King Mutesa
JF-Expert Member
- Aug 23, 2012
- 227
- 141
Hata ekari moja sio mbaya,kimfaacho mtu chakeTatizo lako una panda ekari 2 . Miti ukitaka udaidi panda kuanzia ekari 50.
Imagine 50×400= unakua na miti 20000.
20,000x20000= 400,000,000
Hii ina maana kila baada ya miaka 10 unavuna mil 400
Sent using Jamii Forums mobile app
Mjadala hapa ni changamoto za gharama za utunzaji, moto nk gharama za kuhudumia acre 50 kwa miaka 15 si lelemama kwa mtanzania!Tatizo lako una panda ekari 2 . Miti ukitaka udaidi panda kuanzia ekari 50.
Imagine 50×400= unakua na miti 20000.
20,000x20000= 400,000,000
Hii ina maana kila baada ya miaka 10 unavuna mil 400
Sent using Jamii Forums mobile app
Malila ulini- inspire sana kny miti bless up, moto ni changamoto kubwa sana lakini mapambano yanasonga mbele.
Ushauri mzuri sana.Kuna kitu kinafikirisha sana,
Week iliyopita, kuna mteja ana hela kiasi anataka kununua miti kwa Tsh 2.5M kwa eka. Nikamwambia jamaa yangu mmoja ana eka 40 pale Igeleke Mufindi. Nikampa hesabu hizi, Chukua hiyo 100,000,000/, atoe 12,000,000/ gharama za uwekezaji. Kisha achukue 50,000,000/ anunue shamba lenye miti midogo ya 5yrs hivi, na atoe kama 10,000,000/ matunzo ya shamba jipya. Hizi 28m twende samaki samaki tukafanye yetu, hataki. Nikamkumbusha habari ya moto, asije kuja hapa kutulilia.
Wewe ungemshaurije? Maana yy anataka bei ifike 5m kwa eka apate 200M hivi akachukue Hammer kabisaaaaaa.
Ustake chai inipalie,Ushauri mzuri sana.
Tatizo unachoona wewe sicho anachokiona yeye.
Hivi ushafikisha eka ngapi za miti?
Sent using Jamii Forums mobile app
Malila. Habari Mkuu!!Hamjambo jamani, kuna hii biashara ya Utomvu wamekuja nayo wachina kule Mafinga. Wanagema utomvu kama Ulanzi kwenye miti ya pines. Utata uko kwenye bei, wanunue kwa kilo au kwa mti? niliwashauri wanunue kwa kilo. Ikikubalika basi tutaanza kula miti yetu kuanzia miaka saba. Unagema utomvu na kujipigia hela kiulaini kabisa. Mchina hajaacha kitu
Mkuu.Ustake chai inipalie,
piga ua galagaza sisemiiiiiiiii, we jua kila mwaka naotesha miti sana, basiiiiii.
Hizi hesabu zimefelisha wengi kwenye matikiti...
Huu utomvu wakigema miti haikauki?Hamjambo jamani, kuna hii biashara ya Utomvu wamekuja nayo wachina kule Mafinga. Wanagema utomvu kama Ulanzi kwenye miti ya pines. Utata uko kwenye bei, wanunue kwa kilo au kwa mti? niliwashauri wanunue kwa kilo. Ikikubalika basi tutaanza kula miti yetu kuanzia miaka saba. Unagema utomvu na kujipigia hela kiulaini kabisa. Mchina hajaacha kitu
Mkuu.
Leo nilikuwa naongea na mtu kuhusu mradi unaosimamiwa na Kilombero Teak Company.
Unapewa miche halafu wakati wa kuvuna wanakupa chako.
Ushawahi sikia huu mradi? Nini maoni yako.?
Sent using Jamii Forums mobile app
Mosi; kuna changamoto ktk uwekezaji huu, usiweke hela kwenye miti kama cash flow yako ni ya mawazo sbb unaweza kuambulia majivu.
Sio uwekezaji wa muda mfupi, ili upate faida ni lazima uende zaidi ya miaka 15 mpaka 23 hivi. Aina ya miti na scale ni muhimu sana kuijua ili kufikia malengo.
Pili; mabadiliko ya sera, anguko la uchumi kwenye jamii linaathiri sana uwekezaji huu.
Tatu; kwa wenye pumzi huu ni uwekezaji mzuri kama sector nyingine.
Miaka 15 sio mchezo,hakuna miti inayokua kwa haraka?
Mkuu kuna aina ya miti inaitwa GMELINA ARBOREA (kitaalam) ama white teak/teakmaji ni aina ya miti inayomea fasta (10yrs) na vizuri huku pwani(kisarawe) vipi kwa ukanda huo umewahi kuiskia/kuiona ...Ipo mkuu, unapata. ila mbegu hutoka Zimbabwe mara nyingi
Hapo ni miti mingapi kwa kila acre?Nina 5 acres miaka 7 sasa