snowhite
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 18,065
- 24,559
Huwa nina shida ya kukinai chakula,so nataka tushee recipes tofauti za mchele!
=======
SWEET CHOC RICE
Mahitaji:
-Mchele kg1
-Karoti tatu
-Asali vijiko vitatu
-Vanilla ya maji(kijiko kidogo) ikiwa ya unga nusu kijiko
-Zabibu kavu
-Korosho au almond au karanga zilizokaangwa na kutolewa maganda
-Choc powder vijiko vitatu (vikubwa)
Jinsi ya Kupika:
Kaanga mchele na viungo vyote except choc powder na asali.
Weka maji baridi acha uive, geuza mara moja kisha punguza moto, acha ukauke maji.
Kabla ya kuupalia au kuweka kwenye oven koroga choc powder kwenye kikombe(iwe nzito so maji ni kidoogo), kisha mwagia huo wali katikati, funika palia!
Kabla ya kupakua nyunyiza asali, itajichanganya utakapokuwa unapakua.
Serve na mboga uipendayo.
=======
WALI WA UFUTA
Mahitaji:
-Ufuta kikombe kimoja
-Mchele kg 1
-Nazi mbili
-Hiliki
-Maji
-Chumvi
Jinsi ya Kupika:
Kuna nazi zako kisha tenganisha kabla ya kuchuja, kisha chuja kwa kuweka maji ya vuguvugu kidoogo kidogo maliza kundi la kwanza kisha kundi la pili hivyo hivyo mpaka upate kiasi cha maji ya kuivisha wali wako.
Andaa ufuta kwa kuuloweka kisha uuengue ili usiwe na mchanga.
Rudi jikoni kuangalia tui lako, hakikisha halichemki kiasi cha kutengana pale juu, toa wengu(chukua kijiko kipana engua lile tui,, zito la juu hakikisha hulichanganyi na maji ya chini), liweke pembeni.
Weka hiliki, chumvi na mchele, funika wacha viive.
Wakati wali unaiva, chukua mafuta yachemke jikoni kaanga ufuta, usiungue!
Geuza wali, punguza moto.
Kabla ya kuupalia au kuweka kwenye oven, weka ufuta uliotoa kwenye mafuta, changanya kisha mwagia lile tui zito, kisha palia wali wako au weka kwenye oven, moto uwe mdogo ili usikauke bali tui lile libaki utamu wake!
After 5-10 minutes wali wako tayari, serve na chochote.
=======
WALI WA RANGI
Mimi huuita mini-biriani manake nimevunja na kupaste some of the biriani tips, so kwa wale ambao biriani inazingua, try this!
Mahitaji:
-Rangi tatu(preferebly Green, Red, na Njano)
-Mchele (kwa kiasi chako)
-Vanilla syrup au powder (ikiwa syrup vijiko viwili vidogo, ikiwa powder nusu kijiko)
-Nyanya tano
-Tomato sauce vijiko viwili
-Vitunguu vikubwa vitatu, kata kwa urefu
-Karoti mbili kubwa kata kwa urefu
-Royco vijiko viwili vikubwa
-Hiliki iliyosagwa vijiko viwili
-Zabibu kavu nusu kikombe
-Nyama ya kuku, ng'ombe, kondoo, mbuzi poa (fanyia marination mapema) kumbuka kuku, mbuzi vinaiva fasta so unaweza tengeneza rost yake moja kwa moja bila kuchemsha, but ng'ombe hasa hawa wa vingunguti nakushauri uchemshe.
-Tui la kwanza la nazi mbili(yawe mazito hasa, usijali uchache wake, still yatakupa best results)
Jinsi ya Kupika:
Weka mafuta jikoni kaanga mchele na zabibu kavu, vanilla essence geuza mpaka uridhike viko poa. Weka chumvi weka maji baridi, funika.
Katakata nyanya, vitunguu, karoti, vyote changanya kwenye nyama uliyoimarrinate, kisha chemsha mafuta, Weka vyote kwa mara moja, (no kusubir kitunguu kiwe Brown) mix vyote, acha vijipike usifunike.
Rudi kwa wali wako, geuza mara moja, punguza moto ubaki unaiva taratibu.
Chukua rangi moja, (kila rangi robo kijiko) mix na maji (naasume ni za unga)
kidogo kisha koroga (kila rangi na kikombe chake).
Wali utakuwa umekauka vizur by now, mwagia zile rangi kwenye wali kwa patterns like mstari mmoja red, unawafata Green, the following njano, nenda hivi mpk rangi ziache,pishanisha ili ubaki na white pia.
Weka kwenye oven, au wale wa mkaa palia.
