Darasa la saba tulinunua majibu kwa shilingi 15,000/-, mimi nikakubaliana na jamaa niliyekaa naye dawati moja snipe 5,000/- nimpe majibu yote.
Tulifanya paper zote na nilimpa majibu yote ila hakunipa hata 100, akamwambia mzee wake, mzee wake akamwambia baba, baba akaja kunibana nikamwambia ilibidi nifanye hivyo kwa sababu zile karatasi za majibu zilikuwa zikiletwa wanaziona na alitishia kunisema.
Matokeo yalivyotoka jamaa hakufaulu, tuliofaulu ni wale tuliotoa hela peke yake, akaanza kulalamika kwamba nilimpa majibu ya uongo, nikamuuliza ulitoa sh ngapi?
Kitu ambacho sielewi mpaka leo ni kwa nini tuliowapa majibu hawakufaulu wakati tumejaza sawa sawa.