Chaliifrancisco
JF-Expert Member
- Jan 17, 2015
- 26,021
- 79,710
Mimi kama Mtanzania mwenye nia nzuri na malengo na hii nchi japo nimetamani kuikimbia na nimepata nafasi kadhaa ila nikaamua kubaki naomba kupendekeza ofisi za serikali na bunge zianze kupima pombe na madawa ya kulevya.
Hii itasaidia kuondoa wafanyakazi na wabunge ambao wanafanya maamuzi ya kipuuzi ambayo mwisho wa siku yana madhara ya kudumu kwa walipa kodi wa nchi hii.
Akikutwa mtumishi na BAC (Blood Alcohol Concentration) ya zaidi ya 0.02 wakati anaingia kazini au akiwa kazini basi ni termination bila warning yoyote.
Na ikitokea mfanyakazi iwe waziri au balozi wa nyumba kumi amefanya maamuzi yasiyo sahihi au yakuleta maswali apimwe pombe na pia mkojo kugundua kama anatumia madawa ya kulevya.
Kuna kampuni za kigeni zinazingatia haya kwa kujali usalama mahali pa kazi. Je sisi kama watanzania tunashindwa nini? Kwani breathalysers ni bei gani? Je ni bora kununua hizo breathalysers au kuendelea kuliteketeza taifa?
Mtumishi wa umma ama mbunge anaingia kazini/bungeni akitokea bar saa 12 asubuhi je huyu atafanya maamuzi sahihi kwa taifa letu?
Naomba serikali ije na mpango huu kambambe ili tupunguze wasiokuwa na akili serikalini na taasisi zake pamoja na bunge.
Tuwapime pombe na madawa ya kulevya. La sivyo tutaendelea kupiga hatua kurudi nyuma.
Nawakilisha.
Mwananchi aliechoshwa.