Tupia jina la memba mmoja wa JF ambaye katoweka humu

Tupia jina la memba mmoja wa JF ambaye katoweka humu

Nimefurahi kukuona tena.. Ila wengi tunahitaji sana michango yako kwenye jukwaa la intelligence
Asante sana kwa heshima hii nisiyostahili uliyonipa.

Hata ningestahili heshima hiyo, bado naona changamoto nyingi.

Changamoto kubwa imekuwa ni kufuta nini kisichotakiwa kusemwa kutoka nini kinachotakiwa kusemwa (redaction). Kwa sisi tusiotegemea magazeti, unaweza kukaa na mzee wako yuko barazani (la mawaziri) akaongea nawe kama mazungumzo ya familia, wewe ukahamaki kesho ukayaelezea hapa isivyofaa, unaweza kuhatarisha usalama wa watu wasio na hatia.

Nyingine ni kusema kwa staha itakayohimiza na kutunza heshima katika ulimwengu ambao hauna heshima hata kwa wenye heshima. Ni vigumu kusemezana sana na watu wengi, hususan kama wengine hawajui kanuni za kusemezana kwa staha hata ndogo tu ya kujuana na kuheshimiana kama jamaa moja angalau kwa uraia.

Kijamii, kwa upande, hatujawa na utayari kwa habari zenye ukweli unaohitajika. Upande mdogo ambao tumepata huo utayari hatujawa na mipango ya kuendeleza hizo habari zikishapatikana.

Ndiyo maana nikiongea na ahali zangu fulani wanaojua yanayoendelea kwa undani, wanashauri kuendeleza biashara zetu na ustawi wa familia ughaibuni tu.

Maana nikiangalia email za balozi za Tanzania nje mpaka mazungumzo ya watu wa ndani ni shida.

Na hapo kuna wazee wangu nawaheshimu wanaendesha mambo.

Inaelekea ufahamu ni bidhaa adimu.

Na kulazimu adimu ni wazimu.
 
Back
Top Bottom