Tupia vimbwanga vya siku ya mtihani wa darasa la saba

Tupia vimbwanga vya siku ya mtihani wa darasa la saba

Dah mtihani wangu wa darasa la saba sikuufanya kwa amani kabisa. Nilikua ka-bwana mdogo mno ( mfupi) hivyo kupelekea watu wanishangae sana nnavyopita mitaani kwenda shule kufanya mtihani.

Ilinibidi niwe napita 'chocho kwa chocho', stendikuu- jakaranda- mto meta- mbalizi road ili kukwepa 'macho' ya watu sababu ya kuonea aibu maneno ya wanaonitania njiani.
 
Rubber band zilitumika sana kutransfer chabo (unaweka kikaratasi kwenye rubber band kisha unamlenga mhusika), msimamiz alikuwa zake bize anasoma gazeti la michezo[emoji4] [emoji1]
[emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] duu noma sisi tulikuwa tunabadilishana booklet inamjazia ukimaliza unarudisha
 
Ninachokumbuka tulichanga pesa baada ya msoto wa uji. Hatimae ktk mtihani tulikula nyama saana. Na wadada walivyokua wananipenda. Basi nyama nyama sana. Tu. Sisis usafi tulipiga deki mpaka madirisha nakumbuka. Ila chuo balaa jamani. Hakuna misala kama chuo. Mtu anakimbia kama bolt.
 
mimi baada ya pepa jioni nilienda kibanda umiza kuangalia video, nilichezea kichapo heavy toka kwa mama sitasahau
 
Kitu ambacho sikielewi ni kwa nini mitihani ya darasa la saba ilikuwa na askari wengi?

Form askari wachache, form six askari wachache.
 
Maajabu mengine sio ya kusimulia, mm sikuwahi kushika no moja au mbili darasani. niliwahi kuwa wa 5, 6 siku nyingine 11, etc lakini cha kushangaza darasa zima tulishindaga wasichana 4 ndo tulifanikiwa kwenda sec school ahaaaaa
 
Darasa la saba tulinunua majibu kwa shilingi 15,000/-, mimi nikakubaliana na jamaa niliyekaa naye dawati moja snipe 5,000/- nimpe majibu yote.

Tulifanya paper zote na nilimpa majibu yote ila hakunipa hata 100, akamwambia mzee wake, mzee wake akamwambia baba, baba akaja kunibana nikamwambia ilibidi nifanye hivyo kwa sababu zile karatasi za majibu zilikuwa zikiletwa wanaziona na alitishia kunisema.

Matokeo yalivyotoka jamaa hakufaulu, tuliofaulu ni wale tuliotoa hela peke yake, akaanza kulalamika kwamba nilimpa majibu ya uongo, nikamuuliza ulitoa sh ngapi?

Kitu ambacho sielewi mpaka leo ni kwa nini tuliowapa majibu hawakufaulu wakati tumejaza sawa sawa.
 
wakati nimemaliza mtihani wa hesabu nasubiri kukusanya alidondoka bonge la mjusi akadondokea answer sheet
 
Teh teh umenikumbusha mbali sana nilikuwa kwenye mtiahani wa sayansi kunamaswali nilikosa majibu yake nikachana karatasi nikaandika maswali niliyo shidwa nikampupia jamaa angu frani iv si msimamizi akaona mchezo ulivofanyika nilifuatwa nilipewa kofi moja tu afua akachukua lile karatasi akalichana baada ya apo akaondoka zake ila nashkru saiv nimemaliza chuo kikuu nafanya kazi.......kweli maisha nisafar...... pia katika kipindi hicho hicho tulikuwa tunafanya mtihani wa hesabu kuna jamaa mmoja alikuwa anaakili ni balaa( kipanga wa darasa) alifanya maswali 48 kati ya 50 mda ukawa umeisha siakanza kulia hajamaliza paper unajuani jamaa(kipanga) nilimshanga kwa sababu mimi nilishia swali la 39 au 40 nilijisiakia fresh tu....Mungu mkubwa jamaa baada ya apo tukakutana advance ananishanga nimefikaje apo wote tukaenda chuo baada ya kumaliza sijui yupo wapi saiv
 
Nakumbuka tukikuwa tunaenda na vyakula sababu shule hazikuwa na uwez ku afford chakula na kipindi kile mtihan ni siku moja, so nakumbuka nilinunukiwa skonsi na fanta kwa vile ni vitu adim kukutana navyo nilivyipiga asubuhi ile ile baadae mchana had kumalizia mtihan ilikuwa masoto sana....nilifaulu second selecton lakin..!

Maisha hatua
 
Hahahaaaa. Ila umenikumbusha mbali maana na sisi ilikuwa vivyo hivyo enzi hizo na pia kuna ile ya kubandikiwa namba ya mtihani iliyoandikwa kwenye kipande cha karatasi nyeupe iliyowekwa gundi pembeni ya dawati upande wa kulia sijui kushoto.
 
Back
Top Bottom