Tupime thamani ya pesa hapa (Value for Money) Je, Maslahi ya Mbunge yanaakisi hali halisi ya mwananchi wa kawaida?

dmkali

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2014
Posts
11,793
Reaction score
22,552
MASLAHI YA MBUNGE:

- Mshahara: TZS 3.8M kwa mwezi
- Shangingi la kutembelea (wanakopeshwa bei chee)
- Posho ya mwezi: TZS 8M kwa mwezi
- Posho ya Kikao: TZS 240K kwa siku
- Posho kujikimu: TZS 120K kwa siku
- Pensheni: TZS 240M baada ya miaka mitano
- Bima ya afya ya daraja la kwanza kwako na familia yako
- Safari za nje
- Mshahara hauna makato ya Bima ya afya wala mifuko ya hifadhi ya jamii.

Je; Thamani ya shilingi (Value for Money) inaendana na majukumu ya MBUNGE? Tiririka maoni yako!
 
Hii ndio Tanzania , unaambiwa kama ubunge una maslahi gombea na wewe
hatuwezi wote kuwa wabunge! Nani atajenga madaraja, Nani atalima, Nani atajenga minara, Nani atakulinda wewe ....hapa tunaangalia keki ya Taifa je inatumika ipasavyo?
Ebu piga hesabu idadi ya majimbo inchi nzima 264 zidisha kwa pesa hiyo! Ni kiasi gan Cha pesa kinapotea?
 
Tuwaombe wabunge wapunguze posho zao angalau jumla wapate 5M. Kuna watumishi wengine wanalipwa 3.5k au pungufu na hawana posho, wanalipa kodi ya nyumba, wanalipia huduma za maji na umeme, hawana bima kama wanayo baadhi ya matibabu hawapati. Wabunge wa awamu ijayo nahisi si walafi watapenda wengine nao wawe na mishahara minono, huduma nzuri za kijamii na matibabu kwa bei nafuu au bila malipo
 
sijui Kama huruma hiyo wanayo! just imagine Mambo Kama haya yanachangia hata wachungaji wanaacha kondoo kwenda kugombea!
hawajui kwamba Hata Mbunge na waziri Ni muumini (kondoo) maanake ASKOFU Ni mkubwa Kuliko Mbunge
 
Hiki ndicho kinasababisha watu wengi wakimbilie huko na ndio maana awam hii watu wengi wamejitokeza kutia nia ya kugombea kiukwel inaonyesha huko kuna mpunga mkubwa na fursa kede kede
 
hatuwezi wote kuwa wabunge! Nani atajenga madaraja, Nani atalima, Nani atajenga minara, Nani atakulinda wewe ....hapa tunaangalia keki ya Taifa je inatumika ipasavyo?
Ebu piga hesabu idadi ya majimbo inchi nzima 264 zidisha kwa pesa hiyo! Ni kiasi gan Cha pesa kinapotea?
hakika kiasi hicho cha pesa kinapotea...output ni ndogo sana sana!.

swali, tunatokaje hapa sasa????.
 
Back
Top Bottom