Tupo kwenye nchi Ambayo inawzalishaji wengi lakini walaji wachache!

Tupo kwenye nchi Ambayo inawzalishaji wengi lakini walaji wachache!

Prof_Adventure_guide

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2023
Posts
533
Reaction score
1,499
Kuna hali ya ndani inayokua kimyakimya katika taifa letu, hali inayosababisha movement nyingi lakini progress ndogo. Wengi wetu tumejenga maisha yetu juu ya misingi ya kujituma, kutumika, na kutoa huduma halisi kwa taifa. Tunazalisha kwa mikono, kwa akili, kwa muda, na hata kwa ndoto. Tunaamka mapema, tunasimama majukwaani, maofisini, mashambani na mitaani, tukiwa na imani kwamba jasho letu litazaa thamani. Lakini tunapoyatazama matokeo, ni kama tumebaki kuwa background ya system inayowaridhisha wachache. Kile tunachokizalisha kwa wingi, kinatafunwa na watu wasio na mchango wa moja kwa moja beneficiaries of the system, not contributors to the cause.

Hii huzaa hali ya inner conflict! mtu anaonekana yupo vizuri, anafanya kazi, anatoa huduma, lakini ndani yake kuna huzuni ya kimya, ya kutotambulika, ya kuona matunda ya kazi yake yakihamishiwa kwa wale waliokaa pembeni ya mapambano. Taratibu, tunajikuta tunaishi katika loop ya emotional exhaustion, siyo kwa sababu kazi ni nyingi, bali kwa sababu hakuna uwiano wa heshima na matokeo. Wale wanaofanya sana, wanabaki na very little; wale wanaofanya kidogo au chochote, wanashika makubwa. It's a distortion of fairness, mfumo usiozingatia merit bali proximity to power.

Ukweli mchungu ni kuwa taifa limekuwa kama kiwanda kinachotegemea nguvu ya wengi, lakini soko lake ni midomo ya wachache. Wananchi wamebeba mzigo wa uzalishaji, lakini wamekuwa wasindikizaji tu wa ulaji. Na huku juu, wale waliokalia meza ya maamuzi hawasikii tena kelele za chini, kwa sababu mfumo tayari umewapa comfort ya detachment. Hawana tena connection na reality ya maisha ya watu wanaowatumikia. Wako busy na language ya fursa, ajira, uwekezaji lakini ground ni tofauti. Wako wanaoishi kwa hope tu, si kwa outcome.

Na kinachouma zaidi, siyo tu kukosa fursa, bali ni ile hali ya kuona kila unachofanya hakijengi chochote kinachogusa nafsi yako. Unakuwa mzalishaji wa maendeleo ya wengine, lakini si ya kwako. Kuna aina ya ukimya unaoenea—ukimya wenye machungu ya ndani, ambapo watu wameamua kusonga mbele kimwili, lakini wameacha mioyo yao nyuma. Wamejifunza kutabasamu bila sababu, kukubali bila kuuliza, na kuishi bila matarajio. Survival has replaced ambition.

Taifa linahitaji siyo mabadiliko ya sera tu, bali realignment ya values. Tunahitaji mfumo unaotambua kuwa kila anayezalisha, anastahili kuonja. Kwamba maendeleo hayapaswi kuwa privilege ya wachache bali reflection ya juhudi za wote. Hii siyo tu kuhusu uchumi, bali kuhusu dignity kuwa mwananchi siyo tu kuwa mkazi, bali kuwa sehemu ya maamuzi, sehemu ya ulaji wa haki, na sehemu ya ndoto ya taifa. Maana hakuna maumivu makubwa kama ya kuona nchi inakua juu ya jasho lako, lakini maisha yako yanabaki kusinyaa.
 
Notes nyingi, ila umeeleweka maana jamaa kampelekea moto sana!!
 
Back
Top Bottom