Rudi kwa rosti yako, utageuza mpk uone viungo vyote vimepotea like one can not tell hiki ni kitunguu na hii ni nyanya, ikifika hapo weka royco, hiliki, geuza geuza tena, chukua bakuli la kwanza la tui bubu mwagia kwenye mboga yako, geuza tena, ikae dk 3,kisha weka tui lingine, iache dakika 3 pia! ipua!
Wali wako now will be done, nenda ugeuze geuze mix mpk upate four colors at a one look, yani usiache rangi moja iwe dominant mahali.
Iko tayari hapo, serve, pakua wali kisha rosti pembeni!
hihihi unaweza kurusha insta baada ya upakuzi huo!
Enjoy!
=======
MSETO WA CHOROKO, KUNDE, DENGU (Chagua kimoja)
Mahitaji
-Mchele (kwa kiasi chako)
-Nafaka uliyochagua (ratio iwe kg 1:1/2 nafaka)
-Nazi/maziwa fresh
-Vitunguu maji
-Tangawizi
-Chumvi
-Maji
Jinsi ya Kupika:
Pika kunde, maharage, DENGU, choroko viive.
Andaa mchele.
Twanga au kereza tangawizi, vitunguu vikate pia, vile saumu viponde.
Bandika jikoni sufuria la tui la nazi (fata process za tui kama nilivoelekeza kwenye pishi la mini biriani), kama ni maziwa yachemshe pia.
Kisha bandika mafuta jikoni kaanga vitunguu saumu, kisha vitunguu maji, kisha tangawizi, kisha weka nafaka yako, geuza kama mara tatu kisha weka mchele uliokoshwa, geuza pamoja vichanganyike.
Weka tui lililochemka(lile la chini) wengu lake liache kwanza. Kwa anayetumia maziwa pia ataweka kwa stage hii geuza kisha funika uive.
Utaacha ukauke geuza mara moja, punguza moto.
Utageuza tena, palia au weka kwenye oven, after 5 mins uko tayari.
Serve na salad of your choice, mi hupenda nda kuila na guacamole (parachichi lililopondwa likachanganywa na white vinegar na nyanya zilizokatwa cubes ndogo ndogo)
Enjoy.
=======
VEG RICE
Mahitaji:
-Mchele (kwa kipimo chako)
-Karoti
-Broccoli
-Vitunguu vichanga
-Red cabbage
-Vanilla(ukipata ile ya kienyeji unprocessed) poa zaidi, ulizia masokoni ipo
-Green beans
-Sweet corn, vijiko vitano
-Mafuta (ukiweza kuufanya steamed au boiled poa zaidi) ila mchele uwe the most super. vinginevyo tumia tu mafuta
Jinsi ya Kupika:
Andaa mchele.
Chemsha maji.
Bandika mafuta kisha kaanga mchele ukiwa umeweka vanilla kaanga vizuri, Weka chumvi, Weka maji, geuza funika uive.
Osha na kata mboga mboga zote kwenye bakuli moja, broccoli ikate kwa kufuata pattern yake ya kitawi kimoja kimoja, vimix vikiwa vibichi, uone rangi zote at a single glance.
Funua wali, Weka mboga zote hapo juu, funika kwa dakika tano, kisha geuza wali wako hakikisha ziko mixed na wali vizuri.
Funika, punguza moto, after five mins ipua.
Serve na juice, chai, maziwa.
=======
UJI WA MCHELE
Mahitaji:
-Mchele (Kiasi ukitakacho)
-Maji
-Maziwa fresh
-Blueband
-Sukari/Chumvi (Inategemea na unachopenda)
Jinsi ya Kupika:
Andaa mchele, usafishe ipasavyo.
Weka jikoni na maji kiasi.
Ongeza chumvi/sukari kutegemea na unachopenda.
.
Acha kwa muda hadi mchele uive sana na maji yaishe.
Ongeza maziwa fresh na blueband kidogo.
Kama ni mpenzi wa viungo waweza ongeza hiliki ya unga kwa harufu nzuri.
Koroga ili vichanganyike vizuri na kuwa laini zaidi.
Acha maziwa yachemke pia, kuwa mwangalifu isiungue kwa chini, itakuwa na harufu mbaya.
Shusha tayari kwa kuliwa.
Wepesi wa uji uzingatie umri wa walaji, kama ni watoto wadogo sana, iwe nyepesi na laini sana, punje zisije mkaba kooni.
Ni lishe nzuri kwa watoto, hasa sie tunaowaacha na ma hg, walau kina kaa tumboni kwa muda, hata akimsahau sahau ana survive.

Last edited by a moderator: