo, miye bado kwanza.
 
Mimi nimewahi poteza eka 350 za miti ya mbao na nguzo kwa msimu mmoja yenye miaka mitano. Lakini msimu uliofuata nikaotesha zaidi ya hizo. Nilichofanya ni kutafuta sababu ya moto ule. Nilijua chanzo chake nikarekebisha na nina songa mbele.
Safi na hongera kwa juhudi, muhimu umejua tatizo na umejipanga kwa asiyejua tatizo bado ni changamoto kubwa kwake.
 
Hongera sana, naona mambo ya fedha yamekunyookea mpaka kufanya uwekezaji huu.

Mimi nimesitisha shughuli zangu zote na sasa nipo kwenye kilimo mazima 100%. Kuna potential kubwa sana huku iwapo utapata access ya masoko na bei za uhakika. Njombe, iringa, mbeya neema imefunguka tushindwe wenyewe
 
Mimi nimewahi poteza eka 350 za miti ya mbao na nguzo kwa msimu mmoja yenye miaka mitano. Lakini msimu uliofuata nikaotesha zaidi ya hizo. Nilichofanya ni kutafuta sababu ya moto ule. Nilijua chanzo chake nikarekebisha na nina songa mbele.
Pole sana, wewe ni mbishi.. nimependa hii spirit
 
Mimi nimewahi poteza eka 350 za miti ya mbao na nguzo kwa msimu mmoja yenye miaka mitano. Lakini msimu uliofuata nikaotesha zaidi ya hizo. Nilichofanya ni kutafuta sababu ya moto ule. Nilijua chanzo chake nikarekebisha na nina songa mbele.
Hongera mkuu kwa mentality hiyo.... hii biashara inahitaji mtu ambar hataki pesa za haraka haraka na anazo pesa za kutoa tu bila kuingiaza for a long time....
uwe na mishe zingine za kuingiza pesa....

Endelea kupambana mkuu all the best
 
Pole sana mdau moto ulitokana na nini?

Uwekezaji wa miti ni rahisi sio mpaka uwe na milion 500 pata ardhi Hata kama ni haka 2 anza Utapata hamu na uzoefu a long the way. Lakini usipoamua kuanza kwa kusikiliza wakatisha tamaa kwa excuses mbalimbali. Alafu usisikilize watu ambao wanatoa ushuuda wa watu wengine. Ongea na wasikilize waliokwenye game (hii ni katika venture yoyote ile. Get started kwenye maisha hamna kuchelewa ukikumbuka umewahi
 
Shukran mkuu ngoja tujipange tuingie deep zaidi
 
Shukran mkuu ngoja tujipange tuingie deep zaidi
Katika maisha kanuni za kutoboa kila mmoja ana mikaksti yake ni vile maono yake ,,, kilimo cha miti kinatoa watu na wengine kinawaangusha ...
Katika hayo yote nimejifunza kitu kimoja unapoamua kufanya jambo lolote
=== Fanya kwa ukamilifu na ustadi utafanikiwa
 
Sehemu gani!?
 
Skeleton makini HIZI... Zimekosa nyama tuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…